Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema kitendo cha Walimu na Wanafunzi kutumia choo kimoja shuleni ni uzembe wa wazi, akisisitiza kuwa hakuna Halmashauri nchini inayoshindwa kujenga miundombinu ya Vyoo kwa viwango vinavyotakiwa.
Profesa Mkenda ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati wa Hafla ya Uzinduzi na Ugawaji wa Magari pamoja na Vifaa vya Kidijitali vya Kielimu na Saidizi kwa Walimu, Wakufunzi na Walimu tarajali wenye ulemavu nchini.
Amesema katika mazingira hayo, Wadhibiti Ubora wa Elimu wanapaswa kuwa macho na kuwajibika ipasavyo, kwa kuwa wao ni mboni ya Serikali katika kubaini na kuibua changamoto zote zilizopo mashuleni ili zichukuliwe hatua mapema, badala ya kusubiri Wananchi au watu wasiokuwa na dhamana kuzitangaza kupitia Mitandao ya Kijamii.
Aidha, Profesa Mkenda amefafanua kuwa si kosa kwa Wananchi kupiga picha na kuibua changamoto za shule mitandaoni, kwani hatua hiyo imekuwa ikisaidia Serikali kuzitambua na kuzitatua. Hata hivyo, amesisitiza kuwa Wadhibiti Ubora wa Elimu wanapaswa kuwa wa kwanza kugundua changamoto hizo kabla hazijawekwa hadharani.
Akizungumzia suala la Walimu na Wanafunzi kutumia Choo kimoja, Waziri Mkenda amesema hakuna sababu ya msingi kwa hali hiyo kuendelea, kwani fedha za ujenzi wa miundombinu zipo, lakini changamoto hujitokeza pale ambapo Viongozi wa Halmashauri wanapoelekeza rasilimali katika maeneo wanayoona yanafaa wao, badala ya kuzingatia mahitaji halisi ya shule.
Vilevile, Waziri Mkenda ameagiza Wadhibiti Ubora wa Elimu kote Nchini kuunda Makundi Kazi yatakayojumuisha Walimu Wakuu wa Shule, kwa lengo la kutoa taarifa za changamoto zinazojitokeza kila siku.
Katika hatua nyingine, ametaja tukio la kumwondoa kazini Mdhibiti Ubora Mmoja wa Elimu aliyeshindwa kutekeleza wajibu wake ipasavyo, akisisitiza kuwa uzembe hautavumiliwa katika Sekta ya Elimu.