Prof. Lipumba: Mafisadi CCM wamefanikiwa

Prof. Lipumba: Mafisadi CCM wamefanikiwa

Huyu mzee hana mvuto wala ushawishi anashindwa kujenga chama chake na kutwa kuitaja ccm kama anataka uenezi si aseme tuu ,kama ccm kunamafisadi si ujenge chama chako ili ukamate dola aache utani na ccm anaboa sana huku prof uchwara kwake tabora ameshindwa kupata hata kata anatakiwa kuumiza kichwa kuwashawishi wananchi wake waache uvivu kutwa yeye na ccm,hopeless prof
 
18 DECEMBER 2012

Na Rehema Maigala

MWENYEKI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amesema mtandao wa mafisadi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), umefanikiwa kupata uongozi kwa asilimia
75 na mikakati waliyonayo ni kuchukua nchi ifikapo 2015.


Prof. Lipumba aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akifungua mkutano wa Baraza Kuu la Taifa la chama hicho ambao wajumbe walijadili mambo 11 ya msingi.

Alisema chaguzi mbalimbali za CCM zilizofanyika hivi karibuni, zilitawaliwa na vitendo vya rushwa kwa wagombea wasioa na sifa za kuwa viongozi na wenye masilahi binafsi badala ya chama.

“Chaguzi za CCM zilitawaliwa na rushwa hasa wa wanawake, mafisadi wasipewe nafasi ya kuongoza nchi na safari hii, hatuta kubali wachaguliwe viongozi wenye masilahi binafsi,” alisema.

Alisema Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli, mkoani Arusha, Bw. Edward Lowassa, naye aliwahi kulalamikia vitendo vya rushwa ndani ya chama na kusisitiza kama mgombe haba pesa, hawezi kushinda nafasi ya Halmashauri Kuu (NEC).

“Gharama za maisha zimepanda, elimu imeshuka na kusababisha Watanzania waishi bila ya matumaini katika nchi yao, Tanzania hakuna mwananchi anayepata haki kama binadamu,” alisema.

Akitolea mfano wa Shekhe Ponda Issa Ponda na kudai hadi sasa amenyimwa dhamana wakati kisheria kesi yake alistahili kuipata lakini hadi sasa anaendelea kusota rumande.

Prof. Lipumba alilalamikia muda mchache waliopewa wananchi kutoa maoni ya Katiba Mpya tofauti na wanavyofanya katika nchi zingine ambazo hutoa muda wa mwaka mmoja kama Kenya.

tulipewa taa


SOURCE; MAJIRA
tulipewa taarifa ,kupitia vyombo vya habari kuwa CUF ndani hawaelewani, mh Lipumba analalamika, mikakati waliokuwa wamejiwekea, kuimarisha CUF, zanzibar kisha wahamie Bara haitekelezwi, vilevile kumekuwa na taarifa kuwa CUF ni CCM B, taarifa ambazo uongozi umejaribu kuzipinga kwa nguvu zote, ila hili si rasmi tunaelezwa huku mitaani, kuwa wale wapenda siasa za udini, ambao ni wanachama au mashabiki wa CUF,hivi sasa wanakiunga mkono chama cha mapinduzi, huku wakisingizia kuwa hawaitaki CDM kwa kuwa ni chama cha kikristo. baada ya kuyasema hayo sasa binafsi nahitimisha kwa kukubaliana kuwa CUF iko TAABANI, kwani hainiingii akilini, MWENYEKITI wa chama ndani ya vikao halali vya chama, azungumuzie mambo ya chaguzi za CCM na kuahidi kutokubaliana na kuchaguliwa mgombea asiyefaa, jiulize kwanini? CCM, nadhani kuna hoja za msingi chama kiko chali.
 
Back
Top Bottom