Prof. Lipumba: Mafisadi CCM wamefanikiwa

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
18 DECEMBER 2012

Na Rehema Maigala

MWENYEKI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amesema mtandao wa mafisadi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), umefanikiwa kupata uongozi kwa asilimia
75 na mikakati waliyonayo ni kuchukua nchi ifikapo 2015.

Prof. Lipumba aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akifungua mkutano wa Baraza Kuu la Taifa la chama hicho ambao wajumbe walijadili mambo 11 ya msingi.

Alisema chaguzi mbalimbali za CCM zilizofanyika hivi karibuni, zilitawaliwa na vitendo vya rushwa kwa wagombea wasioa na sifa za kuwa viongozi na wenye masilahi binafsi badala ya chama.

"Chaguzi za CCM zilitawaliwa na rushwa hasa wa wanawake, mafisadi wasipewe nafasi ya kuongoza nchi na safari hii, hatuta kubali wachaguliwe viongozi wenye masilahi binafsi," alisema.

Alisema Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli, mkoani Arusha, Bw. Edward Lowassa, naye aliwahi kulalamikia vitendo vya rushwa ndani ya chama na kusisitiza kama mgombe haba pesa, hawezi kushinda nafasi ya Halmashauri Kuu (NEC).

"Gharama za maisha zimepanda, elimu imeshuka na kusababisha Watanzania waishi bila ya matumaini katika nchi yao, Tanzania hakuna mwananchi anayepata haki kama binadamu," alisema.

Akitolea mfano wa Shekhe Ponda Issa Ponda na kudai hadi sasa amenyimwa dhamana wakati kisheria kesi yake alistahili kuipata lakini hadi sasa anaendelea kusota rumande.

Prof. Lipumba alilalamikia muda mchache waliopewa wananchi kutoa maoni ya Katiba Mpya tofauti na wanavyofanya katika nchi zingine ambazo hutoa muda wa mwaka mmoja kama Kenya.

SOURCE; MAJIRA
 
Prof. Lipumba anasema UKWELI KABISA; Lakini Wana-UNION GVT ZANZIBAR ina MAANA inawakubali hao MAFISADI
 
wavunje ndoa yao na ccm kwanza ndio aje kusema hayo vinginenvyo ni unafiki wa hali ya juu sana
 
Yaani Lipumba na usomi wooooooote huu hajui kuwa hata sasa serikali iliyopo madarakani imesimikwa na mafisadi?
 
Hapo kwa ponda ndo kachemsha. we huoni ijumaa sasahivi hakuna mabomu ya machozi!
[FONT=courier
new]18 DECEMBER 2012[/FONT]

Na
Rehema Maigala

MWENYEKI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amesema
mtandao wa mafisadi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), umefanikiwa
kupata uongozi kwa asilimia
75 na mikakati waliyonayo ni kuchukua nchi ifikapo 2015.

Prof. Lipumba aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akifungua mkutano
wa Baraza Kuu la Taifa la chama hicho ambao wajumbe walijadili mambo 11
ya msingi.

Alisema chaguzi mbalimbali za CCM zilizofanyika hivi karibuni,
zilitawaliwa na vitendo vya rushwa kwa wagombea wasioa na sifa za kuwa
viongozi na wenye masilahi binafsi badala ya chama.

“Chaguzi za CCM zilitawaliwa na rushwa hasa wa wanawake, mafisadi
wasipewe nafasi ya kuongoza nchi na safari hii, hatuta kubali
wachaguliwe viongozi wenye masilahi binafsi,” alisema.

Alisema Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli, mkoani Arusha, Bw.
Edward Lowassa, naye aliwahi kulalamikia vitendo vya rushwa ndani ya
chama na kusisitiza kama mgombe haba pesa, hawezi kushinda nafasi ya
Halmashauri Kuu (NEC).

“Gharama za maisha zimepanda, elimu imeshuka na kusababisha Watanzania
waishi bila ya matumaini katika nchi yao, Tanzania hakuna mwananchi
anayepata haki kama binadamu,” alisema.

Akitolea mfano wa Shekhe Ponda Issa Ponda na kudai hadi sasa amenyimwa
dhamana wakati kisheria kesi yake alistahili kuipata lakini hadi sasa
anaendelea kusota rumande.

Prof. Lipumba alilalamikia muda mchache waliopewa wananchi kutoa maoni
ya Katiba Mpya tofauti na wanavyofanya katika nchi zingine ambazo hutoa
muda wa mwaka mmoja kama Kenya.

SOURCE; MAJIRA
 
Nafika mahali mtu anayeelewana na ccm na kuunda naye serikali nakosa kabisa kuamini maneno yake. Halafu maneno yake yanaonekana mepesi kweli kwanini asiseme wanakusudia kupressurelize serikali ili ilazimike kutekeleza anayodhani ni sawa. Cha kushangaza kiongozi mwandamizi CUF Julius Mtatiro leo kaandika kwenye wall yake fb kuwa kuna watu wana kadi 2 ili waweze kuhama kirahisi kama upande walipo hapatalipa hivi kweli hii ni hoja ya maana kwa Mtatiro........ kwani nani ataenda kwenye chama flani akakataliwa kama ni mtu safi au ndo kusema SUK Zanziba imemuunganisa pia Nape na Mtatiro?
 
18 DECEMBER 2012

Na Rehema Maigala

MWENYEKI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amesema mtandao wa mafisadi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), umefanikiwa kupata uongozi kwa asilimia
75 na mikakati waliyonayo ni kuchukua nchi ifikapo 2015.

Prof. Lipumba aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akifungua mkutano wa Baraza Kuu la Taifa la chama hicho ambao wajumbe walijadili mambo 11 ya msingi.

Alisema chaguzi mbalimbali za CCM zilizofanyika hivi karibuni, zilitawaliwa na vitendo vya rushwa kwa wagombea wasioa na sifa za kuwa viongozi na wenye masilahi binafsi badala ya chama.

"Chaguzi za CCM zilitawaliwa na rushwa hasa wa wanawake, mafisadi wasipewe nafasi ya kuongoza nchi na safari hii, hatuta kubali wachaguliwe viongozi wenye masilahi binafsi," alisema.

Alisema Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli, mkoani Arusha, Bw. Edward Lowassa, naye aliwahi kulalamikia vitendo vya rushwa ndani ya chama na kusisitiza kama mgombe haba pesa, hawezi kushinda nafasi ya Halmashauri Kuu (NEC).

"Gharama za maisha zimepanda, elimu imeshuka na kusababisha Watanzania waishi bila ya matumaini katika nchi yao, Tanzania hakuna mwananchi anayepata haki kama binadamu," alisema.

Akitolea mfano wa Shekhe Ponda Issa Ponda na kudai hadi sasa amenyimwa dhamana wakati kisheria kesi yake alistahili kuipata lakini hadi sasa anaendelea kusota rumande.

Prof. Lipumba alilalamikia muda mchache waliopewa wananchi kutoa maoni ya Katiba Mpya tofauti na wanavyofanya katika nchi zingine ambazo hutoa muda wa mwaka mmoja kama Kenya.

SOURCE; MAJIRA

Hapo Majira nimewaelewa na mlengo wenu. Maana kuna watu hawana huo msamiati wa rushwa kwenye maongezi yao nyie mnawawekea maneno ndani ya mdomo
 
hivi kwa nini lipumba akiongea watz hawamchukulii seriously?
 
Mbona Lipumba hajawahi kusema ''hadi sasa makanisa 25 yamechomwa Zanzibar na hakuna aliefikishwa Mahakamani?
 
18 DECEMBER 2012

Na Rehema Maigala

Alisema chaguzi mbalimbali za CCM zilizofanyika hivi karibuni, zilitawaliwa na vitendo vya rushwa kwa wagombea wasioa na sifa za kuwa viongozi na wenye masilahi binafsi badala ya
chama.

"Chaguzi za CCM zilitawaliwa na rushwa hasa wa wanawake, mafisadi wasipewe nafasi ya kuongoza nchi na safari hii, hatuta kubali wachaguliwe viongozi wenye masilahi binafsi," alisema.

Kwa maelezo haya, Lipumba anaamini kuwa watakaoshika nafasi za uongozi ndani ya CCM ndio watakaoongoza nchi, je kwa nini anagombea?

Yeye ndio anajua kiongozi gani ana sifa ya kuiongoza CCM na yupi hana sifa? Kama anaamini waliochaguliwa hawafai ila wapo wanaofaa, suala ni yeye kuingia ndani ya CCM na kufanikisha hao anaowaona yeye wanafaa waingie madarakani na sio kuwa kiongozi wa CUF

"Gharama za maisha zimepanda, elimu imeshuka na kusababisha Watanzania waishi bila ya matumaini katika nchi yao, Tanzania hakuna mwananchi anayepata haki kama binadamu," alisema.

Akitolea mfano wa Shekhe Ponda Issa Ponda na kudai hadi sasa amenyimwa dhamana wakati kisheria kesi yake alistahili kuipata lakini hadi sasa anaendelea kusota rumande.

Haki gani anayoizungumzia Lipumba? Kitu pekee hapo nilichoweza kukiona ni lalamiko lake kuhusu ELIMU. Ni kweli, Shekhe Ponda angekuwa alipatiwa elimu, usingekuta amefanya ujinga kama aliofanya mpaka leo yupo gerezani.

Lakini Lipumba hakuacha kuongezea PUMBA, anasema KISHERIA kesi ya Ponda inastahili dhamana, lakini Lipumba amekuwa mwepesi wa kutuambia KISHERIA, KISHERIA ila
huwa hasemi ni sheria namba ngapi, ya nchi gani na katiba ipi. Ni profesa huyu huyu alisema ile kesi ni ya madai.
 
Kimwili CUF Kiroho CCM lipumba bwana mbona ndoa ya Zenzi hamjaivunja?
 
huu mkutano wa kamati kuu ni CUF AU CCM naona hoja nyingi ni za tathmini ya chaguzi za ndani ccm wapi tathmini ya chaguzi za cuf au huyu ni msemaji wa ccm bado wa cuf hajafika mkutanoni
 
Serikali hii yenyewe iliopo madarakani iliingia kwa nguvu za mafisadi...
 
18 DECEMBER 2012

Na Rehema Maigala

MWENYEKI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amesema mtandao wa mafisadi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), umefanikiwa kupata uongozi kwa asilimia
75 na mikakati waliyonayo ni kuchukua nchi ifikapo 2015.

Prof. Lipumba aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akifungua mkutano wa Baraza Kuu la Taifa la chama hicho ambao wajumbe walijadili mambo 11 ya msingi.

Alisema chaguzi mbalimbali za CCM zilizofanyika hivi karibuni, zilitawaliwa na vitendo vya rushwa kwa wagombea wasioa na sifa za kuwa viongozi na wenye masilahi binafsi badala ya chama.

“Chaguzi za CCM zilitawaliwa na rushwa hasa wa wanawake, mafisadi wasipewe nafasi ya kuongoza nchi na safari hii, hatuta kubali wachaguliwe viongozi wenye masilahi binafsi,” alisema.

Alisema Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli, mkoani Arusha, Bw. Edward Lowassa, naye aliwahi kulalamikia vitendo vya rushwa ndani ya chama na kusisitiza kama mgombe haba pesa, hawezi kushinda nafasi ya Halmashauri Kuu (NEC).

“Gharama za maisha zimepanda, elimu imeshuka na kusababisha Watanzania waishi bila ya matumaini katika nchi yao, Tanzania hakuna mwananchi anayepata haki kama binadamu,” alisema.

Akitolea mfano wa Shekhe Ponda Issa Ponda na kudai hadi sasa amenyimwa dhamana wakati kisheria kesi yake alistahili kuipata lakini hadi sasa anaendelea kusota rumande.

Prof. Lipumba alilalamikia muda mchache waliopewa wananchi kutoa maoni ya Katiba Mpya tofauti na wanavyofanya katika nchi zingine ambazo hutoa muda wa mwaka mmoja kama Kenya.

SOURCE; MAJIRA

Mimi binafsi huwa nashindwa kuitenga CUF na udini. Kwani watanzania wangapi wamekosa dhamana kutokana na uongozi mbovu tulionao, leo huyu jamaa anaye hatarisha usalama wa raiå ndo kamuona tu.

Hakuwahi kuongeleah tukio la kuchoma makanisa na mali za kanisa. Hafai kuwa kiongozi wa watanzania kwa maoni yangu.

😱
 
Lipumba asilaumiwe kwa CCM na CUF Zanzibar, issue ya Zanzibar ni zaidi ya Lipumba na inajulikana vizuri CUF wamekuwa ngome imara Zanzibar na inasemekana wameshinda chaguzi nyingi za mwanzoni. Huo muungano wa CUF na CCM Zanzibar uliwekwa kuepusha matatizo kama yaliyotokea miaka ya nyuma.
Lipumba amejimaliza kisiasa mwenyewe badala ya kufanya harakati ya kuimarisha chama bara amebaki akilalamika, kuiondoa CCM madarakani inatakiwa umoja wa vyama vya upinzani kwa nguvu moja na kuondoa udini, ukanda etc kwa vyama vyote.
 
Back
Top Bottom