Prof. Maghembe: Marufuku kuuza kahawa mbichi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Prof. Maghembe: Marufuku kuuza kahawa mbichi

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MziziMkavu, Jan 24, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jan 24, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Kahawa


  Sakata la ununuzi wa kahawa mbichi wilayani Ileje limepata ufumbuzi, baada ya Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Prof. Jumanne Maghembe, kuruhusu serikali ya mkoa na wilaya kuendelea na msimamo wake wa kuzuia biashara hiyo kwa maslahi ya wananchi.
  Kabla ya ujio wa Prof. Magembe, kutoa ruhusa hiyo, kulikuwa na mvutano wa muda mrefu kutokana na kampuni moja ya kununua kahawa wilayani hapa kupinga amri halali ya serikali ya wilaya na mkoa kuzuia kununua kahawa mbichi.
  Prof. Magembe juzi kwenye mkutano wa wadau wa kahawa kutoka wilaya nne zinazolima kahawa za Mbeya Vijijini, Ileje, Rungwe na Mbozi, alisema uamuzi wa halmashauri pamoja na serikali ya mkoa wa kukataa ununuzi wa kahawa mbichi unapaswa kutekelezwa ipasavyo.
  Miongoni mwa wadau waliohudhuria mkutano huo ni wakuu wa wilaya, wakurugenzi, wenyeviti wa halmashauri za wilaya hizo, wawakilishi wawili wa wakulima kutoka kila wilaya, na makampuni yanayojihusisha na ununuzi wa zao hilo.
  Hata hivyo, kabla ya Prof. Magembe kutoa tamko, kulikuwa na mvutano mkubwa baina ya upande unaotetea ununuzi wa kahawa mbichi na ule unaopinga.
  Awali, akitoa taarifa ya zao hilo, Afisa Kilimo wa Mkoa wa Mbeya, Nyasebwa Chimaga, alisema moja ya changamoto zinazokabili
  kilimo cha zao hilo ni ununuzi wa kahawa mbichi.
  Alisema ununuzi huo unamnufaisha zaidi mfanyabiashara anayenunua kahawa hiyo ambaye baadaye anaiuza kwa bei nzuri katika masoko ya ndani na nje ya nchi, jambo ambalo limesababisha wanunuzi hao ambao pia baadhi yao ni wakulima kujikita katika ununuzi huo na kuachana na kazi ya kufufua mashamba ya kahawa.
  Alisema baada ya wakulima kuuza kwa rejareja kahawa mbichi, unapofika msimu wa kuuza kahawa mbivu, wao huwa hawana kahawa ya kutosha na hivyo kukosa fedha kwa ajili ya kufufua na kuendeleza mashamba yao.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. M

  Mamatau Member

  #2
  Jan 24, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uamuzi huo ni wa busara na faida zaida zaidi kwa wakulima na kuongeza thamani ya zao hilo katika soko la dunia. Lakini Prof. Maghembe anafahamu kuwa uchakachuaji katika kamati za mauzo za mikoa umekwamisha mauzo ya zao lla Korosho katika mikoa Mtwara Lindi na Pwani? Ajiandae kusaidia ulipaji wa madeni ya vyama vya msingi kwa mabenk!!!!
   
Loading...