Prof muhongo kuondoa kero za wachimbaji wadogo tanzania.

kumusoma

JF-Expert Member
Feb 3, 2014
566
890
Waziri Muhongo akutana na Wachimbaji wadogo

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo hivi punde amemaliza mkutano wake na viongozi pamoja na baadhi ya wachimbaji wadogo wa madini wa Mkoani Mwanza na Geita.

Katika kikao hicho, kilichofanyikia katika Ukumbi wa Mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Waziri Muhongo amezungumza masuala mbalimbali ambayo baadhi yake ni:

🔹Amewahakikishia wachimbaji wadogo kuwatafutia maeneo ya uchimbaji. Vilevile ameagiza kuwanyang'anya maeneo wachimbaji ambao hawayaendelezi.

🔹Ameagiza Stamico ifanye kazi kwa karibu na GST ya kuhakikisha maeneo wanayopewa wachimbaji wadogo wa madini yamefanyiwa utafiti ili kuzuia tabia ya baadhi ya wachimbaji wadogo ya kuchimba kwa kuhamahama.

🔹Ameiagiza Stamico kusaidia wachimbaji wadogo katika masuala mbalimbali kama kuwatengenezea maandiko, kutoa ushauri wa uchimbaji bora bila malipo.

🔹Ameagiza kabla kufikia mwezi Juni mwakani kufanyike kikao kingine na wachimbaji wadogo nchini ili kuwa na ufanisi kwenye shughuli za uchimbaji madini.

🔹Amewaagiza wachimbaji madini nchini kutunza mazingira wakati wote wa shughuli zao.

🔹Ameagiza wachimbaji wadogo nchini kutunza amani na kuepuka uchochezi wa aina yoyote.
 
Back
Top Bottom