Prof. Ndalichako rudisha Syntax A-Level

Prof. Ndalichako rudisha Syntax A-Level

Egwugu

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2011
Posts
17,558
Reaction score
8,551
Mama popote pale ulipo.

Kwanza nikukumbushe ya kuwa katika somo la kiingereza hakuna msingi wa hii lugha zaidi ya kitu kinaitwa tense. Nakumbuka hii niliambiwa toka nikiwa darasa la sita mwaka 1997 na nilipoingia form one nikayaona. Kipindi hicho tulikuwa majirani na seminari moja ndogo (std5-7) na mara nyingi tulikutana nao hasa kwenye kushindana kuongea a.k.a debate na mara nyingi walitupa shida. Shida haswa ilitokea kwasababu wenzetu waliivishwa vizuri katika kuelewa msingi wa lugha ya kiingereza (tense).

Tukaendelea kukomaa na msingi wa kiingereza (structure) tukiwa O-Level huku tukijitutumua. Mungu si Athumani huko tukatoka na kuingia A-Level na huko HGL yangu ikaendelea kujengeka chini ya topic mpya kabisa ya Syntax. Nikiri wazi, hii ni topic mama katika maandalizi adhimu ya kuelekea kuifaulu hii lugha. Mtu akiiweza vizuri hii topic hutoweza kumsumbua sana lakini hata pale atakapokuwa ni wazi utaelewa anamudu hii lugha walau kwa kuiandika make kuongea ni majaaliwa kidogo na wepesi wa ulimi wa mhusika.

Sasa leo tunayaona, mliamua kuifumua elimu kwa kuanza na kuunganisha masomo ya sayansi O-Level, mkatoka hapo mkafuta biashara na kilimo na mkaenda Advance mkaondoa baadhi ya topic katika baadhi ya masomo hasa zile zilizoonekana kuwa tatizo. Kwenye hesabu mliondoa baadhi ya vipengele na katika kiingereza mkaondoa Syntax na sasa mnafundisha vitu vya juu juu tu na kuchora kadi za mialiko. Hivi kadi ndo mmeona jambo la maana sana? Kwa sababu hamna tense pale, lakini mnafundisha kuandika makala na kuripoti habari. Sasa huyu amabaye amekosa structure huko O-Level na Syntax huko A-Level hiyo ripoti anaenda kuiandikaje? Anaendaje kuandika makala?

Lakini huyu mtu kesho mnataka asimame aongee mbele ya watu, huyu mtu anaanzaje? Kama haitoshi, tunawaona wanaotoka vyuoni, nikiri wazi mie nakutana nayo sana haya matatizo. Kuna watu wako mpaka vyuoni wanaandika research zao na wengine tayari tunao huku mtaani makazini lakini wanashindwa hata kukokotoa sentensi moja ya maana katika Syntax yake sahihi. Akikuletea kazi yake umsaidie kuedit unaweza kushangaa unatakiwa kuedit kila neno juu ya neno ukurusa wa kwanza hadi ule wa mwisho, na mbaya kuliko unakuta huyu mtu anasoma hata masomo hayo hayo ya lugha huko chuo kama vile linguistics n.k. Kuna mda unajiuliza hivi kama hii ndio hari sawa, inakuwaje wakienda huko makazini kwao? Vipi huku maofisini?
 
we unataka wanafunzi wakimbie shule??
syntax

Sent from my Infinix HOT 3 LTE using JamiiForums mobile app
 
Hakika vijana wamelemazwa na mtaala huu wa advance ambao hauna Syntax. Naunga mkono hoja, Ndalichako aweke mzigo wa Syntax mezani

Sent from my TECNO-Y3+ using JamiiForums mobile app
 
Naiunga mkono hoja hii kwa akili yangu yote, moyo wangu wote na uwezo wangu wote. Syntax ndiyo msingi wa kiingereza. Pasipo hiyo, hakuna kiingereza. Wahusika msikieni Mkuu Rweye
 
teh! teh!! Syntax ni hatari
Walimu wenyewe sijui kama wapo wanaoeza kufundisha hii kitu.. Wamebak wachache sana
 
Naiunga mkono hoja hii kwa akili yangu yote, moyo wangu wote na uwezo wangu wote. Syntax ndiyo msingi wa kiingereza. Pasipo hiyo, hakuna kiingereza. Wahusika msikieni Mkuu Rweye
Mie juzi nilimkuta dogo anasoma nikamwomba syllabus bahati nzuri alikuwa nayo, nilivyoicheki kusema kweli nilisikitika sana. Pale hakuna kitu wanafundishwa. Phonology yenyewe imechakachuliwa, ukirudi huku kila kitu kimeharibiwa. Nikajiuliza, hivi haya mambo kuondolewa yalikosea wapi, mbona sie tuling'ang'ana nayo hivyo hivyo na leo walau inatusaidia kusimama. Hawa wa leo watasimamaje?
Very sad!
 
Syntax ndo mdudu gani?
We isikie tu hivyo hivyo mtu wangu. Kwa kifupi ni roho ya lugha ya kiingereza huko shuleni.

= Sheria ya Kiingereza i.e The rules that govern a Language.
 
Inauma sana Mkuu hasa kwetu wana-HGL.
 
teh! teh!! Syntax ni hatari
Walimu wenyewe sijui kama wapo wanaoeza kufundisha hii kitu.. Wamebak wachache sana
Ni wa kuokoteza okoteza make walioko shuleni wengi wao hawajapitia huko. Wao walisoma CL/CS
 
We isikie tu hivyo hivyo mtu wangu. Kwa kifupi ni roho ya lugha ya kiingereza huko shuleni.

= Sheria ya Kiingereza i.e The rules that govern a Language.
Inabeba nini?na mimi nipate shule hapa.
 
Ila nasikia language of instruction itakuwa kiswahili kwa level zote si muda mrefu.

Sent from my TECNO-L5 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom