Prof. Mwandosya kung'olewa u-NEC Mbeya...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Prof. Mwandosya kung'olewa u-NEC Mbeya...!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Mar 7, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 7, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  * Kamati ya siasa ya mkoa yabariki
  * Nikutokana na utoro wa vikao kwa miaka Nane


  WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji Prof, Mark Mwandosya ambaye ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) anayewakiloisha mkoa wa Mbeya, juzi ameazimiwa kung'olewa katika cheo hicho.

  Maazimio hayo yalifikiwa katika kikao cha kamati ya siasa ya mkoa wa Mbeya iliyoketi chini ya uenyekiti wa Verena Shumbusho ambaye ni katibu wa CCM mkoa wa Mbeya baada ya Mwenyekiti wa chama hicho mkoani humo Nawab Mulla kutohudhuria kikao hicho kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kuwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.

  Kikao hicho kilidumu kwa zaidi ya masaa sita katika ukumbi wa ofisi za chama hicho ambapo hoja binafsi ya kusudio la kumhg'oa Prof, Mwandosya ikaibuka na sababu kubwa iliyotolewa na kuungwa mkoano ni utoro wa vikao kwa zaidi ya miaka Nane sasa.

  ''Hoja hiyo ilikuja na kuungwa mkono na sisi wajumbe kwasababu ilikuwa na ukweli kwa asilimia 100 maana MNEC wetu hajawahi kuhudhuria vikao vinavyomhusu kimkoa tangu achaguliwe'' alisema mmoja wa wajumbe wa kikao hicho alipohojiwa na mtandao huu kwa makubaliano ya kutoandika jina lake.

  Kwa mujibu wa taarifa za vyanzo vyetu hivyo kutoka ndani ya kamati hiyo ya siasa, zimeeleza kuwa ajenda hiyo haikuwemo katika muhtasari wa ajenda ya kikao hicho lakini ilipotolewa na mjumbe mmoja wapo hoja hiyo iliungwa mkoano na wajumbe zaidi ya Nane kati wajumbe ambao hawakuzidi 13 wa kikao hicho.

  Sanjari na hayo wajumbe hao waliweka bayana kuwa aliyejawa na ujasiri wa kufumua hoja hiyo ambayo ilionekana kukaa mioyoni mwa wajumbe wengi ni Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Mbeya Reginald Msomba (Obama).

  Habari hizo zimepabanuliwa kuwa katika hali ya kushangaza wajumbe walisikiliza kwa makini na kuitikia kwa kutikisa vichwa wakiwemo wale waliokuwa wapambe wa Prof, Mwandosya wakati wa kampeni za kuwania wadhifa huo dhidi ya Tom Mwang'onda ambao nao waliunga mkono hoja na hatimaye kuweka maazimio ya pamoja.

  Baada ya hoja hiyo kukubaliwa ilipigiliwa msumali na wajumbe kwa kumtaka Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya kutopunguza hata neno katika uchapaji wa maazimio hayo na kwamba waliweka msimamo wa kuhakiki nakala zinazotarajiwa kupelekwa katika Kamati kuu ya chama hicho (CC).

  Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya Verena Shumbusho alipotafutwa ili kuthibitisha maazimio hayo ya wajumbe wenzake ambapo alijibu kwa kulalama na kusema kuwa taarifa hizo hazikuwa sahihi.

  ''Jamani nani kawaambia mambo haya? mbona hatukuwa na ajenda ya namna hiyo kwenye kikao chetu? jamani!'' alisema kwa kifupi Katibu huyo huku akionesha kuishiwa nguvu kwa swali la kutaka kuthibitisha kikao hicho na ajenda hiyo nzito ya kumg'oa Prof, Mwandosya.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Mbeya Reginald Msomba alipotafutwa kwa njia ya simu na Gazeti hili alikataa kutoa ushirikiano wa kujibu maswali ya mwandishi.

  ''Ni kweli kikao kilikuwepo lakini kwanini unanihoji wakati umesema kuwa uliyasikia tukijadili? lakini naomba unipe muda nitaweza kujibu maswali hayo na siwezi kujib kwa usahihi kwa njia ya simu'' alisema Msomba.

   
 2. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #2
  Mar 7, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Jaribu kuedit uongeze font ya post yako, wengi humu hawatoweza kusoma post ndefu yenye fonti ndogo kiasi hiki
   
 3. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #3
  Mar 7, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  duh mwandosya inamaana hayuko makini kiasi hicho anagombea wadhifa ambao hawezi kutimiza wajibu? Au ndiyo zengweee
   
 4. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #4
  Mar 7, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mnamvumiliaje kiongozi mkuu kuwa mtoro kwa miaka nane? Muda huo wote mlikuwa mnasubiria nini?

  Btw kama na yeye ndiyo tabia yake hii basi ni heri asi gombee urais kabisa.
   
 5. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #5
  Mar 7, 2011
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Kwani huo UNEC kakaa miaka nane mpaka wampe adhabu ya kuwa mtoro miaka nane? Hivi imeshapita hata miaka minne toka achaguliwe NEC?
   
 6. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #6
  Mar 7, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Acha wafu wazike wafu wao!
   
 7. m

  maselef JF-Expert Member

  #7
  Mar 7, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 255
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wacha wamalizane maana sasa wamechanganyikiwa wanatafuta mchawi ndani ya familia ya CCM
   
 8. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #8
  Mar 7, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Jina la Obama linatumika vibaya Tanzania, hata kwa vilaza wa CCM, Obama siyo kilaza hivyo jina lake halipaswi kutumika na kila mpumbavu hata UVCCM ambako hakuna kichwa hata kimoja wote vilaza.
   
 9. anti-fisadi

  anti-fisadi JF-Expert Member

  #9
  Mar 7, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Jamani, hivi zengwe la uraisi ndio limeanza mapemaaa..!! Ah, wang'oeni tu watu wenu makini, cdm isipate tabu...weraaaaah
   
 10. V

  Vipaji Senior Member

  #10
  Mar 12, 2011
  Joined: Jun 11, 2009
  Messages: 115
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani sisiemu mpaka sasa hawajui wafanye nini mwisho watasema wanataka kumng'oa mama Jey Key. Miaka nane ni uongo katiba inasemaje kwa mtu asiyehudhuria vikao? huu ni uhuni mtupu.
   
Loading...