Prof. Muhongo anatembelea nyota ya William Ngeleja

Prof. Muhongo anatembelea nyota ya William Ngeleja

Usilinganishe mlima na kichuguu na waliobaki wafanyie kazi hizo unazodai bunifu zao Nazi so uwaziri tuu babaangu we!!!
 
Kila mtu ana wakati wake wa Kufanya kazi, huu ni wakati wa muhongo
 
muhongo ni habari nyingine kawazidi mbali sana hao akina ngeleja kuanzia ubunifu, ni sawa na kumfananisha "messi(muhongo) vs chicharito(ngeleja).
 
Ifikie wakati watu muache kutudanganya..

inawezekana ni kweli aliyafanya hayo,LAKINI JE ANASTAHILI PONGEZI ZA NINI.?ALIYAFANYA BURE.?ALIJITOLEA.?

KWANI HAKULIPWA MSHAHARA NA KODI ZETU KAMA POSHO.?
 
Miaka yote amekaa wizarani kazi yake ilikuwa ni kuanzisha tu, hakuna utekelezaji? Ujinga..
 
Tatizo la Tanzania siyo mipango bali ni utekelezaji wa mipango. Mipango ilikuwepo tangu wakati wa Ngeleja, na mingine Ngeleja aliikuta lakini Ngeleja alikuwa ni kati ya mawaziri dhaifu kabisa katika kusimamia utekelezaji. Hastahili sifa hata kidogo.

Naona kwenye uvumbuzi wa gesi umepotea kabisa. Utafiti hausimamiwi na Waziri, makampuni ya utafiti hufanya tafiti zao bila kumtegemea waziri. Makampuni haya huhitaji tu sheria ambayo huelekeza taratibu zote kuanzia upatikanaji wa leseni mpaka uchimbaji, hata kusipokuwepo waziri kama gesi ipo itagunduliwa tu.
 
Ajol katoa data sasa wanaopinga si nao walete data.
naona wewe Mgope na mwenzako Ajol hamumuogopi Mumgu ila mnataka kutuleta mtu MFU hapa JF tupigwe BAN au tuvunje Sheria za Mitandao.
Mm nipo Dodoma na ndipo pana Wizara ya Nishati na Madini sio hiyo ya DSM kula chimbuko lipo hapa na hata wanapokuja kuandaa Bajeti na kuomba 50m EWURA ikiwepo tunapata kabla
Hakuna Bajeti mbaya kama za huyu jamaa maana zote alitumia Mamilioni kuzivusha tofauti na za Ujenzi za Magufuli enzi hizo
mnataka DATA ili uweje Sakata la Escrow tu mpaka vimada wamenunuliwa nyumba huku Kisasa na wamezikimbia
Wamenunua Club ya Starehe na Katibu wake (Jairo) sasa ni mabasi na wauza urembo wamepatawala unataka DATA gani?
Rostam ndio alimuweka Ngeleja na hilo litamgharimu km mnataka arudushwe popote kwa Magufuli
Jikumbushe Data hizi mm simo

  • Napenda kutoa mwanga na historia ya waziri wa Nishati na madini Bwana William Ngeleja na mtandao wa kifisadi wa Rostam Aziz na Pius Msekwa. Bwana Ngeleja aliwekwa na mafisadi kama mwanasheria wa VODACOM (T) LTD mpaka mwaka 2005, chini ya wakurugenzi wake akiwamo ROSTAM AZIZ, PIUS MSEKWA kama mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi na Peter Noni kama wakurugenzi wazalendo wa VODACOM.
    [*]https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...a-rweyemamu-kwenye-suala-la-dowans.htmlhttp:/
    [*]/www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/103015-historia-ya-mtandao-wa-kifisadi-baina-ya-william-ngeleja-rostam-aziz-pius-msekwa.html
Rostam | Gazeti la MwanaHALISI
 
inamaana aliyoyafanya ngeleja haujaona
hakuna kipindi ambacho umeme ulikatika kama kipindi cha ngeleja, alipokuja tu muhongo hali ikakaa shwari. naamini wafanyabiashara waliokuwa wanasababisha umeme kukatika watamchukia muhongo milele.
 
Karibu yote uliyo yaongea ni kweli
lakini naomba urekebishe hapo...Idrisa Rashid hakupokea amri ya kuleta mgawo
aliepokea amri ni Mhando....Idrisa aliuondoa mgao
ulikuja kuanza tena alipo ondoka na kuingia mhando chini ya maelekezo ya Ngeleja
The Boss nakukubalia kwa 50 + 50%
ila nachoogopa JF ya leo si ile ya jana Sheria za mitandao. Idrisa mpaka leo Wafanyakazi wa Tanesco wanamkumbuka na wanaombea arudi hizi Mada za kichokozi zimeletwa kutagutana kwani Ngeleja kwa sisi tuliokuwa naye hapa jitani hatuwezi bishana nao
Hata hivyo Ngeleja alipoulizwa kama alimruhusu Dk Rashid atangaze kuwa nchi itaingia gizani baada ya Tanesco kujitoa katika ununuzi wa mitambo hiyo, Ngeleja alisema: ?Jamani nimeshasema kwamba yote nitazungumzia siku hiyo.
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/39663-dk-rashid-na-mabosi-wake-hawakuiva.html
https://www.jamiiforums.com/habari-...mba-muda-kuhusu-kauli-ya-dk-rashid-print.html
 
Lazima tujifunze kukubali, Ngeleja kstika wakati wake alifanya makubwa

Yess ikiwemo kutumia fedha za mafunZo kwa wataalam wa TPDC yeye akazitumia kwenda safar zake za nje.
 
Hakuna waziri aliyefanya kile kinachopaswa kufanywa katika nchi hii, wengi hufanya kwa wanachotaka wao au wengine na sio kinachopaswa kufanywaa!!

Hivyo hata nyerere hakufanya kilichopaswa kufanywa, labda naona Magufuli anajaribu ila kwa mbali sana kwani bado kakosea sehem nyingi na muhimu mnoo!!

Mkuu yaani baba was taiga letu mwl. Nyerere hakufanya kilichopaswa ila maghufili ndiye anajaribu kufanya kinachopaswa!!! Duuuuuuuh sometimes kama Hanna komenti no bora ukakaa kimya kuliko kujidhalilsha mbele ya jamii kiasi hiki maana inaonekana una chuki binafsi na nyerere. Hats juhudi zake kupigania na hatimaye kutuletea Uhuru wa taifa letu pia alifanya kisichostahili? Only in your head!
 
Mkuu yaani baba was taiga letu mwl. Nyerere hakufanya kilichopaswa ila maghufili ndiye anajaribu kufanya kinachopaswa!!! Duuuuuuuh sometimes kama Hanna komenti no bora ukakaa kimya kuliko kujidhalilsha mbele ya jamii kiasi hiki maana inaonekana una chuki binafsi na nyerere. Hats juhudi zake kupigania na hatimaye kutuletea Uhuru wa taifa letu pia alifanya kisichostahili? Only in your head!

Kila kitu ni msingi, ukishindwa kuujenga msingi wenye nguvu basi matatizo hayaepukiki.

Nyerere hakujenga viongozi bali alijijenga yeye kama yeye, hakujua ipo siku atang'oka, hakujenga misingi ya uongozi bora, aliiacha nchi njia panda, aliyemfuata hakujua njia sahihi ya kupita, matokeo yake ndio haya tunayo shuhudia leo, siasa zetu, wabunge wetu, vyama vyetu, elimu yetu, yaani kila sehemu ni matatizo ambayo yamesababishwa na misingi mibovu.
 
Mbona umeandika mambo aliyofanya Ngeleja pekee yake, ungeweka na aliyayafanya Prof, kisha ndo tuwapime kwa vigezo vya utendaji pamoja na muda waliotumia kufanya yote waliyoyafanya. Ila ukumbuke huyu prof. huenda kupewa uwaziri, na katitle ka uprof. kamesaidiamo.
 
Pelekaroho, ndiyo maana mada inasema Mhongo anatembelea nyota ya Ngeleja. Sasa kama kuna mtu anajua aliyofanya Mhongo zaidi ya hayo yaliyoanzishwa na Ngeleja aseme. Dr Rashid aliwaasa watz umuhimu wa kununua mitambo iliyokuwa ya Dowans kwa sababu ilikuwa inauzwa bei chee just 59.7 mil usd ili isaidie kutatua tatizo la umeme, lakini wanasiasa wanafiki walipinga. Cha ajabu mitambo hyo hyo iliponunuliwa na wamarekani Symbion wote wameufyata.
 
Waliokuwa wanafuatilia mijadala bajeti Bungeni mnakumbuka jinsi Ngeleja alivyokuwa akipangua hoja hadi Bunge zima linasisimuka! Enzi za Ngeleja wizara ya N n M ilikuwa haitumii fedha kama wakati wa Mhongo, hilo hata wabunge wanajua na wanasema. Issue ya Jairo kuchangisha taasisi ilikuwa yake kwa mamlaka yake ndiyo maana ikulu ilimsafisha Jairo, ngeleja hakuwa na hatia yoyote na hata Bunge lilibaini hivyo
 
Back
Top Bottom