Kuna ndugu mmoja aliniambia kuwa katika kipindi hiki cha uchaguzi kila mmoja anasema lake, kila mmoja anakuja na propaganda kwa yeyote na kwa namna yoyote. Nilipoona ujumbe wa vuta nkuvute nikafananisha na yale niliyoambiwa na yule ndugu. Kiukweli sijaelewa mleta mada anataka kutuambia nini. Kama kawaida yangu huwa sikurupuki kushabikia hoja kabla ya kufanya kautafiti. Ndugu oim2015 ameeleza vyema kuhusu maendeleo yanayoonekana UDSM na chuo kinavyojitegemea. Kuna ndugu amesemea ni majungu. Huko mi sitaongelea sana ila nitaongelea utafiti mdogo na wa haraka nilioufanya UDSM siku ya leo. Malengo yangu yakiwa ni kujibu maswali yafuatayo Prof Mukandala yupo safarini, kama ndiyo kwa shughuli ipi? chuo kimefilisika? Ipo miradi iliyosimama kwa kukosa pesa? Kama ndiyo tatizo liko wapi? Na mwisho swala la hati chafu na ukabila nimeliweka by the way maana ni shutuma zilizojileta (shutuma mjongeo). Matokeo ya kautafiti kangu ni kama ifuatavyo:--
kwanza ni kweli Prof. Mukandala yuko safarini kikazi na kwa mujibu wa ushahidi usio na shaka kuwa ni safari ya kikazi.-
Pili, chuo hakijafilisika, kwa kuwa ni chuo cha umma ambacho mapato yake yanatoka serikalini, utafiti na ushauri wa kitaalam, miradi ya kimaendeleo, ada toka kwa wanafunzi na kutoka kwa wafadhili ambao ni wahitimu na wadau wa elimu.-
Miradi imesimama ama la and why? Kwa mujibu wa chanzo toka kwa msarifu mkuu wa UD, ni kwamba kila mradi una chanzo chake cha mapato hivyo haiwezekani mtu akachukua fedha za miradi kwa matumizi tofauti na ilivyopangwa labda litokee janga. Amenipa mifano aliyoitoa oim2015 pamoja na extension ya jengo la utawala ambalo nilishuhudia mafundi wakiwa kazini.-
Kuhusu hati chafu nijikuta naulizwa swali maana ya hati chafu ni nini? Nami nikajiuliza hivi hati chafu mbona kama imekuwa personalized kwa Prof. Mukandala? Lakini mwisho nikakumbuka kaka yangu Prof. Kitila mkumbo aliwahi kuniambia nitofautishe Mukandala kama mtu na ka makam mkuu wa chuo. Nikachoka kabisa.-
Swala la ukabila kwa kweli sikulifuatilia sana si kwamba nimemdharau aliyelichomekea kwenye hoja kuu, au kwamba haijanigusa mzigua mie, bali naitafutia muda wa kuifanyia kazi ya ziada baada ya kumuuliza mtu mmoja aliyejinasibu kuwa moja ya waanzilishi wa THTU akaniuliza je manaibu wakuu wa chuo taaluma na utawala ni wachaga au wahaya? Je mhasibu Mkuu? Je mwanasheria? Nikamjibu sijui maana siwafaham vyema na ni muda toka nimalize shahada yangu ya pili ya uhandisi.
Akaniambia ndiyo maana umekuja bila kufanya utafiti wa angalao kukagua tovuti ya chuo maana list ya viongozi wote na majina yao kwa kirefu. Nikaona aibu nikasepa.
Maoni binafsi. Ndugu zangu nadhani ni vyema tuwe na mtazamo chanya dhidi ya viiongozi kabla ya kuhukumu. Sisemi tusikosoe na sitaki kumtetea mtu, bali tusioneshe hali fulani ya chuki, giliba, fitina au kijicho hasa tukitambua sisi sote ni binadamu.