DCONSCIOUS
JF-Expert Member
- Oct 4, 2010
- 1,269
- 473
Tuikiwa tunaelekea kumpata mgombea wa urais kwa tiketi ya UKAWA naomba niongee machache juu ya kile kinacho endelea ndani ya UKAWA .Kikubwa ni nachotaka kuzungumza ni juu ya Prof lipumba na chama chake kuiga yale yanayo fanywa na vyama vingine bila kuangalia madhara yake au muendelezo wake. Ngoja niwakumbushe kidogo mwaka 2012 pale chama cha demokrasia na maendeleo chadema kilipo kua kina endeleza operation yake ya M4C yaani Movement for Change, mikoa ya kusini ndipo chama cha wananchi CUF walikasirika na kuhisi wamevamiwa kwenye ngome yao hali iliyo wapelekea na wao kuzindua operation yao waliyo ipa jina la Vision for change (V4C). Nilifurahishwa sana na operation ya CUF niliamini chama kimezinduka kutoka usingizini. Lakini nilishituka hasa baada ya kupata taarifa kutoka ndani ya chama hicho kwamba lengo lilikua kuwajibu chadema walio vamia kile wanacho kiita ngome yao . Hivyo operation ya CUF ililenge mkoa wa Arusha waliio amini ni ngome ya Chadema.Baada ya hapo wakarudi Mtwara na Lindi na ndipo operation yao ilipo fia.Sina tatizo sana na mipango ile ya CUF. Lakini pia naamini umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) ulilenga kufuta tofauti zilizo kuwepo kati ya vyama vikubwa vya upinzani. Nakuvifanya viwe imara zaidi kupambana na CCM .Nimeshituka zaidi baada ya kusikia kua Prof Lipumba anataka kutangaza nia kama walivyo fanya wagombea wa ccm yaani kwa mbwembwe nyingi . Huku akijua kua UKAWA hawajampitisha mgombea wa nafasi hiyo. Lengo kubwa ni kuwaaminisha wanachama wa CUF kua yeye ni bora zaidi ya wengine ndani ya UKAWA hivyo hakuna anae stahili kupitishwa zaidi yake.Inawezekama ikawa kweli yeye akawa bora zaidi ya wegine. Lakini je njia anayo tumia ni si sahihi. Wote tunajua kua prof Lipumba ni mtaaramu wa uchumi. Hivyo anataka kutumia hicho kama kigezo cha kuteuliwa na UKAWA. Inawezekana kikawa nikigezo lakini kwa siasa za Tanzania kigezo cha utaaram wa uhumi kinatosha kumfanya awe Rais?. Hajiulizi kwamba kwanini pamoja na uprofesa wake lakini amegombea urais kalibia mala nne, lakini zote ameshidwa na kura zinazidi kupungua. Hivi ni muujiza gani anao utegemea utakao mfanya mwaka huu ashinde, ikiwa chama chake kimeishia kufanya mikutano Lindi, Mtwara na Tabora tu? Hata mikoa ya pwani tuliyo aminishwa kua ni ngome yao kama Tanga wamshindwa kabisa kujijenga.Chama kina majimbo mawili tu huku bara, lakini prof anataka agombee yeye. Kwa harakati zipi walizo zifanya na chama chake mpaka tuamini ataweza kushinda na kuwauza wagombea wa ukawa?. Wenzenu chadema wakiwa wana zunguka nchi nzima kujenga chama chao, nyinyi mnabaki ofisini kutoa matamko alfu mnataka . mgombea wenu apitishwe kugombea urais. Toka uchaguzi wa mwaka 2010 Profesa hajawai kanyaga mkoa wowote wa nyanda za juu kusini au kanda ya ziwa kwa ajiri ya kujenga chama lakini leo anataka apewe nafasi. Nakumbuka siku David Kafulila alipo pendekeza Dr Slaa awe mgombea wa UKAWA hao hao CUF walikuja juu na kudai amevunja taratibu . https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...igawa-ukawa-zinazofanywa-na-wana-ukawa-9.html. lakini cha ajabu wanashindwa kumlaani prof lipumba anae fanya yaleyale waliyo kua wanamlaumu kafulila aliye toa maoni yake tu.