tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,038
"Dira 2050 imeweka matarajio mahsusi pia: kuwa na sera, sheria na kanuni wezeshi zinazopunguza udhibiti uliokithiri na zinazochochea ukuaji wa biashara za ndani pamoja na kuvutia uwekezaji wa ndani na nje; kuwa na mfumo imara wa kidijitali unaoendeleza biashara zinazochipukia kupitia sera, ufadhili, mitaji na sheria zinazoharakisha ukuaji ili kuongeza ajira na kuimarisha uchumi; kuwa na jamii yenye utamaduni wa kuweka akiba na uwekezaji kwa ajili ya kuendeleza biashara, kuongeza kipato na kuimarisha hali ya maisha; na kuwa na sekta ya umma iliyoandaliwa kuwezesha na kufanikisha biashara na uwekezaji",- Prof. Kitila.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo akizungumza siku ya Ijumaa mkoani Dar es Salaam katika hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), Watoa Huduma katika sekta ya uwekezaji na Kongamano la Uwekezaji lililoratibiwa TISEZA