PostGE2025 Prof. Patrick Lumumba: Ningependa kuona Lissu akiachiwa

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,131
Mwanamajumuiya wa Afrika kutoka Kenya, Prof. Patrick Lumumba, amesema hatua za awali alizoziona kutoka kwa Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassana ikiwamo kumuelekeza Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kupitia mashauri ya vijana mbalimbali waliokamatwa kutokana na maandamano yaliyoambatana na vurugu Oktoba 29, 2025, kwa lengo la kuyafuta ni dalili za mabadiliko chanya lakini akasisitiza kuwa juhudi hizo hazijatosha kurejesha utulivu wa kisiasa Tanzania.

Akizungumza na Diamond TV ya Zambia, Prof. Lumumba ambaye pia ni mwanasheria na mwandishi wa vitabu amesema hatua muhimu zaidi inayotakiwa ni kuachiwa kwa kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu, ambaye anakabiliwa na tuhuma za uhaini. “Ningependa kuona jambo kubwa zaidi…ningependa kuona Tundu Lissu akiachiwa,” amesema akisisitiza kuwa kuachiwa kwake kutafungua njia ya maridhiano ya kitaifa.

Lumumba ameongeza kuwa Rais Samia ana nafasi ya kihistoria kurejesha imani ya wananchi kwa kuanzisha mchakato mpana wa maridhiano ikiwamo kuwaachia huru wote waliokamatwa kutokana na sababu za kisiasa, kuunda tume huru ya kuchunguza yaliyotokea wakati wa uchaguzi ikiwezekana kwa kushirikisha wataalamu kutoka Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki, kuitisha mkutano wa kitaifa utakaojumuisha vyama vyote vya siasa, asasi za kiraia, viongozi wa dini na wadau wengine muhimu kuzungumzia hatima na mustakabali wa taifa.

Tatizo Rais Samia ameamua amsikilize Mwigulu ambaye watanzania wanamuona mhalifu namba moja wa ufisadi, wizi na mficha data mkuu ambaye hapendi ukweli.
 
Ukweli mama ana wish sana kukutana na Tundu Lissu, ila mwamba kamkazia ile kinyma yani
 
CCM itubu kwanza dhambi zake haramu na mbaya mbele ya wananchi kwa kujutia na kisha waseme hawatarudia

CCM, imekuwa ikihonga watu ili wana CCM wafanye kila wanachotaka na kwa uovu

Wanahonga wananchi ili wapewe kura, wamewahonga mpaka viongozi wetu wa dini ili wawasemee vizuri na mambo yao maovu yafanikiwe

Sasa, CCM wanasema na wanalalamika sana eti wananchi walala hoi nao wameamua kuhongwa ili kuandamana

CCM analalamikia kitendo ambacho wao wanakiishi??

Dhambi ambayo CCM wamekuwa wakiitenda kwao wanaona ni sawa, sasa wananchi nao wameamua kuifanya, CCM wananuna...!

😂
 
nafikiri labda haelewi mazingira ya tanzagiza, sasa mtu ambaye ni mhusika mkuu halafu unamwambia aunde ''tume huru'' ya kujichunguza? hilo linawezekana vipi hata tu mtoto wa shule ya msingi anaweza kuona hilo kwamba haliwezekani, tume huru inaweza tu kuundwa na watu ambao siyo sehemu ya tatizo ...
 
Patrick Lumumba mwanasheria na mwandishi wa vitabu kutoka Kenya, amesema hatua muhimu zaidi inayotakiwa ni kuachiwa kwa kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu, ambaye anakabiliwa na tuhuma za uhaini.

Akizungumza na Diamond TV ya Zambia, Lumumba amesema hatua za awali alizoziona kutoka kwa Rais wa Tanzania Samia Suluhu ikiwamo kumuelekeza Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuwafutia mashtaka vijana mbalimbali waliokamatwa kutokana na maandamano yaliyoambatana na vurugu 29 Oktoba ni dalili za mabadiliko chanya.

"Ningependa kuona jambo kubwa zaidi…ningependa kuona Tundu Lissu akiachiwa," amesema akisisitiza kuwa kuachiwa kwake kutafungua njia ya maridhiano ya kitaifa.

Lumumba ameongeza kuwa Rais Samia ana nafasi ya kihistoria kurejesha imani ya wananchi kwa kuanzisha mchakato mpana wa maridhiano ikiwamo kuwaachia huru wote waliokamatwa kutokana na sababu za kisiasa, kuunda tume huru ya kuchunguza yaliyotokea wakati wa uchaguzi ikiwezekana kwa kushirikisha wataalamu kutoka Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki, kuitisha mkutano wa kitaifa utakaojumuisha vyama vyote vya siasa, asasi za kiraia, viongozi wa dini na wadau wengine muhimu kuzungumzia hatima na mustakabali wa taifa.
 
Huyu Lumumba huwa anaongea pumba sana.

Ni pro CCM huyo na ndo maana hajasema chochote kuhusu watoto waliochinjwa na risasi za kuulia tembo.

Samia hana tena nafasi yoyote ile ya kuleta mabadiliko chanya.

Samia ni muuaji.
 
Sikumbuki Patrice Loch Otieno Lumumba kuwa mwandishi wa vitabu zaidi ya mwanasheria na mhamasishaji mitandaoni. Ana kaunafiki fulani. Alipopigwa risasi Tundu wakati wa utawala wa rafiki yake Magufuli, Lumumba aliishia mitini na kuufyata. Sasa, kama chawa wengine, anajitokeza kujionyesha anamjali siyo? Huyu na gwajima tofauti yao ni ndogo.
 
Lissu ni Kamanda asiyependa huruma za kinafiki. Yeye anataka kutoka kwa kuishinda dhuluma. Na hapa ndipo watawala wanapojikuta njia panda.

Walifikiri ni mwepesi mwepesi tu kama Mbowe. Yaani unambambikia kesi, unamtoa jela kinyemela na kumuita Ikulu ili umfunge mdomo na mikono! Lissu yuko dunia nyingine kabisa ya kupigania kile anachokiamini.
 
Ukisoma komenti unajua watu sasahivi wana uelewa mpana na kumbukumbu juu ya mtu
 
Kwa sasa watakachokisikiliza watanganyika ni wauaji wote, kuanzia na wale wa Ali Kibao, na wadhulumaji haki wote, kuanzia Samia mwenyewe wanawajibika kwa makosa yao. Mengine yote ni porojo za kupuuzwa.
 
Huyu Lumumba huwa anaongea pumba sana.

Ni pro CCM huyo na ndo maana hajasema chochote kuhusu watoto waliochinjwa na risasi za kuulia tembo.

Samia hana tena nafasi yoyote ile ya kuleta mabadiliko chanya.

Samia ni muuaji.
Anaongea kuchiwa kwa Lissu ili kuwepo maridhiano sijui hii Kaitoa wapi?
 
Huyu Lumumba huwa anaongea pumba sana.

Ni pro CCM huyo na ndo maana hajasema chochote kuhusu watoto waliochinjwa na risasi za kuulia tembo.

Samia hana tena nafasi yoyote ile ya kuleta mabadiliko chanya.

Samia ni muuaji.

Alishasema kwenye Podcast zake za Nyuma. Fuatilia
 
Back
Top Bottom