KakaKiiza
JF-Expert Member
- Feb 16, 2010
- 11,679
- 8,866
Serikali imesema ifikapo mwaka 2018 mfumo wa umeme katika Mkoa wa Kagera utakua umeingizwa kwenye gridi ya Taifa.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo katika muendelezo wa ziara yake ya Kikazi kanda ya Ziwa ambapo yupo mkoani Kagera ili kukagua mitambo ya uzalishaji umeme katika maeneo ya Bukoba mjini, Biharamulo, Ngara, Murongo na Kyerwa.
Ilielezwa kuwa mkoa una miradi ya umeme kama vile mradi wa Orio Biharamulo, mradi wa kuzalisha umeme wa maji RUSUMO na mradi wa umeme Murongo ambapo miradi hii ikikamilika itachangia kupunguza upungufu wa umeme na gharama kubwa za kununua umeme kutoka Uganda.
Ilielezwa kwamba mkoa huo kwasasa unapata umeme kutoka nchini Uganda ambao umekuwa ukikatika mara kwa mara kutokana na umeme huo kuwa mkubwa wa zaidi ya MW 152 ya uwezo wa TANESCO wa MW 132 na hivyo kulilazimu shirika hilo kutumia mitambo yake inayotumia mafuta kwa MW 2.2 ambayo haikidhi mahitaji ya umeme ya mkoa wa MW 5.2
Profesa Muhongo aliliagiza shirika hilo kuhakikisha linaharakisha mpango wa kuunganisha mkoa wa Kagera kwenye gridi ya Taifa.
"Tanesco ni lazima muharakishe mipango ya kuunganisha mkoa huu kwenye gridi ya taifa ili kuwapatia wananchi huduma ya umeme wa uhakika,"
Alisema ifikapo mwaka 2025, Tanzania itaingia kwenye uchumi wa kati ambao utatokana na uwekezaji mkubwa kwenye viwanda ambavyo vitahitaji umeme wa kutosha na uhakika.
Mbali na hilo, Profesa Muhongo aliliagiza Shirika hilo la Tanesco mara baada ya mkataba uliopo wa kuuziana umeme kati ya Tanzania na Uganda kuisha, wahakikishe wanaingia mkataba wa muda mfupi lengo likiwa ni kuepusha kuwa ndani ya mkataba wa muda mrefu wakati tayari mkoa huo utakua kwenye gridi ya taifa.
Akielezea hali ya umeme mkoani humo, Meneja wa Tanesco Kanda ya Ziwa, Mhandisi Amos Maganga alisema kwa sasa Tanzania inanunua umeme kwa gharama ya senti za Marekani 8.4 kwa kila ankara.
Alisema Tanzania inao mkataba wa kununua umeme kutoka Uganda kiasi cha megawati 10 ambao unahudumia wilaya za Bukoba Mjini na Vijijini, Karagwe, Muleba na Misenyi.