barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Waziri mwenye dhamana na mambo ya Uchukuzi,Mh.Prof Mbarawa Makame,amesema serikali imeamua kununua rada nne na kuziweka sehemu tofauti ili kuweza kulinda anga la Tanzania ili kuweza kuongeza ufanisi wa ufuatiliaji wa ndege za ndani na nje ya nchi zinazotumia anga la Tanzania.
Waziri Mbarawa ameyasema hayo wakati akiwa mkoani Mtwara akikagua miundombinu ya uchukuzi ya bandari na uwanja wa ndege wa Mtwara,ambapo kwa sasa uwanja huo unapokea ndege moja tu ya Shirika la Precision inayofanya safari zake kila siku kutoka Dsm kwenda Mtwara.
Hoja ya kuongeza rada nne (4) zaidi,ni kuhakikisha serikali inaweza kuliongoza vizuri anga lake na kufuatilia kwa ukaribu ndege ndogo ambazo hutua na kuondoka ktk migodi yetu huku ikiondoka na madini au kubeba mali na nyara bila taarifa sahihi.
Rada hizo mpya na za kisasa,zitasaidia kung'amua ndege zinazopita na kuruka ktk anga la Tanzania ili kuweza kuongeza mapato,kuimarisha ulinzi na usalama ktk anga na nchi kwa ujumla.
Katika ziara hiyo,Mkuu wa Wilaya ya Mtwara,ndugu Mmanda,amemuomba Waziri Mbarawa,kufanya inalowezekana ili ndege za ATCL ziweze kutua ktk uwanja wa Mtwara kama ilivyo kwa ndege za kampuni ya Precision,kwani kwa uchumi wa gesi na kiwanda cha Saruji cha Dangote,ni wazi kuwa mkoa wa Mtwara una abiria wa kutosha.