Prof. Mukandala 'aifilisi' UDSM

Prof. Mukandala 'aifilisi' UDSM

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Prof. Rwekaza S. Mukandala amekiweka katika ukata chuo hicho. Taarifa za kuaminika kutoka chuoni hapo zinaonesha kuwa Prof. Mukandala amekuwa na matumizi makubwa na hivyo kukifilisi chuo hicho kikongwe nchini. Matumizi hayo makubwa yametajwa kuwa ni safari zake binafsi nje ya nchi na huduma kwa wanafamilia wake.

'Amekuwa akilazimisha matumizi ya kufuru kwake na familia yake. Kwasasa chuo kiko kwenye hali mbaya kiuchumi. Malipo na miradi mbalimbali imesimama kwakuwa hakuna fedha. Zimemalizwa' kimesema chanzo toka UDSM.

Kwasasa,Prof. Mukandala yuko nchini Marekani kwa safari yake binafsi lakini imegharimiwa na UDSM. Viongozi wetu wanapaswa kujitazama vyema na kutenda haki!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Hayo yote yametokana na system mbovu ya uongozi wa CCM nchini. Na si yeye tu,wapo viongozi wengi wanaojinufaisha wenyewe kwa kupitia jasho la wananchi bila kujali waliochini yao. Ila mwisho ni tarehe 25 october keshokutwa.
 
Yeye ni Mteule bhanaa....aliyemteua anasikia? Wanajopo wenzake kiutawala wanathubutu kulisemea? Tusubirie moshi unafuka, na pengine moto ndiyo utafumua bati tuuone kwa juu...!
 
Yeye ni Mteule bhanaa....aliyemteua anasikia? Wanajopo wenzake kiutawala wanathubutu kulisemea? Tusubirie moshi unafuka, na pengine moto ndiyo utafumua bati tuuone kwa juu...!
Si alimpa digrii ya heshima juzi kati sasa kuna shida akigonga hayo ma inter. per diem
 
UDSM wamefanya mambo makubwa sana Kwa hivi sasa ukipita pale kuna renovation inaendelea, juzijuzi tu jengo jipya LA UDBS lilifunguliwa. Lectures wengi wamepelekwa kusoma PhDs nje ya nchi. Ukizingatia pia chuo kinajitegemea kwa kiasi kikubwa. Fanya utafiti usitoe mada za kuambiwa.
 
ukweli unabaki pale pale kwamba kuna matumizi mabaya ya fedha kwa vitu ambavyo havina tija kwa chuo.
 
Umeshindwa toa fact unatafuta visingizio. Juzi Mgombea kupitia UKAWA kawaambia no research no what? Jipangeni kwanza ndipo mtoe mada.
 
VUTA-NKUVUTE

@vutanikute ni kweli Mukandala ni fisadi mkubwa sana anafanya matumizi binafsi na safari Marekani kwa fojari za hatari.anakwea ndege first class na matumizi yake binafsi.TAKUKURU CHUNGUZENI OFISI YA VC MUKANDALA LAZIMA AFUNGWE TU MWIZI SANA.
 
Last edited by a moderator:

'Amekuwa akilazimisha matumizi ya kufuru kwake na familia yake. Kwasasa chuo kiko kwenye hali mbaya kiuchumi. Malipo na miradi mbalimbali imesimama kwakuwa hakuna fedha. Zimemalizwa' kimesema chanzo toka UDSM.

Kwasasa,Prof. Mukandala yuko nchini Marekani kwa safari yake binafsi lakini imegharimiwa na UDSM. Viongozi wetu wanapaswa kujitazama vyema na kutenda haki!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Wewe Vuta-Nkuvute mwenye mwenye uzee wa ku-Tupatupa wewe! Haya, nani kakuambia uchungulie mambo ya maprofesa? Eti, anamaliza pesa za UDSM, kwani wewe ulitaka afanyeje profesa wa watu?

Huyu VC ni wa kipekee kabisa hapa nchini kwani hata alipomaliza muda wa kuitumikia Tanzania (kwa maana ya kutakiwa kuustaafu), mwenyekiti wenu mwenyewe alimuongezea muda. Sasa kumbe afanyeje katika kustaafu? Si ajitunze japo kidogo?

Yaani, mzee Tupatupa unalalamika nini VC kusafiri kwa ndege na huku gari yake yenye walinzi wawili ikitangulia chini kwenda kumpokea Bukoba ili aitumie kwa matumizi ya huko. Ulitaka apande daladala au magari yasiyo na hadhi huko mikoani?

Naona na wengine wanadai eti kuna harufu mbaya hapo chuoni kwake. Kwanza mwenyewe huenda hakai hapo chuoni. Kuna uhalali gani kwa mtu wa hadhi yake aishi mazingira yanayonuka na kwenye majengo yanayofanana na magofu? Hiyo harufu yeye hatakiwi kuinusa. Bila shaka watakuwa wamempa gari yake maalum kabisa yenye AC humfikisha ofisini bila kulazimika kuvuta hewa chafu (ya DARUSO). Sasa unataka VC afanye nini? Hata hivyo maneno "choo kikuu" na Chuo Kikuu si yanafanana, harufu mbaya ina tatizo gani hapo?

Pengine nyie wenyewe serikali yenu inatoa hela
kidogo kwa ajili ya chuo. Lakini huoni usafiri wa Makamu Mkuu wa Chuo tena professa (wa kipekee) unastahili kupewa kipaumbele (cha mbele) katika matumizi ya chuo kuliko hiyo miradi mingine?

Mzee Tupatupa katika vuta-nkuvute na shule, shule ilikuvuta nini? Usiwaonee wivu wasomi wetu hasa wale wachache walioonyesha upekee ulitukuka hata kuonwa na mboni za mwenyekiti wa chama tawala.
 
Nionavo mimi, Mukandala has nothing to loose. Anajua by anymeans ataondoka baada ya JK kuondoka madarakani, ngoja amalizie vya mwisho mwisho. Hii ndo bongo bana. Kwenye colleges kama MKWAWA mpaka sasa wiki ya tano wahadhiri wameshindwa kwenda field kuassess wanachuo. Malipo yamesitishwa tangu mwezi Mei kwa sababu chuo hakina hela. Ulitaka Mukandala afanyaje?
 
Vyuo vyote vya umma vina hali mbaya kuliko saizi kulipa bill ya umeme tu issue........
 
Nionavo mimi, Mukandala has nothing to loose. Anajua by anymeans ataondoka baada ya JK kuondoka madarakani, ngoja amalizie vya mwisho mwisho. Hii ndo bongo bana. Kwenye colleges kama MKWAWA mpaka sasa wiki ya tano wahadhiri wameshindwa kwenda field kuassess wanachuo. Malipo yamesitishwa tangu mwezi Mei kwa sababu chuo hakina hela. Ulitaka Mukandala afanyaje?

Point of correction
Ni lose siyo Loose mkuu....ni kweli umeongea point
 
UDSM wamefanya mambo makubwa sana Kwa hivi sasa ukipita pale kuna renovation inaendelea, juzijuzi tu jengo jipya LA UDBS lilifunguliwa. Lectures wengi wamepelekwa kusoma PhDs nje ya nchi. Ukizingatia pia chuo kinajitegemea kwa kiasi kikubwa. Fanya utafiti usitoe mada za kuambiwa.

Hivi unafahamu kuwa hiki chuo Mwaka wa Fedha ulioisha (2013/2014) kimepata Hati Chafu ya Mkaguzi wa Mahesabu ya Serikali (CAG)?
Na hakina Historia ya Hati safi!!
 
Back
Top Bottom