Prof Muhongo: Tumbua hili jipu la mafuta

Davion Delmonte Jr.

JF-Expert Member
Oct 27, 2013
2,149
1,717
Niliweka uzi wangu wiki iliyopita kutilia mkazo na kuonesha uhaja wa serikali ya Magufuli kuangalia hili jipu lakini naona umepotea. Kwa sasa bei ya mafuta huko duniani inaendelea kuporomoka kwa kasi kutokana na sababu kadha wa kadha ikiwamo suala la mtikisiko wa uchumi nchini China, masuala ya interest rate nchini America ambayo yame slow down uchumi na kupelekea pressure ya demand ya oil kupungua ikilinganishwa na kuongezeka kwa supply kubwa ya OPEC ambao wana pump oil kwa fujo.

Lengo langu leo sio kuelezea sababu hizo, leo nilitaka kuendeleza shinikizo la 'bei ya mafuta ishuke nchini' wakati nilipotoa tamko wiki iliyopita kuna mdau mmoja alisema EWURA wali respond kwamba kuanzia tarehe 6 mwezi huu bei ya mafuta ingepungua kwa wastani wa Tzs 70 kwa lita. Ki ukweli sikuridhika kabisa na punguzo hilo la mafuta kwani ki uhalisia kabisa hata kwa mda wa miezi sita iliyopita mafuta yalikuwa yakitrade kwenye $60 kwa barrel na leo hii ni $30 kwa barrel kwa hiyo inamaana yamedondoka kwa asilimia 50 sasa inakuwaje EWURA juzi wametangaza kupungua kwa bei kwa asilimia kati ya 4?

Hivi huu sio unyonyaji? kwanini serikali inashindwa kuona umuhimu wa kusimamia hili suala ili wananchi wa chini wafaidike? Kwa mafuta yanavoshuka hivi ingepaswa sasa hata lita moja ipatikane kwa Tzs 1500 hapo kidogo ndo ingekuwa afadhali.

Na ukumbuke kuwa bei inavoshuka hivi hata gharama za usafirishaji mafuta pia zinaenda chini.

Sitaki kugusia yale makampuni yanayofua umeme kwa niaba ya serikali kwa kutumia mafuta, sijui kama kuna mtu wa kuratibu gharama maana usikute ile gharama ya zamani wakati oil ikiwa juu ndo bado ina exist mpaka sasa wakati Oil ipo chini. Kama ipo hivo basi kuna margin kubwa sana hapa inapotea kwa sababu tu za kutokufuatilia mambo kama haya.

Pia kutokana na hoja hapo juu ingepaswa pia umeme upungue bei kwa % fulani tena nyingi tu lakini naona hakuna mabadiliko. Nilisikia Muhongo akiongea mwanzoni mwa mwaka huu kwenye kichwa kimoja cha habari kwamba umeme unapaswa kushuka kwa sababu mafuta yanashuka bei ila sijui kama imefanyiwa kazi kwa kina.
 
Uwa sielewi njia wanazotumia ewura kupunguza na kupandisha bei hasa ya mafuta. Bei huko duniani imeshuka kutoka usd60 hadi usd32 almost by half, wkt kwetu imeshuka kidogo sana yaani hata akili ya kawaida inakataa haya mahesabu.
Mtizamo wangu sidhani kama ni sahihi kupunguza bei mara Kwa mara pale inaposhuka hii inayumbisha uchumi wa nchi, nadhan njia sahihi ni TRA kuhusishwa ili waipige kodi 100% ya kiasi chote kilichozid ambacho hakiko kwenye mkataba wa wauza mafuta na ewura. Mfano, mafuta sasa yanauzwa tshs1,900 kutoka tshs2,100 tofauti ni tshs200, ewura ingeacha bei hile hile ya awali yaani tshs 2,100/= lkn TRA wangepiga kodi tshs200 asilimia mia moja.
So bei ya mafuta inabaki tshs2,100 wkt huo huo tra wanakusanya tshs200 yao automatically wauza mafuta wanabakiwa na tshs1,900 yao ambayo ndo ingewapasa wauze na bado zile kodi nyingine zinaendelea kuwepo kama kawaida. Windfall gains should be taxed 100% for the sake of stabilizing prices of commodities in the markets. Lkn tukiruhusu kushusha shusha na kupandisha bei za bidhaa mara Kwa mara kwanza ina kera Kwa walaji sbb hawana uhakika kesho bei zitakuaje pili anaeneemeka ni mfanya biashara zaid kuliko mlaji, sbb kumkontrol ashushe bei anapotakiwa kushusha ni ngumu na tumeshuhudia wanavyokua wagumu kushusha bei wakiweka visingizio lukuki.
Mtizamo tu.
 
Back
Top Bottom