Ngoja wakunywee viroba waje
Sijawahi kunywa pombe maishani mwangu. Jee nikimpinga Lipumba nitakuwa nimekunywa kiroba? Ujinga wenu ndiyo mauti ya taifa, kwani kwa bahati mbaya sana chama chenu ndiyo kinaongoza Serikali ya taifa letu kwa sasa! Ni kama laana kuwa na CCM Madarakani.
Hapo wengine tunajua Lipumba anazungumzia nini na nini kitafuatia baada ya hapo. kwa taarifa yako Lipumba atateuliwa na Magufuli kuwa Mbunge, halafu yeye kwa ujinga wake anatengeneza mazingira kwamba CUF ndiyo yenye uhalali wa kushutumu serikali kwa hivyo ndiyo yenye haki ya kuunda Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na yeye ndiye anatamani kuwa kiongozi wake. CCM imekuja na mkakati mpya wa kuisambaratisha UKAWA.
Kama Lipumba ni mtu anayeaminika ndani ya chama chake kwa nini alishindwa kukataa muungano wa UKAWA kumpokea Lowassa. Falsafa haijengwi kwa tukio bali kwa jinsi tukio linavyotafsiriwa na anayeliona, kwa maana nyingine Lipumba analiona tukio la CHADEMA kumpokea Lowassa kama vile vile anavyoliona Kinana au Slaa. Ni ajabu sana mitizamo ya watu hawa watatu kwa sasa kufanana kama watoto mapacha wanaotoka kwenye mfuko mmoja wa uzazi.
Hoja yangu hapa ni kwamba ukimkuta Msabato au Muislam ukawauliza Nguruwe ni Nyama haramu au halali, bila shaka watakwambia ni haramu, dini mbili tofauti lakini mtazamo mmoja. Na ukikutana na Mkatoliki au na Mtu anayeabudu mzimu bila shaka kwao nguruwe ni nyama halali kabisa tena inanoga kupita nyama zote. Hawa nao dini mbili tofauti toka kwenye misingi isiyofanana kabisa lakini wana mtazamo mmoja!
Kufanana kwa mitazamo hakuji kiholela bali kunatokana na misingi mahsusi ambayo hujengwa juu ya falsafa. CCM wanaigopa UKAWA ikiwa na Lowassa na Lipumba naye UKAWA ikiwa na Lowassa imemtumbukia nyongo. Wote Lipumba na CCM wanahofia nafasi zao kisiasa kwa uwepo wa Lowassa.
Kuna swali Lipumba ameulizwa mara nyingi kuwa kama Mwenyekiti amefanya nini kukijenga chama kabla ya "Fisadi" Lowassa kukaribishwa UKAWA mpaka sasa hana jibu, na wala hatapata jibu kwani anakodokolezea (CCM) nao hawana jibu au wanajua wao ndiyo chanzo cha CUF kuwa hivi ikiwa mikononi mwa Lipumba hivyo hawatamwambia jibu ni nini!