Prof. Mark Mwandosya ni mpotoshaji

Prof. Mark Mwandosya ni mpotoshaji

Uwezo wako wa kufikiri na poa hayo ni maoni yako hongera sana kwa kupost unacho fahamu
 
Ukiwa Mbeya upepo ndiyo huo hivyo ukitengwa na chama tawala ni lazima utafute uungwaji mkono kwa kutumia chama kingine hiyo siyo tatizo kabisa tatizo ni lile wazo kwamba hawa wakiondoka madarakani wakija wengine matatizo yetu yatakwisha??
 
Mwandosya kafanya kitu gani cha kukumbukwa kwenye utumishi wake katika taifa hili?? Hata CCM walishamkataa amegombea mara mbili kwenye kura za maoni ya uraisi lakini hakupata kitu!! Sasa uprofesa wake unatusaidia nini sasa?? Ana stress za kushindwa kwenye kura za maoni mara mbili. Aende huko hatusaidii kitu kama Chadema wanafikiri atawasaidia wampendekeze kugombea uraisi 2020 apambane na Raisi Magufuli tuone nani zaidi.
Kwa mambumbumbu kama wewe kamwe huwezi kujua mchango wa Mwandosya ktk nchi hii, bali kwa wenye akili wanajua mchango wa Prof. Ameandika majarida mengi sana ktk Nyanja mbalimbali kwa wewe naamini hujawahi kusoma hata moja na wala huwezi kuelewa.
 
Mhe Joseph Mbilinyi SUGU alisema ” Mhe Rais Magufuli hawezi kupendwa na watu kwa kumshoot risasi Lissu, kumtupa Jela miezi minne Lema, kumteka Ben saanane, kumteka Roma na kumzuia SUGU asiongee..!!”.....Matukio yote haya hakuna aliyekamatwa...kama sio serikali basi jeshi la polisi lifutwe tujilinde wenyewe kwa sungusungu ,.hiiiiiiiiiiiiiiii
Kuna mambo yanayotia shaka kwenye kesi za.namna hii. N.a. vema Mahakama ya juu ikayatolea msimamo.
1.Hakuna kesi ya jinai inayofanyika bila kuwepo mlalamikaji(aliyeathirika) ambaye huwa ni shahidi 1(PW1).
2.He mtu kusema maneno ambayo mtu mwingine hatari kuwasikia ni jinai?
3.Kwa kuwa ni lazima aliyeathirika na kutukanwa aonyeshe athari zilizompata ni kigezo gani kilichotumika kuthibitisha kosa "beyond reasonable doubt"?
MENGINE
1.Ni kitu gani "kilichomkimbiza" hakimu baada ya kutoa hukumu ile?
2.Jana nilimsikia msemaji wa Magereza akisema two mfungwa akiachiwa halafu akakaa siku moja zaidi anakuwa ana "trespass", am ball kosa jingine la jinai, ilikuwaje mfungwa huyo aendelee ku trespass siku zote hizo?
2.Kama hiyo haitoshi, ni kwa nini "mhalifu" aliyeachiliwa apewe "lift" na gari ya RCO mpaka nyumbani kwake?
Nawaza tu!
 
Kutokuelewa namba 1 ndio inaonesha upungufu wako kichwani ! Hivi mpaka leo hujamjua MLALAMIKAJI katika kesi hii?? au kwa akili yako ulitaka RAIS ndio asimame MAHAKAMANI?? AIBU!
 
Mkuu uko sahihi mwandosya kazeeka anatakwa avuliwe uprofesa Ni wapi hukumu inasomeka kuwa sugu kafungwa kwa siasa hakuna neno siasa kwenye judgement nzima Mwandosya Kama profesa alitakiwa ajue hilo
Hii ya kumvua Uprofesa kwa kumtembelea Sugu ni ya kuanzia na kufungia mwaka!

Ulisikia pale Dr. Mwakyembe aliposomewa sehemu ya andiko lake la shahada ya uzamivu PhD alikosema serikali tatu ndio zinafaa halafu akawa anakataa mfumo huo wakati wa Bunge la Katiba?
Hicho ndio kinaweza kumuondolea mtu sifa ya kitaaluma.

Usisahau pia Mzee Mwandosya ni "icon" wa siasa za Mbeya na hii imetokana na yeye kuwa "fatherly figure" kwao wote!
 
Na Jumanne Lutengano Majoka
Mjasiriamali Mbeya Mjini.

Hakuna mashaka kuwa mapokezi ya bashasha na kauli aliyoiandika Prof. Mark Mwandosya katika ukurasa wake wa Twitter baada Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi “Sugu” kuachiwa kwa msamaha wa Rais hapo jana anaungana na kauli ya Sugu mwenyewe kuwa adhabu aliyoipata kwa kumtusi Rais ilikuwa ni kifungo cha kisiasa.

Kwa Prof. Mwandosya na Sugu mwenyewe ni vizuri kujiepusha na upotoshaji huu. Sugu alifungwa kwa kosa la jinai na hivyo alikuwa mfungwa wa kosa la jinai na sio mfungwa wa kisiasa kama anavyodai.

Mfungwa wa kisiasa ni mtu aliyefungwa jela kutokana na kujihusisha na shughuli ama imani za kisiasa. Hapa ndipo mtu kama Nelson Mandela anaitwa mfungwa wa kisiasa.

Lakini Sugu sio mfungwa wa kisiasa, Sugu ni mhalifu, alifanya makosa ya kuvunja sheria za nchi kwa kumtukana Rais. Hata utambulisho wake anaitwa Mfungwa namba 219/2018 na sio Mfungwa wa Kisiasa namba 219/2018 kama anavyodai na kama Prof. Mwandosya anavyounga mkono.

Hizi ni siasa za kipuuzi na zinapoungwa mkono na mtu mwenye utumishi kwa nchi kama Prof Mark Mwandosya inatia wingu zito na inavunja heshima.

Nimejiuliza sana kuhusu lengo la Prof. Mark Mwandosya kumpokea Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi “Sugu” aliyetolewa jana Mei 10, 2018 kwa msamaha wa Rais na ujumbe aliouandika kupitia ukurasa wake wa Twitter. Tena Prof. Mwandosya kafunga safari hadi nyumbani kwake Sugu kumpokea na kuandika alichoandika.

Kwa ambao hamjasoma alichopost Prof. Mwandosya, kapiga picha akiwa na Sugu nyumbani kwa Sugu kaandika hivi nanukuu “Nikimpa hongera Mbunge wa Mbeya Mhe.Joseph Mbilinyi kwa kuhitimu Chuo cha Uanasiasa,Gereza la Ruanda,Mbeya.Kutofautiana vyama,itikadi na misimamo kusilete uhasama na uadui.Mungu Ibariki Tanzania.

Na akaendelea kwa kimombo “Congratulating Hon.Joseph Mbilinyi-right after graduating from Ruanda Prison Mbeya”

Baadaye Sugu nae kapost picha kwenye Instagram wakiwa wamekaa na Prof Mwandosya nyumbani kwake Sugu na Prof Mwandosya akinywa juisi na kaandika “Nikiwa na Prof. Mwandosya nyumbani kwangu leo. Asante kwa maneno ya busara na ujasiri ulionipa leo na hata ulipokuja kuniona gerezani”

Ukiunganisha nukta za kauli za Prof. Mwandosya na Sugu haileti mashaka kuwa wanaongea lugha moja kwamba Sugu ni mfungwa wa kisiasa na wanataka kuaminisha umma kuwa Sugu alionewa kwa adhabu ile.

Niseme hivi kwa Sugu kutoa kauli hizo haina shida kwa sababu kwa namna yoyote baada ya kukumbwa na adhabu ile ilitarajiwa kuwa atataka kuitumia kwa manufaa ya kisiasa, lakini kwa Prof Mwandosya kuna ukakasi.

Kuna ukakasi kwa sababu Prof. Mwandosya ni Mwanachama wa CCM na aliyetukanwa na Sugu ni Mwenyekiti wake. Kwa alichokiandika Prof. Mwandosya ni wazi kuwa anaamini Sugu alionewa na anamtia moyo kuwa amefuzu chuo cha uanasiasa katika gereza la Ruanda. Anaamini kuwa Rais Magufuli alistahili kutukanwa vile na Sugu na hakubaliani na adhabu aliyopewa na mahakama kwa mujibu wa sheria.

Prof. Mark Mwandosya ni Mwenyekiti wa Bodi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ambacho awali kilifanya kazi ya kutengeneza makada na sasa kinafundisha kozi mbalimbali za uongozi, siasa, uchumi n.k. Aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa chuo hiki na Rais Magufuli ambaye ametukanwa na Sugu na hakukataa uteuzi huu.

Prof. Mwandosya ni Waziri mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne na ni mtu aliyejitokeza mara mbili kutaka ridhaa ya wana CCM ili agombee kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila mafanikio.

Kwa mazingira hayo hapo juu, Prof. Mwandosya angepaswa kuwa makini na kauli zake na ikiwezekana aamue moja ama kujipambanua kuwa yeye sasa anaunga mkono siasa za upinzani na kujihusisha na upinzani kwa uwazi ama kuchunga kauli zake. Aamue ama kuwa moto ama kuwa baridi aache double standards.

Ni jambo linalokanganya kwamba anatumikia cheo alichopewa na Rais Magufuli, anatibiwa na Serikali inayoongozwa na Rais Magufuli na ni mwanachama wa chama kinachoongozwa na Rais Magufuli halafu anamuunga mkono mtu anayemtukana Rais Magufuli.

Na hii sio mara ya kwanza kwa Prof. Mwandosya kufanya double standards hizi. Mwaka 2015 alipokosa kuteuliwa kugombea Urais kupitia CCM aliibuka na kumshambulia Mwenyekiti wake Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, akipinga mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM.

Ilitushangaza wengi kwa sababu Prof. Mwandosya alipaswa kujua kwa nini chama kiliamua kumteua Magufuli na angepaswa kuelewa hata manufaa ambayo chama kimeyapata maana ni wazi kwamba kama wangepitishwa waliokuwa wanatajwatajwa pengine chama kingepoteza kwenye uchaguzi mkuu.

Nakusihi Prof Mwandosya kama una mahaba na upinzani hamia huko, mimi kama Mtanzania ninayeamini katika utawala wa sheria, na ninajitahidi kupambanua mambo kwa maslahi ya Taifa naona unachokifanya sio sawa, kama wanavyosema vijana inawezekana unataka kupata Kiki au uendelee kupata umaarufu wa kisiasa, lakini kwa heshima yako hili unalolifanya unakuwa Kivuruge.

Sipendezwi na aina ya siasa zinazofanywa na upinzani na ni miongoni mwa watu wanaopenda kuwepo upinzani wenye tija na sio upinzani unalivuruga Taifa kama huu tulionao Tanzania. Tuna upinzania ambao hauna dalili za kushika dola na hauna tija.

Alituhumiwa hivyo kutokana na namna alivyofanya siasa zake mwaka 2005 alipochuana na Jakaya Kikwete katika ngazi ya chama. Kwa wakati ule zilikuwa ni nguvu za mtandao. Mtandao wa Prof. Mwandosya ulibeba sura ya kikanda zaidi.

Nionavyo mimi kama Prof. Mwandosya hatojisahihisha ni wakati sasa wa Rais Magufuli kumuengua katika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kilichopo Kigamboni. Aachwe huru ili afanye siasa za upinzani kwa uhuru zaidi, aungane na Sugu na wanasiasa wengine wa upinzani kufanya siasa bora zaidi.

Prof Mwandosya aamue kuwa baridi au kuwa moto.

Mimi ni mwananchi wa Tanzania
Naitwa Jumanne Lutengano Majoka.
Nakuunga mkono hapo unaposema prof ana siasa za kikanda ni kweli kabisa yan kama kavurugwa hivi..yeye inabidi apumzike tu maana kama ana ndoto ya uraisi umri ule ni kujidanganya tu. Sugu kamtukana raisi sasa alipooenda magareza alienda kutumikia alichostahili sasa huyu prof wenu aache mihemko ya kikanda
 
Kutokuelewa namba 1 ndio inaonesha upungufu wako kichwani ! Hivi mpaka leo hujamjua MLALAMIKAJI katika kesi hii?? au kwa akili yako ulitaka RAIS ndio asimame MAHAKAMANI?? AIBU!
Sijamjua.
Au ni RCO au DPP?
Sehemu ya pili ya hoja yangu ni kuwa he, hao watathibitishaje "beyond reasonable doubt" kuwa rahisi ametukanwa na kaathirika?
Supposing yeye angekuwa ameyachukulia kama mambo ya siasa tu?
My brother Mimi ni wanachama wa CCM ila hapa naongelea suala la kitaaluma sio kuhemka.
Tusipopeana maangalizo mambo haya yasije kutugeuka huko mbeleni.
Wabillah tawfiq!
 
Profesa hapangiwi nini chakufanya, mitazamo haiwezi fanana tuvumiliane
 
Mwandosya kafanya kitu gani cha kukumbukwa kwenye utumishi wake katika taifa hili?? Hata CCM walishamkataa amegombea mara mbili kwenye kura za maoni ya uraisi lakini hakupata kitu!! Sasa uprofesa wake unatusaidia nini sasa?? Ana stress za kushindwa kwenye kura za maoni mara mbili. Aende huko hatusaidii kitu kama Chadema wanafikiri atawasaidia wampendekeze kugombea uraisi 2020 apambane na Raisi Magufuli tuone nani zaidi.

Kwa kuwa hajaliibia Taifa hawezi kukumbukwa!Tutawakmbuka daima waliojiuzia nyumba za serikali na nyingine kuzigawa kwa makahaba na ndugu zako!

Tutawakumbuka waliolisababishia Taifa hasara ya mabilioni kutokana na maamuzi yao ya kukurupuka!

Tutawakumbuka walionunua chuma chakavu kwa bilioni 10 na sasa chuma hicho kilichokuwa kinajulikana kama "MV Dar es Salaam" kilibatizwa na kuwa "kifaru cha jeshi"

Tutawakumbuka waliotokomea gizani na 1.5+Trilioni!

Tutawakumbuka milele waliojimilikisha mgodi wa makaa ya mawe wa kiwira kupitia kampuni yao ya ANBEN!

Tutawakumbuka milele mafisadi wa Escrow,EPA,TanGold,Meremeta,Kagoda,DeepGreen,Radar,Wizara ya ujenzi na Majengo pacha ya BOT!

Tutawakumbuka walionunua Pangaboi ambalo sasa hivi lina mwezi mmoja linaoza pale Mwanza airport!

Tutawakumbuka wanaojenga uwanja wa ndege Chattle!

Tutawakumbuka waasisi wa jeshi la watu waliojulikana ambao wamegeuka mumiani kwa kunyonya damu za watu na miili kuitupa kwenye vilindi vya maji!

Tutawakumbuka waliowaita watoto wa masikini pale UDOM kuwa ni vilaza!

Tutawakumbuka walioijimilikisha hazina ya nchi kwa kumuweka mtoto wa Dada kuwa katibu mkuu hazina!

Orodha ni ndefu,Mwandosya hawezi kukumbukwa kwa sababu hakuyafanya hayo.
 
Acheni kumshambulia mleta mada, Jibubi hoja zake. Mleta mada yuko sahii, Sugu alifanya kosa la jinai na alihukumiwa kifungo baada ya kutiwa hatiani. Hili halina ubishi, na utabaki kuwa ukweli daima.

Kosa alilohukumiwa sugu ni kosa la jinai na si kosa la kisiasa kama inavyopotoshwa. Sheria zimetungwa, makosa na adhabu zikabainishwa. Hilo kosa na adhabu yake lipo kwa mtu yeyote. Hata Nyangema mchoma mikaa kule tuliani akifanya kosa hilo atashtakiwa na kuhukumiwa tu.
Kwani kosa la kisiasa lipoje????

Kama mnaweza kupindisha risasi hewani, mtashindwa kupindisha kosa????

Acheni mambo yenu
 
Na Jumanne Lutengano Majoka
Mjasiriamali Mbeya Mjini.

Hakuna mashaka kuwa mapokezi ya bashasha na kauli aliyoiandika Prof. Mark Mwandosya katika ukurasa wake wa Twitter baada Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi “Sugu” kuachiwa kwa msamaha wa Rais hapo jana anaungana na kauli ya Sugu mwenyewe kuwa adhabu aliyoipata kwa kumtusi Rais ilikuwa ni kifungo cha kisiasa.

Kwa Prof. Mwandosya na Sugu mwenyewe ni vizuri kujiepusha na upotoshaji huu. Sugu alifungwa kwa kosa la jinai na hivyo alikuwa mfungwa wa kosa la jinai na sio mfungwa wa kisiasa kama anavyodai.

Mfungwa wa kisiasa ni mtu aliyefungwa jela kutokana na kujihusisha na shughuli ama imani za kisiasa. Hapa ndipo mtu kama Nelson Mandela anaitwa mfungwa wa kisiasa.

Lakini Sugu sio mfungwa wa kisiasa, Sugu ni mhalifu, alifanya makosa ya kuvunja sheria za nchi kwa kumtukana Rais. Hata utambulisho wake anaitwa Mfungwa namba 219/2018 na sio Mfungwa wa Kisiasa namba 219/2018 kama anavyodai na kama Prof. Mwandosya anavyounga mkono.

Hizi ni siasa za kipuuzi na zinapoungwa mkono na mtu mwenye utumishi kwa nchi kama Prof Mark Mwandosya inatia wingu zito na inavunja heshima.

Nimejiuliza sana kuhusu lengo la Prof. Mark Mwandosya kumpokea Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi “Sugu” aliyetolewa jana Mei 10, 2018 kwa msamaha wa Rais na ujumbe aliouandika kupitia ukurasa wake wa Twitter. Tena Prof. Mwandosya kafunga safari hadi nyumbani kwake Sugu kumpokea na kuandika alichoandika.

Kwa ambao hamjasoma alichopost Prof. Mwandosya, kapiga picha akiwa na Sugu nyumbani kwa Sugu kaandika hivi nanukuu “Nikimpa hongera Mbunge wa Mbeya Mhe.Joseph Mbilinyi kwa kuhitimu Chuo cha Uanasiasa,Gereza la Ruanda,Mbeya.Kutofautiana vyama,itikadi na misimamo kusilete uhasama na uadui.Mungu Ibariki Tanzania.

Na akaendelea kwa kimombo “Congratulating Hon.Joseph Mbilinyi-right after graduating from Ruanda Prison Mbeya”

Baadaye Sugu nae kapost picha kwenye Instagram wakiwa wamekaa na Prof Mwandosya nyumbani kwake Sugu na Prof Mwandosya akinywa juisi na kaandika “Nikiwa na Prof. Mwandosya nyumbani kwangu leo. Asante kwa maneno ya busara na ujasiri ulionipa leo na hata ulipokuja kuniona gerezani”

Ukiunganisha nukta za kauli za Prof. Mwandosya na Sugu haileti mashaka kuwa wanaongea lugha moja kwamba Sugu ni mfungwa wa kisiasa na wanataka kuaminisha umma kuwa Sugu alionewa kwa adhabu ile.

Niseme hivi kwa Sugu kutoa kauli hizo haina shida kwa sababu kwa namna yoyote baada ya kukumbwa na adhabu ile ilitarajiwa kuwa atataka kuitumia kwa manufaa ya kisiasa, lakini kwa Prof Mwandosya kuna ukakasi.

Kuna ukakasi kwa sababu Prof. Mwandosya ni Mwanachama wa CCM na aliyetukanwa na Sugu ni Mwenyekiti wake. Kwa alichokiandika Prof. Mwandosya ni wazi kuwa anaamini Sugu alionewa na anamtia moyo kuwa amefuzu chuo cha uanasiasa katika gereza la Ruanda. Anaamini kuwa Rais Magufuli alistahili kutukanwa vile na Sugu na hakubaliani na adhabu aliyopewa na mahakama kwa mujibu wa sheria.

Prof. Mark Mwandosya ni Mwenyekiti wa Bodi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ambacho awali kilifanya kazi ya kutengeneza makada na sasa kinafundisha kozi mbalimbali za uongozi, siasa, uchumi n.k. Aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa chuo hiki na Rais Magufuli ambaye ametukanwa na Sugu na hakukataa uteuzi huu.

Prof. Mwandosya ni Waziri mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne na ni mtu aliyejitokeza mara mbili kutaka ridhaa ya wana CCM ili agombee kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila mafanikio.

Kwa mazingira hayo hapo juu, Prof. Mwandosya angepaswa kuwa makini na kauli zake na ikiwezekana aamue moja ama kujipambanua kuwa yeye sasa anaunga mkono siasa za upinzani na kujihusisha na upinzani kwa uwazi ama kuchunga kauli zake. Aamue ama kuwa moto ama kuwa baridi aache double standards.

Ni jambo linalokanganya kwamba anatumikia cheo alichopewa na Rais Magufuli, anatibiwa na Serikali inayoongozwa na Rais Magufuli na ni mwanachama wa chama kinachoongozwa na Rais Magufuli halafu anamuunga mkono mtu anayemtukana Rais Magufuli.

Na hii sio mara ya kwanza kwa Prof. Mwandosya kufanya double standards hizi. Mwaka 2015 alipokosa kuteuliwa kugombea Urais kupitia CCM aliibuka na kumshambulia Mwenyekiti wake Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, akipinga mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM.

Ilitushangaza wengi kwa sababu Prof. Mwandosya alipaswa kujua kwa nini chama kiliamua kumteua Magufuli na angepaswa kuelewa hata manufaa ambayo chama kimeyapata maana ni wazi kwamba kama wangepitishwa waliokuwa wanatajwatajwa pengine chama kingepoteza kwenye uchaguzi mkuu.

Nakusihi Prof Mwandosya kama una mahaba na upinzani hamia huko, mimi kama Mtanzania ninayeamini katika utawala wa sheria, na ninajitahidi kupambanua mambo kwa maslahi ya Taifa naona unachokifanya sio sawa, kama wanavyosema vijana inawezekana unataka kupata Kiki au uendelee kupata umaarufu wa kisiasa, lakini kwa heshima yako hili unalolifanya unakuwa Kivuruge.

Sipendezwi na aina ya siasa zinazofanywa na upinzani na ni miongoni mwa watu wanaopenda kuwepo upinzani wenye tija na sio upinzani unalivuruga Taifa kama huu tulionao Tanzania. Tuna upinzania ambao hauna dalili za kushika dola na hauna tija.

Alituhumiwa hivyo kutokana na namna alivyofanya siasa zake mwaka 2005 alipochuana na Jakaya Kikwete katika ngazi ya chama. Kwa wakati ule zilikuwa ni nguvu za mtandao. Mtandao wa Prof. Mwandosya ulibeba sura ya kikanda zaidi.

Nionavyo mimi kama Prof. Mwandosya hatojisahihisha ni wakati sasa wa Rais Magufuli kumuengua katika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kilichopo Kigamboni. Aachwe huru ili afanye siasa za upinzani kwa uhuru zaidi, aungane na Sugu na wanasiasa wengine wa upinzani kufanya siasa bora zaidi.

Prof Mwandosya aamue kuwa baridi au kuwa moto.

Mimi ni mwananchi wa Tanzania
Naitwa Jumanne Lutengano Majoka.
Umelogwa wewe
 
duu haya mambo ya siasa majanga
sasa sijui maneno yote hayo uliyoandika hapo juu yanini si ungesema tu "kafungwa kisiasa yatosha tu"
 
Kwa mambumbumbu kama wewe kamwe huwezi kujua mchango wa Mwandosya ktk nchi hii, bali kwa wenye akili wanajua mchango wa Prof. Ameandika majarida mengi sana ktk Nyanja mbalimbali kwa wewe naamini hujawahi kusoma hata moja na wala huwezi kuelewa.
Hayo majarida ya kucopy na kupaste yamesaidia nini nchi hii wewe mwelewa. Wewe ni zaidi ya mbumbumbu nafikiri wewe ni asshole!
 
Kwa kuwa hajaliibia Taifa hawezi kukumbukwa!Tutawakmbuka daima waliojiuzia nyumba za serikali na nyingine kuzigawa kwa makahaba na ndugu zako!

Tutawakumbuka waliolisababishia Taifa hasara ya mabilioni kutokana na maamuzi yao ya kukurupuka!

Tutawakumbuka walionunua chuma chakavu kwa bilioni 10 na sasa chuma hicho kilichokuwa kinajulikana kama "MV Dar es Salaam" kilibatizwa na kuwa "kifaru cha jeshi"

Tutawakumbuka waliotokomea gizani na 1.5+Trilioni!

Tutawakumbuka milele waliojimilikisha mgodi wa makaa ya mawe wa kiwira kupitia kampuni yao ya ANBEN!

Tutawakumbuka milele mafisadi wa Escrow,EPA,TanGold,Meremeta,Kagoda,DeepGreen,Radar,Wizara ya ujenzi na Majengo pacha ya BOT!

Tutawakumbuka walionunua Pangaboi ambalo sasa hivi lina mwezi mmoja linaoza pale Mwanza airport!

Tutawakumbuka wanaojenga uwanja wa ndege Chattle!

Tutawakumbuka waasisi wa jeshi la watu waliojulikana ambao wamegeuka mumiani kwa kunyonya damu za watu na miili kuitupa kwenye vilindi vya maji!

Tutawakumbuka waliowaita watoto wa masikini pale UDOM kuwa ni vilaza!

Tutawakumbuka walioijimilikisha hazina ya nchi kwa kumuweka mtoto wa Dada kuwa katibu mkuu hazina!

Orodha ni ndefu,Mwandosya hawezi kukumbukwa kwa sababu hakuyafanya hayo.
Kumbe unajua huyo Prof hawezi kukumbukwa kwa lolote!! Sasa povu lote hilo la OMO la nini??
 
Acheni kumshambulia mleta mada, Jibubi hoja zake. Mleta mada yuko sahii, Sugu alifanya kosa la jinai na alihukumiwa kifungo baada ya kutiwa hatiani. Hili halina ubishi, na utabaki kuwa ukweli daima.

Kosa alilohukumiwa sugu ni kosa la jinai na si kosa la kisiasa kama inavyopotoshwa. Sheria zimetungwa, makosa na adhabu zikabainishwa. Hilo kosa na adhabu yake lipo kwa mtu yeyote. Hata Nyangema mchoma mikaa kule tuliani akifanya kosa hilo atashtakiwa na kuhukumiwa tu.
Were mtetee sisi tumshambulie usitulazimishe wote kula mihogo.
 
Kifungu kipi cha sheria halali za nchi hii kilitumika kumtia hatiani na kumfunga Sugu?
 
Back
Top Bottom