Leo baada ya Kipindi cha Maswali na Majibu Bungeni nilibahatika kuwa karibu na TV huku nikiingalia TBC japo Sijisikii Vizuri kutizama kituo hiki cha TVCCM. Lakini kwa kua sikua na njia Mbadala kwani nilikua na hamu sana ya kumuona Waziri wa Nishati na Madini,mwenye Mbwembwe nyingi Prof Muhongo akihitimisha hotuba ya Bajet ya wizara yake.
Kama nilivyotarajia kweli alianza kwa kuikosoa Hotuba ya kambi ya upinzani kuwa ni ya Porojo na haina takwimu. Tena akawashauri wapinzani wakajifunze kwa Wafadhili wao jinsi ya kuwasilisha Bajet ya Upinzani.
Hakuishia hapo bali alimkosoa Sendeka kwa kumuita Muongo anaemlisha Mh rais maneno ambayo hakuyasema.
Baadae nilimshangaa wakati akiwasisitiza Wabunge na wananchi kua kila mmoja anae msikiliza achukue,Kalamu na Karatasi kwani anaenda kutoa Takwimu Kisayansi na sio Porojo! Pale na mimi nikachukua Kalamu na Karatasi.Hakika baada ya kuelezea mambo ya ujenzi wa Bomba la gesi kutoka Mtwara kuja Dar km Zaidi ya 400 na kufananisha garama na umbali wa ujenzi wa bomba la nchini China km 8000,Naigeria 500,Brazil 400na Ujerumani kwa hakika nikajua kweli huyu ndie Profesa.
Likaja swala la ukuaji wa Uchumi.Hapo ndipo niligundua kwamba jamaa anasoma vitu vya kuambiwa baada ya KUSEMA KUWA UCHUMI WA TANZANIA UNAKUA KWA CENTEMETRE 6 HADI 7 kwa Mwaka. Hakika baada ya kusikia hivyo nilitupa kalamu na kusema Kimoyomoyo kumbe Profesa ni Mtupu na hana tofauti na Prof Maji Marefu!!