wewe ndio hauchambui mada vizuri, lazima ujue lipumba alisema nini mara ya kwanza juu ya mengi
RA, manji na wenzake wanamatatizo siku nyingi mbona huyo Lipumba hajawahi kumuhimiza JK awachukulie hatua, DR Slaa amekuwa akilia peke yake utasema yeye ndio yuko kwenye chama cha upinzani peke yake
Lipumba amesema huo ugomvi hauna tija kwa taifa, halafu baadae akasema RA amesema mambo ya maana juu ya NBC kuhusu mengi. Mengi alivoongea juu RA, manji et al LIPUMBA AKAMWAMBIA MENGI ANASABABISHA UBAGUZI NA ANAJIPENDEKEZA KWA RAIS WALA HAKUMWOMBA RAIS AYASHUHULIKIE YALE ALIYOSEMA MENGI, LAKINI RA ALIVYOONGEA YA MIKOPO YEYE AMEYAONA YA MAANA, JE KWA NINI?????????
LIPUMBA NI KAMA VILE SOFIA SIMBA ALIVYOMUAMBIA MENGI KACHEMSHA NA RA ALIVYOONGEA AMEKUA BUBU, "BUBU AMBAYE ATAKI KUSEMA" ANGALAU WA JF ANASEMA
kutoka mwananchi
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF) Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba amesema malumbano ya wafanyabiashara yanayoendelea kushika kasi nchini kuhusiana na ufisadi, hayana tija kwa taifa badala yake yanalitoa katika harakati zake ya kukabiliana na changamoto za maendeleo.
Profesa Lipumba alisema hayo jana katika mahojiano na gazeti hili kuhusiana na kauli ya mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Aziz aliyemtuhumu Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi kuwa ni nyangumi wa ufisadi.
Alisema malumbano hayo yanawafanya Watanzania wengi kuacha kujadili mambo muhimu ya kimaendeleo na kubaki kwenye fitina zinazosambazwa na wafanyabiashara hao.
Aliitaka serikali ya Rais Jakaya Kikwete kukomesha tabia ya wafanyabiashara kukamiana kupitia vyombo vya habari, kwa lengo la kuwashirikisha wananchi kwenye chuki zao ambazo zinaotesha mbegu za rangi na ukabila, hivyo kutishia amani ya nchi.
Tanzania ni nchi maskini ingawa tuna rasilimali nyingi. Tumekuwa na tatizo kubwa la kushindwa kujipanga vizuri katika kuzitumia. Kwa jinsi suala hili la ufisadi linavyokwenda, linazidi kutuvuruga, alisema Lipumba na kufafanua: Mijadala (malumbano) hii inazidi kututoa kwenye mstari.
Hata hivyo, alisema katika maelezo ya Rostam, ambaye pia ni Mbunge wa Igunga, kuna hoja nzito alizozitoa na ambazo zimewafumbua macho Watanzania, hivyo Rais Kikwete hana budi kuzishughulikia kikamilifu.
Alitaja miongoni mambo hayo kuwa ni tuhuma kuwa Mengi alikopa mabilioni Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kabla haijabinafsishwa na hakurejesha na vile vile alichukua mabilioni mengine kwenye mfuko unaochangiwa na wahisani; Kuagiza Bidhaa kutoka Nje (CIS) ambazo pia hakuzirudisha serikalini kama ilivyo utaratibu wa mfuko huo.
Aliitaka Wizara ya Fedha na Uchumi kuutangazia umma wote waliokopa NBC na CIS na kuwaamuru walipe na kwamba, wachukuliwe hatua kama ilivyokuwa kwa mafisadi wengine waliochota mabilioni ya fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Profesa Lipumba, alisema kama nyaraka zinazohusu fedha za CIS zitakosekana Hazina, serikali iwasiliane na nchi wahisani wa mfuko huo, kwa sababu wana kumbukumbu za kampuni zote zilizokopa.
Alimtaka Rais Kikwete kuonyesha dhahiri nia yake ya kupambana na ufisadi kwa kutowaonea huruma wafanyabiashara wote wawili ambao kila mmoja anaonekana yuko karibu naye (rais).
Profesa Lipumba alisema anamtambua Rostam kuwa ni Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mengi ni mwanachama wa CCM ambaye amekuwa akijinadi kuwa anamsaidia Rais Kikwete kwenye vita dhidi ya mafisadi; hivyo akasisitiza wote wako karibu na Rais Kikwete.
Alisema fedha za Mfuko wa CIS hutolewa na wahisani ili kuwasaidia wafanyabiashara kuagiza bidhaa nje na hutakiwa kurejeshwa serikalini kwa shughuli nyingine za maendeleo, hivyo kama hazikurudishwa, huo utakuwa ni wizi wa mali ya Watanzania.
Kuhusu EPA, Profesa Lipumba aliendelea kusisitiza kuwa ripoti ya awali ya ukaguzi ilionyesha kampuni ya Kagoda ilighushi nyaraka ili kuzichota hizo fedha, hivyo haoni sababu ya serikali kutowapeleka mahakamani wahusika au wamiliki wake ambao mpaka sasa wanafichwa.
lipumba unataka kikwete amshughulikie mengi je marafiki zako RA, manji(nssf). tanil, jetu et al vipi.
Mengi ameshamaliza hizo kesi zote mahakamani!
Kweli RA payroll yake ni kubwa mpaka Lipumba....!
Joka Kuu ktk Pumba ulizozitoa ni hizi...kama upenzi wako wa Chadema ili CUF ionekane inawachukia wakristo endelea....huku ni kufilisika kifikra....kela72,
..mara ya mwisho nilisikia Prof ameoa mwanamke toka lile kabila linalochukiwa kabisa hapa jamii forums.
..pia mwanamke huyo ni alikuwa muumini wa dini inayochukiwa na chama cha CUF.
Nimesoma post huku nimebana pumzi, siamini Lipumba kama anakuja na mashambulizi namna hii dhidi ya mtu aliyejitoa mhanga kuwataja mafilisi wa nchi hii!
Sasa naanza kuamini kuwa Lipumba si tu kwamba yupo ktk payroll ya mafilisi bali pia zile kelele zake alizokuwa anapiga dhidi ya mafisadi ni kwamba alijua hakuna hatua zitakazochukuliwa dhidi yao na alikuwa tu anatimiza wajibu ili kupata reputation ya kisiasa. Wanasiasa bwana ni kama upepo vile.
Anyway sasa naamini kuwa CUF si chama makini kama alivyosema Prof. Safari na wanajua wanachokifanya, they just stir in order to survive and who knows, may be wanasiasa wa kulipwa.
Yaleyale ya Kipofu na Jogoo! Wacha kujifanya kipofu. Hebu soma para ya mwisho ya maelezo uliyotuletea, kwani si mnasema Kagoda ni Rostam? Akili zenu ziwe macho kuliko ushabiki!!!!!!!
Msiumize vichwa sana, kama alivyofanya nyakati za DOWANS ndivyo anavyofanya nyakati hizi.
Inabidi hawa wanasiasa uchwara na wapenda hela bila kuangalia maslahi ya taifa wawe wanaangalia timing. Si kila jambo kubwa utie domo ili kutafuta umaarufu, tumeni makanjanja wenu waboronge tutaacha lakini kwa mwendo huu nazidi kumwona Lipumba kilaza tu, anajaribu kutafuta jinsi ya kusikika upya.
Nonesense!!!!!!!!!!!!!!!!!
mbona hakumtaja na slaa ashughulikiwe? kwa kuwa naye aliwataja tena kwa mapana na kina kama alivyowataja Mengi.
mkuu nomba ku-differ hapo
as far as this debate concern bado tuko kwa mengi na rostam. Slaa si mpumbavu kama mengi, slaa ana data na bado ni msafi hatujapata maovu yake na kama yatatolewa naye ataandamwa.
kela72,
..mara ya mwisho nilisikia Prof ameoa mwanamke toka lile kabila linalochukiwa kabisa hapa jamii forums.
..pia mwanamke huyo ni alikuwa muumini wa dini inayochukiwa na chama cha CUF.
Wadini na Wakabila ni sawa na.................... hata wakitiwa ndani ya chupa watatoa japo vidole. Vyereje dini na kabila iwe issue kwa hili. Poleni nyie kumbe mna watu fulani mnaowachukia kutokana na kabila zao na dini? Shame on you all whoever mwenye tabia hiyo humu.
Huyu Lipumba naye yumo mifukoni mwa mapapa mafisadi akitafuna mapesa yao taratibu. Ama kweli viongozi wetu wa nchi yetu ni mandumila kuwili wa hali ya juu na pia ni viongozi uchwara.
wewe ndio hauchambui mada vizuri, lazima ujue lipumba alisema nini mara ya kwanza juu ya mengi
RA, manji na wenzake wanamatatizo siku nyingi mbona huyo Lipumba hajawahi kumuhimiza JK awachukulie hatua, DR Slaa amekuwa akilia peke yake utasema yeye ndio yuko kwenye chama cha upinzani peke yake
Lipumba amesema huo ugomvi hauna tija kwa taifa, alafu baadae akasema RA amesema mambo ya maana juu ya NBC kuhusu mengi. Mengi alivoongea juu RA, manji et al LIPUMBA AKAMWAMBIA MENGI ANASABABISHA UBAGUZI NA ANAJIPENDEKEZA KWA RAIS WALA AKUMWOMBA RAIS AYASHUHULIKIE YALE ALIYOSEMA MENGI, LAKINI RA ALIVYOONGEA YA MIKOPO YEYE AMEYAONA YA MAANA, JE KWA NINI?????????
LIPUMBA NI KAMA VILE SOFIA SIMBA ALIVYOMUAMBIA MENGI KACHEMSHA NA RA ALIVYOONGEA AMEKUA BUBU, "BUBU AMBAYE ATAKI KUSEMA" ANGALAU WA JF ANASEMA
WEWE NDIO MPUMBAVU NA SIO MENGI
kuna mtz gani binafsi anyepambana na ccm ambaye si mwana siasa
leo hii wewe unamuona mengi mpumbavu, mengi akiamua kukaa kimya kutaka ippmedia iimbe ccm, inchi itakuwa wapi?
Mengi ameweka biashara yake hatiani kwa ajili ya wa tz, mengi got so much to loose than any tanzanian in this saga....
Mengi akitaka ccm wanampa mafao na anakaa kimya na magazeti yake hayaandiki habari yeyote ya ufisadi, kaa chini ufikirie kidogo...
He is putting his personal wealth at risk because of you people..
Lipumba si Mnyamwezi? Chuma usimtetee. Hajaanza leo wala jana.
Alikuwa mshauri wa Mwinyi wa Uchumi. Matokeo yake mnayakumbuka.
MENGI NI MPUMBAVU KAMA ULIVYO WEWE< SEMILONGO
Hivyo Mengi alikwambia wapi kuwa anapambana na CCM? Umeisahau kauli yake kuwa anamsaidia JK? Nimeamini sasa ujinga wako upo wapi.Upo katika kusahau haraka hata kile SHUJAA wako anakisema.
Ama kwa ujinga wa Mengi upo kwa vile hana msimamo. Hebu niambie Mengi anasaidia CCM au anamsaidia nani hasa iwapo anatowa misaada kwa mgongo wa CCM na kufuatana na viongozi wa CCM wakati hao viongozi wa CCM wanapanga kummaliza kwa mujibu wa taarifa zenu humu humu. Ondowa Jazba na uwe na hoja tafadhali.