Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,347
- 26,153
Mwanazuoni aliyebobea na mwanaharakati asiyerudi nyuma,Prof.P.L.O.Lumumba amezitaja aina kuu za Wasomi wa Bara la Afrika. Prof.Lumumba ambaye anashiriki katika Tamasha la Kigoda cha Mwalimu Nyerere,Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,amesema kuwa kuna Wasomi uchwara na Wasomi wa kweli.
Mwanazuoni huyo wa tasnia ya Sheria raia wa Kenya,amesema kuwa Wasomi uchwara ni wale ambao hutumia elimu yao kujilimbikizia mali na kujipendekeza katika mfumo uliopo.Hawa,kwa mujibu wa Prof.Lumumba,hawana manufaa yoyote kwa jamii zaidi ya kujihudumia wenyewe.
Kuhusu Wasomi wa kweli, Prof.Lumumba amesema hawa ni wale wanaoutumia weledi wao kuhudumia wenzao kwa fikra,hali na mali. Amesema Wasomi wa kweli Barani Afrika ni wachache sana kutokana na wengi kujipendekeza kwa watawala na hivyo kuwa katika kundi la Wasomi Uchwara.
Wasomi wenzangu wa Tanzania,tupo kundi gani hapo?
Chanzo: Kigoda cha Mwalimu-UDSM na EA Radio