Prof Mbarawa: Serikali kutuma wataalamu kukagua ubora wa ndege mpya ya Dreamliner (B787)

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,874
SERIKALI imesema itatuma wataalamu kwenda kukagua ndege ya Boeing 787 Dreamliner kabla haijaja nchini kwa ajili ya kuanza kutumika rasmi.

Hiyo ni baada ya kuwapo taarifa mbalimbali zinazodai ndege hiyo haina viwango.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, alisema utengenezaji wa ndege hufanywa kwa awamu na kwamba kila hatua wataalamu huwa wanakwenda kukagua.

“Nitafuatilia taarifa hizo lakini kwa kawaida huwa tunalipia kiasi fulani na kila hatua huwa tunaitwa kuikagua…lakini najua wataalamu watakwenda kuikagua,” alisema Profesa Mbarawa.

Hivi karibuni, Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT – Wazalendo), alisema ndege hiyo ni sehemu ya ndege zilizokuwa chini ya kiwango zikiitwa Terrible Teens.

“Nimefanya utafiti kidogo na nimethibitisha kuwa tumenunua ndege zilizokataliwa hata na Rwanda rafiki zetu, kinachofuata ni kikubwa zaidi,” alisema Zitto.

Katika mwaka wa fedha wa 2016/17 Serikali iliweka maazimio ya kununua ndege nne kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) ili kuboresha safari za anga nchini.

Ndege mbili ndege mpya za Bombardier Q400 zilinunuliwa katika awamu ya kwanza, Septemba mwaka jana na Rais Dk. John Magufuli ndiye aliyezizindua.

Rais Dk. Magafuli alisema Serikali ina mpango wa kununua ndege nyingine mbili zenye uwezo wa kubeba watu zaidi ya 150 kuboresha usafari wa anga na kuleta ushindani wa biashara katika mataifa.
 
Ndege lzm ina ubora. Suala la msingi ni tunanunua ndege ipi na kwa bei gani? Maana kuna ndege aina 2 na zote ni 787 dreamliner. Kuna ya kawaida ya dola 224m na hio terrible twin ya dola 100m Wawe wawazi kwa hilo.
 
SERIKALI imesema itatuma wataalamu kwenda kukagua ndege ya Boeing 787 Dreamliner kabla haijaja nchini kwa ajili ya kuanza kutumika rasmi.

Hiyo ni baada ya kuwapo taarifa mbalimbali zinazodai ndege hiyo haina viwango.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, alisema utengenezaji wa ndege hufanywa kwa awamu na kwamba kila hatua wataalamu huwa wanakwenda kukagua.

“Nitafuatilia taarifa hizo lakini kwa kawaida huwa tunalipia kiasi fulani na kila hatua huwa tunaitwa kuikagua…lakini najua wataalamu watakwenda kuikagua,” alisema Profesa Mbarawa.

Hivi karibuni, Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT – Wazalendo), alisema ndege hiyo ni sehemu ya ndege zilizokuwa chini ya kiwango zikiitwa Terrible Teens.

“Nimefanya utafiti kidogo na nimethibitisha kuwa tumenunua ndege zilizokataliwa hata na Rwanda rafiki zetu, kinachofuata ni kikubwa zaidi,” alisema Zitto.

Katika mwaka wa fedha wa 2016/17 Serikali iliweka maazimio ya kununua ndege nne kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) ili kuboresha safari za anga nchini.

Ndege mbili ndege mpya za Bombardier Q400 zilinunuliwa katika awamu ya kwanza, Septemba mwaka jana na Rais Dk. John Magufuli ndiye aliyezizindua.

Rais Dk. Magafuli alisema Serikali ina mpango wa kununua ndege nyingine mbili zenye uwezo wa kubeba watu zaidi ya 150 kuboresha usafari wa anga na kuleta ushindani wa biashara katika mataifa.
KUNA WATU WALIKUWA WANASEMA ZITTO ANATAFUTA KIKI.
WAZIRI ANASEMA ATATUMA WATAALAM KUKAGUA.
HAWA WALIOKUWA WANASEMA ZITTO HAAMINIKI SIJUI WANAWAZO GANI!
 
Waziri amefanya vizuri kufuatilia taarifa hiyo yenye utata ni Ombi uchunguzi uwekwe hadharani mapema ili kuweka kumbukumbu sawa.
Hakuna cha ukaguzi hapo.. Halafu mbona hamjiulizi je wenzenu wanafanya hivyo katika manunuzi..!?
 
Mtaalam kutoka Tanzania akakague ndege?

Kama sielewi hii imekaaje au watachukua watu kutoka huko ng'ambo coz hawajasema wataalamu hao watatoka wapi

Kama kuna mtu anawajua hawa wataalam please aje atuelezee hawa ni watu gani hasa kutoka bongo
 
Waziri amefanya vizuri kufuatilia taarifa hiyo yenye utata ni Ombi uchunguzi uwekwe hadharani mapema ili kuweka kumbukumbu sawa.
Hao watakaokwenda kuikagua report yao imeishaandikwa na ikulu ili boss asiumbuke.Wakaguzi watatoka wapi wakati hatujawahi kuwa na ndegr kama hiuo?
 
Wamelipa cash kabla ya kuangalia ubora wa ndege husika! Mafisadi katika ubora wao duh!

Na hawa "wataalamu wa Kitanzania" huu ujuzi wa kukagua ubora wa ndege walijifunzia wapi!? Na lini!?

SERIKALI imesema itatuma wataalamu kwenda kukagua ndege ya Boeing 787 Dreamliner kabla haijaja nchini kwa ajili ya kuanza kutumika rasmi.

Hiyo ni baada ya kuwapo taarifa mbalimbali zinazodai ndege hiyo haina viwango.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, alisema utengenezaji wa ndege hufanywa kwa awamu na kwamba kila hatua wataalamu huwa wanakwenda kukagua.

“Nitafuatilia taarifa hizo lakini kwa kawaida huwa tunalipia kiasi fulani na kila hatua huwa tunaitwa kuikagua…lakini najua wataalamu watakwenda kuikagua,” alisema Profesa Mbarawa.

Hivi karibuni, Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT – Wazalendo), alisema ndege hiyo ni sehemu ya ndege zilizokuwa chini ya kiwango zikiitwa Terrible Teens.

“Nimefanya utafiti kidogo na nimethibitisha kuwa tumenunua ndege zilizokataliwa hata na Rwanda rafiki zetu, kinachofuata ni kikubwa zaidi,” alisema Zitto.

Katika mwaka wa fedha wa 2016/17 Serikali iliweka maazimio ya kununua ndege nne kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) ili kuboresha safari za anga nchini.

Ndege mbili ndege mpya za Bombardier Q400 zilinunuliwa katika awamu ya kwanza, Septemba mwaka jana na Rais Dk. John Magufuli ndiye aliyezizindua.

Rais Dk. Magafuli alisema Serikali ina mpango wa kununua ndege nyingine mbili zenye uwezo wa kubeba watu zaidi ya 150 kuboresha usafari wa anga na kuleta ushindani wa biashara katika mataifa.
 
SERIKALI imesema itatuma wataalamu kwenda kukagua ndege ya Boeing 787 Dreamliner kabla haijaja nchini kwa ajili ya kuanza kutumika rasmi.

Hiyo ni baada ya kuwapo taarifa mbalimbali zinazodai ndege hiyo haina viwango.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, alisema utengenezaji wa ndege hufanywa kwa awamu na kwamba kila hatua wataalamu huwa wanakwenda kukagua.

“Nitafuatilia taarifa hizo lakini kwa kawaida huwa tunalipia kiasi fulani na kila hatua huwa tunaitwa kuikagua…lakini najua wataalamu watakwenda kuikagua,” alisema Profesa Mbarawa.

Hivi karibuni, Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT – Wazalendo), alisema ndege hiyo ni sehemu ya ndege zilizokuwa chini ya kiwango zikiitwa Terrible Teens.

“Nimefanya utafiti kidogo na nimethibitisha kuwa tumenunua ndege zilizokataliwa hata na Rwanda rafiki zetu, kinachofuata ni kikubwa zaidi,” alisema Zitto.

Katika mwaka wa fedha wa 2016/17 Serikali iliweka maazimio ya kununua ndege nne kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) ili kuboresha safari za anga nchini.

Ndege mbili ndege mpya za Bombardier Q400 zilinunuliwa katika awamu ya kwanza, Septemba mwaka jana na Rais Dk. John Magufuli ndiye aliyezizindua.

Rais Dk. Magafuli alisema Serikali ina mpango wa kununua ndege nyingine mbili zenye uwezo wa kubeba watu zaidi ya 150 kuboresha usafari wa anga na kuleta ushindani wa biashara katika mataifa.
Lisemwalo lipo jamani.
 
Tanzania ina wataalamu wa kukagua ndege kujua ubora wake kweli? Kwenye vivuko wataalamu wengine huwa wanakuwa wapi?
 
Back
Top Bottom