Prof. Mbarawa: Serikali Imetenga fedha kwenye Bajeti ya Mwaka 2023/24 kuanza Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo

Hatushangai kwani tuumeishaambiwa remote iko msonga
 
Sasa unachobisha ni nini wakati hiyo bajeti ni ya kufyeka vichaka kuzunguka eneo la hiyo bandari? Sifa ya bandari ya bagamoyo inaeleweka, kama hizo sifa za eneo la EPZ nk havipo, itakuwa na tofauti gani na bandari bubu huku ukanda wa pwani?
 
 
Huu mradi ungeshaanza tokea enzi za JK changamoto ilikua je ijengwe kwa pesa za ndani, mkopo, au muwekezaji ila bandari ilikua lazima tu ijengwe.

So wameafiki ijengwe kwa pesa za ndani. Hii miradi sio ya JK au mwendazake au Samia ipo kwenye Mpango wa Taifa tokea enzi za Mkapa huko sema ikitekelezwa tu utasikia ubunifu wa JPM mara sijui mradi wa Mama!!
 
Je tunajenga kwa pesa zipi? Za ndani au mikopo? Kwa mkataba upi ule wa china au mwingine?

Pls Naomba mnijibu wajuvi wa mambo nikikosa majibu Bora kushabikia yanga maana inalipa na kuondoa stress za siasa za Tanzania!!
Pesa za ndani mkuu otherwise watakopa ila hakuna joint venture hapo Wala muwekezaji au private sector kama mkataba ulivyokua hapo mwanzo.
 
Hapa inatafutwa namna ya kutukamua ili kumfurahisha Msoga.

The guy will go down in history as the only mistake we made.
Si nyie ndio Kila siku mnasema wananchi sijui system haiwezi wapa upinzani nchi kisa watauza rasilimali, mara sijui ikulu ni mahali patakatifu Sasa ilikuaje mnakiri kuwa Kuna Rais alikua fisadi na Bado system ikamuacha atawale?

So many contradictions
 
NI JAMBO ZURI NCHI KUJENGA MIRADI KAMA HII KWA KUFUNGA MKANDA, HAKUNA NCHI NYINGINE ITAYOJENGA TANZANIA BALI WATANZANIA WENYEWE
 
Sawa, naiona Dubai ya Tanzania
 
Ya kwetu ni sawa na kuiza amna tofauti
 
Pesa za ndani mkuu otherwise watakopa ila hakuna joint venture hapo Wala muwekezaji au private sector kama mkataba ulivyokua hapo mwanzo.
Kwanza nitoe duku duku: ile 'avatar' ya mwanzo ilikuwa na tatizo gani?

Pili, jibu ulilompa mkuu 'technically', ni sahihi, ila ni sehemu moja tu ya mradi.

Mradi waliotaka kujenga waChina na Oman ulihusisha ujenzi wa Bandari (sehemu ambayo sasa tunachukua jukumu hilo, kwa usahihi kabisa sisi wenyewe), na sehemu nyingine ni ya ujenzi wa hiyo SEZ, ambayo serikali haihusiki nao. Wenye kutaka kuwekeza kwenye sehemu hiyo watawekeza na bandari itawahudumia.
Huu ndio uelewa wangu kuhusu jambo hili.

Ninakubaliana kabisa na serikali katika uamzi wa ujenzi wa bandari hii, badala ya kuwaachia wengine waijenge.

Ni sawa tu na jinsi Kenya walivyoamua kujenga zile ghati tatu za bandari ya Lamu; wakitegemea baada ya kufanya hivyo wawekezaji wengine watakuja kujenga ghati nyingine nyingi, pamoja na matakataka mengine ya LAPSSET kama yalivyopangwa.
Ila tofauti ya Bagamoyo na hiyo Lamu, Bagamoyo yetu ni lulu yenye thamani kubwa sana kutokana na mahali ililpo, kwa hiyo uwekezaji kwenye SEZ unatarajiwa kuwa kivutio kikubwa kuliko ilivyo kule Lamu.

Pengine nimalizie kwa "uthubutu" wetu wa kujenga wenyewe hiyo bandari..., mkuu 'zitto jr', niseme wazi hapa, hakuna jambo linalonisisimua sana kama kuona tukijiamini kufanya baadhi ya mambo yetu sisi wenyewe. Tuna umri wa zaidi ya miaka 60 sasa hivi kama taifa huru; kuna mambo mengi sana tunayoweza kuyafanya sisi wenyewe sasa bila ya kutegemea hadi tusaidiwe. Tukibana mianya ya matumizi mabaya ya mapato yetu ninayo hakika kabisa tunao uwezo wa kufanya mambo mengi sana sisi wenyewe.
 
Kwani kuna sheria kwamba lazima miradi ya mwendazake ikamilike ndiyo tuanze miradi mipya?

Au umeandika tu kwa kiwewe cha kuondokewa na mpendwa wako?
 
Nisikilize: Wanatafuta gear ya kuanzia. Ule mpango wa kutumia sijui wachina, sijui waarabu wameona ulikumbana na kelele nyingi. Hivyo basi, watajifanya kuanza kwa kutumia ''fedha za serikali'' halafu baada ya muda watatafuta muda na sababu maalum wawape hao hao waliopigiwa kelele. Mark my words. Bongo hatuna fedha za kujenga. Hii ni danganya toto tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…