Prof. Ndalichako angalia wizi huu

Rufiji dam

JF-Expert Member
Feb 20, 2020
1,497
2,000
Aliyeharibu mfumo wa elimu Tanzania popote alipo endapo yupo hai ama yupo kwenye nyumba yake ya milele moto na adhabu ya mungu itawale juu yake.

Huu ni wizi wa hali ya juu inakuwaje mara baada ya kufunguliwa kuna gharama za kijinga sana katika shule hizi, serikali ipo wapi? Hii tabia isipokemewa itazalisha wajinga wengi. Soma kiambanisho cha ulipaji wa ada mara baada ya kumalizika gonjwa la korona...NDUGU MZAZI,KUFUATIA TAMKO LA KUFUNGULIWA SHULE. KWA DRS LA SABA(VII) UNATAKIWA KUKAMILISHA MALIPO YAFUATAYO:-ADA sh. 1,380,000/=,USAJILI WA MTIHANI WA TAIFA sh.15,000/=,MITIHANI YA UTIMILIFU(MOCKS) YA NDANI NA NJE sh. 15,000/=,VITINI VYA MASOMO YOTE(PAMPHLETS) sh. 50,000/=, GHARAMA YA VIFAA VYA KUJIFUNZIA sh.20,000/=. TAFADHALI,LIPA MAPEMA KWENYE AKAUNTI YA SHULE ILI KUEPUKA USUMBUFU. NAOMBA MAJIBU KAMA UMEPATA UJUMBE HUU.
 

Agenda1

JF-Expert Member
Aug 11, 2017
1,695
2,000
Hiki kilio kimekuwa kikubwa sana, nadhani ni wakati sasa mamlaka zijitokeze kusema neno, wasiache taasisi hizi binafsi zijiamulie zinachotaka kisa wanakusanya kodi.
 

batadume

Senior Member
Mar 4, 2011
100
195
shule zingine tumeambiwa tulipe Ada ya Shule kipindi cha corona na huku kipindi hicho shule zilikuwa zime fungwa Duuu
 

Abdulhalim

Platinum Member
Jul 20, 2007
17,016
2,000
Hamna kosa lolote hapo..Cha msingi kama hunahiyo pesa kwa sasa jisalimishe uweke makubaliano na shule utalipaje hiyo fedha. Msainishane ili dogo amalize shule.
 

Tanayzer

JF-Expert Member
Apr 13, 2017
2,471
2,000
mkuu lipa ila fatilia hapo kwenye pamphlets baada ya mwezi au week 2 mwanao awe amepata hizo pamhphlets za maspmo yote tena zilizojitosheleza sio wanatoa macopy ya ajabu yenye gharama ya shs 2000.... Mjibu mkuu nimepata ujumbe nitajitahidi naimani nanyie mtajitahidi vifaa viwe tayari na vijitosheleze ndani ya week 2....asante
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom