Prof. Muhongo atoa ripoti ya umeme Disemba 21, 2015

kumusoma

JF-Expert Member
Feb 3, 2014
566
890
UMEME - RIPOTI YA TANESCO - Mpango wa uzalishaji wa umeme Jumatatu Jioni (21.12.2015)
Hydro = MW 315, Gas = MW 485, Mafuta = MW 200
Jumla ya Uzalishaji = MW 1000.
Mahitaji ya ya leo jioni = MW 1000.
Mapungufu ya mahitaji = MW 0

UONGOZI WA TANESCO: Hali hiyo hapo juu iendelee. Lazima uzalishaji wa umeme uwe mkubwa kuzidi mahitaji. Huko ndiko tunakotaka kwenda. Tuchape kazi kwa ufanisi na ubunifu mkubwa. Hakuna kushindwa. Umeme ni uchumi.
S Muhongo
 
Bidii bado inahitajika,tunataka tuone mpaka nyumba za tembe zikiwa na umeme kwa bei nafuu,Tunataka tuone faida ya gesi yetu
 
What?? Hizo takwimu kachukua installation power capacity ya kila mtambo au active power inayozalisha kila mtambo kwa sasa? Kama kwa kila mtambo unavyozalisha kwa sasa bado nakataa hizi si za kweli kachakachua. Nyie mliopo dar mimi naweza sema hamna mgao kabisa balaa lipo huko kwa wasiojua kuongea na kupiga kelele. Uhalisia wa umeme unatakiwa kureflect na uhalisia wa upatikanaji wa nishati hiyo huku nchini sio makaratasi yanasema hakuna shida ya umeme alafu huku kitaa kila saa kumi na mbili asubuhi umeme unakatika kurudi baada ya masaa 12 then uje uniambie hakuta upungufu katika uzalishaji tusitaniane kirahisi hivyo. Cha msingi huko tanesco hasa upande wa uzalishaji bado ubunifu, uwekezaji mkubw na uthubutu unahitajika. Pia hawa wanaojiita maofisa wa mipango nchini hapa cjui hawana uwezo au idea zao zinazimwa na kubaki kwenye makaratasi tu au la
 
hiv hawa mawaziri kwa kutaka cheap popularity,hawawezi kukaa siku moja bila kuwa na vyombo vya habari?Muhongo,unataka uraisi?maana naona vyombo vya habari na picha unapenda sana.
mimi naona fanya publication kwenye website ya wizara yako na sio kupiga kelele na fanya kazi na watu wote tanesco na wizarani wewe sio chochote kile,fanya kazi yako nenda nyumbani.
 
Prof. Muhongo hongera kwa kazi nzuri ya kuhakikisha watanzania tunapata nishati hii muhimu. Ila nina mambo mawili ya kukushauri:-
Moja, ongeza juhudi kuhakikisha Kinyerezi 2,3 na 4 zinakamilika ili tujitosheleze kwa umeme na tuwe na ziada ya kutosha, yaani tuwe na standby power plants in case plant fulani inakorofisha au inahitaji service ya kawaida

Pili, fanya hima tuachane na hizo MW 200 za umeme wa mafuta (oil plants). Najua hizi MW 200 ndo za kina IPTL, Aggreko na ule mtambo wa Nyakato Mwanza. Hawa wabanwe wabadilishe mitambo yao kuwa ya gas au tuachane nao kabisaa. Maana umeme wao ni wa ghali mno.

Ukifanya haya hakika tunakuwa na umeme wa uhakika na wa gharama nafuu, hivyo kutupunguzia gharama za nishati hii muhimu. Hatua hii pia itasaidia sana kuokoa misitu yetu.
 
hiv hawa mawaziri kwa kutaka cheap popularity,hawawezi kukaa siku moja bila kuwa na vyombo vya habari?Muhongo,unataka uraisi?maana naona vyombo vya habari na picha unapenda sana.
mimi naona fanya publication kwenye website ya wizara yako na sio kupiga kelele na fanya kazi na watu wote tanesco na wizarani wewe sio chochote kile,fanya kazi yako nenda nyumbani.

Mkuu we hutaki tupewe taarifa aisee?
 
hiv hawa mawaziri kwa kutaka cheap popularity,hawawezi kukaa siku moja bila kuwa na vyombo vya habari?Muhongo,unataka uraisi?maana naona vyombo vya habari na picha unapenda sana.
mimi naona fanya publication kwenye website ya wizara yako na sio kupiga kelele na fanya kazi na watu wote tanesco na wizarani wewe sio chochote kile,fanya kazi yako nenda nyumbani.

Wakati wa Lionchawene ilikuwa umeme hakuna, tatizo hatujui ni nini wala yeye hatujui alipo.....hivyo ndio unavyopenda wewe?
 
What?? Hizo takwimu kachukua installation power capacity ya kila mtambo au active power inayozalisha kila mtambo kwa sasa? Kama kwa kila mtambo unavyozalisha kwa sasa bado nakataa hizi si za kweli kachakachua. Nyie mliopo dar mimi naweza sema hamna mgao kabisa balaa lipo huko kwa wasiojua kuongea na kupiga kelele. Uhalisia wa umeme unatakiwa kureflect na uhalisia wa upatikanaji wa nishati hiyo huku nchini sio makaratasi yanasema hakuna shida ya umeme alafu huku kitaa kila saa kumi na mbili asubuhi umeme unakatika kurudi baada ya masaa 12 then uje uniambie hakuta upungufu katika uzalishaji tusitaniane kirahisi hivyo. Cha msingi huko tanesco hasa upande wa uzalishaji bado ubunifu, uwekezaji mkubw na uthubutu unahitajika. Pia hawa wanaojiita maofisa wa mipango nchini hapa cjui hawana uwezo au idea zao zinazimwa na kubaki kwenye makaratasi tu au la

Mkuu, ukiona MW , hiyo sio active power mzee (kva) wala sio installation capacity, hapo
tayari tunazungumzia useful power.
 
Ulishawahi kupitia hivyo vituo vya kuzalisha umeme ukajionea efficiency yake ya uzalishaji kwa sasa kila mtambo unaweza toa maxmum power kiasi gani??? Hizo ni takwimu za makaratasi tu mitambo imechoka huko inapumulia pua service mbovu kabisa hakuna pesa ya kufanyia service kama inavyotakiwa ila kwenye makaratasi watu wanacopy tu capacity zile zile za tangu mtambo unafungwa. Alafu labda unifafanulie unaposema sio active power ni usefull power kivipi yaani unapinga kitu gani na unaeleza kitu gani?
 
Hizi lugha za Megawatt ni technical sana kwa mimi mwananchi wa kitaa..., mimi nachotaka kila nikiweka Luku yangu basi umeme uwake bila kukatika..., hayo mengine ni ziada
 
Mzee wa kulialia almaarufu dalali wa vitalu vya gesi hafurahii habari hizi.

La msingi umeme upatikane.
 
hizo takwim zenu sisi hatuzielew, kwa akili ya kawaida huwez kumuelekeza ivyo vitu mtanzania ambaye hayajui ayo mahesabu yenu ya umeme, sisi tunachotaka tusione migao apo ndio tutajua kweli kazi umeifanya
 
Kwa muhongo sina wasiwasi tatizo la umeme litakuwa historia. Wale wapiga dili ili wauze jenereta poleni. Tafuteni kazi nyingine.
 
Ulishawahi kupitia hivyo vituo vya kuzalisha umeme ukajionea efficiency yake ya uzalishaji kwa sasa kila mtambo unaweza toa maxmum power kiasi gani??? Hizo ni takwimu za makaratasi tu mitambo imechoka huko inapumulia pua service mbovu kabisa hakuna pesa ya kufanyia service kama inavyotakiwa ila kwenye makaratasi watu wanacopy tu capacity zile zile za tangu mtambo unafungwa. Alafu labda unifafanulie unaposema sio active power ni usefull power kivipi yaani unapinga kitu gani na unaeleza kitu gani?
.
Suala la uchovu wa mitambo ni la kweli, uhaba wa maintenance pia ni kweli, hata muhongo baada ya kufanya ziara aliliweka wazi Hilo. Technically, hizo factors lazima ziathiri uwezo wa machine kufanya kazi vizuri, in this case mitambo kufua umeme kwa kiwango chake. though itategemea pia na kiwango cha uzee wa machine zenyewe na kiwango hicho cha uhaba wa maintenance.

Useful power to me ni after power factor Kuwa applied kwenye generated (active) power. Active sio power inayomfikia mtumiaji, Kama sijakosea mkuu.

Na kama muhongo anaongopa, ni rahisi kujua, coz hakupaswi kuwa na mgao sehemu yeyote.
 
Back
Top Bottom