Prof Lipumba Kujihakikishia Uwaziri Mkuu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Prof Lipumba Kujihakikishia Uwaziri Mkuu?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by akashube, Oct 12, 2010.

 1. akashube

  akashube JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2010
  Joined: Dec 24, 2009
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Kama kuna wakati muhimu kwa chama cha wananchi CUF kufanya maamuzi ya busara basi wakati huo bila shaka ni sasa. Kwa kuwa CHADEMA kinamuuna mkono maalim Seif Zanzibar itakuwa ni jambo la busara kwa Prof Lipumba kumuunga mkono Dk Wilbrod Slaa hivi sasa ili awe mgombea wa Urais wa Muungano anayeungwa mkono pia na CUF.

  Je hii haitamuhakikishia Prof Lipumba uwaziri mkuu, nafasi nyeti ya kushiriki kuunda serikali bora kabisa ya Muungano wa CHADEMA na CUF? Je wakuu wana JF hili mnalionaje?

  Je huu sio wakati wa kumwaga udongo wa mwisho kwenye kaburi la CCM?
   
 2. Ninja

  Ninja JF-Expert Member

  #2
  Oct 12, 2010
  Joined: Feb 5, 2010
  Messages: 318
  Likes Received: 275
  Trophy Points: 80
  mnaogopa utafiti?
   
 3. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #3
  Oct 12, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Ingikuwa nzuri sana!
   
 4. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Mi nakuwa na wasiwasi na wapinzani wengine. Kama kweli wapinzani wangeungana,ccm ingepumua? Naisi wengne wako kama mrema/shushushu aliyetumwa 1995 kuua upinzani. Lipumba akitaka kupata nchi amuunge mkono slaa,tupate Uhuru wa Tanzania.
   
 5. T

  Tofty JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2010
  Joined: Nov 6, 2008
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  hii ni idea nzuri ingawa sidhani kama itaweza kutokea kwani ndoto ya lipumba ni kuingia ikulu akiwa raisi!
   
 6. J

  Jafar JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Sheria iliyotungwa na CCM hairuhusu vyama kuungana katika kuunda serikali - labda iwe ni hiari (descresion) ya Rais mwenyewe. Cha maana tuwe na wabunge wengi tuipindue hii sheria ili nchi iwe na amani ya kweli.
   
 7. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #7
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 414,924
  Trophy Points: 280
  Kazi hiyo CUF kamwe hawataifanya kwa sababu malengo yao ya kismingi yatofautiana na Chadema.

  Mfano CUF wanataka nchi ijiunge na OIC na uanzishwaji wa mahakama za kadhi mambo ambayo Chadema haiafiki hata kidogo.
   
 8. Kiraka

  Kiraka JF-Expert Member

  #8
  Oct 12, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 2,550
  Likes Received: 612
  Trophy Points: 280
  Gsana
  Mimi pia nina mawazo kama yako, hivi kweli kama lengo ni moja kuondokana na hili dudu liumalo.... njia rahisi kuliko zote ilikuwa ni kusema Kura ambazo mngenipa mimi mpeni huyu... inakuwa kama kumsukuma mlevi.....
  Still unakuwa uko within the sheria yao... na yeye akiwa Rais anasema naamua kumpa uwaziri mkuu/waziri wa fedha huyu bwana pamoja na kuwa anatoka chama kingine!!

  Mi nadhani kama kweli wanatakia mema Taifa letu tukufu kuna haja ya kufikiria mikakati kama hii.
   
 9. Kiraka

  Kiraka JF-Expert Member

  #9
  Oct 12, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 2,550
  Likes Received: 612
  Trophy Points: 280
  lengo lingekuwa kuondokana na hawa wahuni kwanza!!! mengine yote yanawezekana tu....
  Sasa kuliko kukosa yote kwa kugawana kura zetu si afadhali kukubaliana....
  I wish watu wapate kufikiria hili....
   
 10. amba.nkya

  amba.nkya JF-Expert Member

  #10
  Oct 12, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 431
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Nakubaliana nawe kwenye RED, Tatizo la vyama vya siasa Tz ni kuganga njaa, ubinafsi na uroho wa madaraka. Wangekuwa na nia ya kuleta mapinduzi ya kweli dhidi ya CCM, wangeunda chama kimoja cha upinzani chenye nguvu kupambambana na CCM. Other wise, they are kidding.
   
 11. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #11
  Oct 12, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Rutashubanyuma

  Inawezekana ingawa ni ngumu kwa kila upande, lakini malengo nini siyo misaafu kwamba haiwezi kubadilishwa. Kumbuka Conservative na Liberal dems za UK zilikuwa na misimamo tofauti hadi siku ya uchaguzi lakini baada ya uchaguzi siku mbili zilitosha kubadili malengo yao.
   
 12. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #12
  Oct 12, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  mtuache tutaunda serikali wenyewe bana
   
 13. Kiraka

  Kiraka JF-Expert Member

  #13
  Oct 12, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 2,550
  Likes Received: 612
  Trophy Points: 280
  Kigogo
  Sikatai hilo lawezekana, lakini je unavyofikiria kwa kuwa na makubaliano ya namna hiyo, yenye lengo moja muhimu kwanza kuwang'oa CCM, hivi huoni kuwa close to 100% success inakuwa guaranteed?
   
 14. g

  guta Senior Member

  #14
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 179
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  katiba inasema ili uwe waziri mkuu lazima utokane na chama chenye wabunge wangi, na uwe mbunge wa kuchaguliwa. Lipumba siyo mbunge
   
 15. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #15
  Oct 12, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  CUF NI CCM B SASA UNATEGEMEA NINI?

  [​IMG]  [​IMG]

  [​IMG]


  [​IMG]
   
 16. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #16
  Oct 12, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Hujui kuwa ccm na cuf wameingia kwenye maridhiano?Wakimuunga Slaa basi watakuwa wanajihatarishia nafasi yao huko Zanzibar.
   
 17. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #17
  Oct 12, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Kwa kweli nimeamini CUF = CCM Underground Family, mie namfuhamu mkewe Lipumba huwa anadai kuwa mumewe ni CCM damu na kadi yao anayo mpaka leo
   
 18. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #18
  Oct 12, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Acheni usanii mkuu!! Kwa CHADEMA gani ya kuiachia CUF ZNZ?! Ni kura ngapi ambazo CHADEMA ingepata ZNZ ambazo imeamua kuwaachia CUF?! Pigeni mzigo, acheni ujanjaujanja!!
   
 19. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #19
  Oct 12, 2010
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Mkuu, una maana Uwaziri Mkuu KIVULI?
   
 20. Kionambele

  Kionambele JF-Expert Member

  #20
  Oct 12, 2010
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 242
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mkuu uko analytical vibaya mno.
   
Loading...