Uchaguzi 2020 Prof Lipumba na Bernard Membe wako wapi?

KAUMZA

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
699
237
Hawasikiki kabisa. Kweli maisha yanaenda kasi sana. Sikuwahi kudhani kuwa Chama cha Chauma na Mgombea wake wa Urais Bw.Hashimu Rungwe wangekuwa maarufu kuliko CUF ya Lipumba au kuliko Bernard Membe.

Kwa sasa Prof Lipumba amepoteza dira kabisa. Nipo visiwani wiki sasa. CUF iliyokuwa na base imara kabisa hapa visiwani, imejifia kabisa. Haisikiki wala haionekani. Sio huku visiwani tu, bali hata Bara.

Chadema inazidi kuimarika siku hadi siku. Nguvu ya Chadema haijapungua licha ya kuzuiwa kwa hamasa za siasa kama vile mikutano etc. Licha ya waungaji mkono (sina uhakika kama walikuwa wanalipwa au kuahidiwa kitu au waliunga kwa hiari yao).

Kila kona ukipita ni aidha umsikie Lissu au Magufuli. The only two giants.

Wapi Lipumba? Wapi Membe?
 
Hao wamepima maji na unga, wakakubali yaishe. Lipumba Magufuli alimwahidi angempa tafu kwani hakujua kuwa hata yeye angekuja kupigania roho yake na ndipo akaamua kila moja afe kivyake.
Ha ha haaaaa!
 
Lipumba na Membe ni marehemu wa kisiasa. Wajinga fulani wasiojitambua. Propumba alitumika kama kondomu ya CCM na Membe alidhani ni maarufu kumbe hata kwao Rondo ni maarufu kwa Baba yake tu. Wana Rondo hawana muda naye.
 
Lipumba ametega pale kwenye kukubali matokeo, maana amezoea kupewa mpunga ili atoke hadharani na kusema kuwa uchaguzi ulikuwa huru na wa haki, ila bahati mbaya uchaguzi huu umekula kwake vibaya sana.
 
Lipumba ni mamluki, Mkwere alikuwa anampa hela ili afanye maigizo ya Chama Cha upinzani kama hadaa kwa wafadhili!!! Sasa naona JIWE hakuendeleza uteja wake ndio maana amekata pumzi!!
 
Mbatia wa nccr na mgombea wao nao wako hoi, DP, NRA nao chalii.

Rungwe tunafahamu kafuata ubwabwa akirudi tunakuwa poa.
 
Lipumba ametega pale kwenye kukubali matokeo, maana amezoea kupewa mpunga ili atoke hadharani na kusema kuwa uchaguzi ulikuwa huru na wa haki, ila bahati mbaya uchaguzi huu umekula kwake vibaya sana.
Haha prof kaamua kumalizia maisha ya siasa ligi ya kina NLD.
 
Akina nccr, cuf, tlp, udp na nra ni vyama tanzu vya ccm ambayo kwayo ni chama mama.
 
Niguse Ninuke
Li Professor
Hao Ni Garasa Hawana Mvuto Wala Madhara
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom