PROF. Lipumba anaposahau alikotoka.....! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

PROF. Lipumba anaposahau alikotoka.....!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Wa Kwilondo, Dec 10, 2010.

 1. Wa Kwilondo

  Wa Kwilondo JF-Expert Member

  #1
  Dec 10, 2010
  Joined: Sep 15, 2007
  Messages: 1,083
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  ….Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa maadhimisho hayo Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba alisema kuwa hatua ya CHADEMA kususa sherehe hizo ni kutokomaa kisiasa kwa kuwa suala hilo linagusa Watanzania wote na si la kisiasa.
  Wakati huo huo, Prof. Lipumba aliwabeza watu wanaopinga Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar na kusema kuwa wanaofanya hivyo hawaitakii mema nchi hiyo na Tanzania kwa ujumla na kama ni wanasiasa
  hawajui wanachokifanya. “Hatua hii imetibu majeraha yaliyokuwepo na kuwaunganisha Wazanzibari...walikubaliana kuwa na serikali hii ili iwaunganishe na kumaliza matatizo yaliyokuwepo
  tangu awali ambayo hayakuwa na amani hata kidogo na ukiwa unazungumzia serikali hii kwa Zanzibar vyama vyenye nguvu ni CUF na CCM ambavyo vimeungana na kama kuna mtu anaona kuna kosa haitakii mema
  na kama ni kiongozi wa kisiasa basi si mwenye busara na kama ana shughuli zake zingine kama za disko basi aende huko na sio kazi ya siasa kwani ukibeza hatua hiyo basi hujui siasa na huijui Zanzibar,” alisema Prof.
  Lipumba.
  Source: Majira
  My take:
  Prof. amesahau ya kule Zanzibar walivyo kuwa wanasusia. Wao ni CCM-B hivyo hakuna haja ya kuwasemea upinzani. Na kama yeye amekomaa kisiasa mbona ktk chaguzi zote anaambulia patupu?
  CUF ni wazandiki, Wanafiki na wanasahau historia. Wao walikua vinara wa migoma sasa wamekua CCM B wanaona wenzao wanafanya makosa. Ameombwa na nani kutolea maoni CHADEMA? Aiache CHADEMA itasema yenyewe na kutoa tamko kuhusu Sherehe hizo za uhuru. Kweli Nyani haoni...............
  Wabara wanapaswa kuamka sasa ili wasichezewe na wazanzibar ambao nia yao ni kufaidi Muungano wa Tanzania na Zanzibar huku sisi wabara tukiendelea kuwabembeleza. Wao wakijifanya wanaonewa kumbe wanatufirisi.
   
 2. M

  Mtu wa Mungu JF-Expert Member

  #2
  Dec 10, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwani nani asiyejua kwamba Li-pumba siyo mwnasiasa, ndiyo maana kule zenj yeye ni mgeni, maalim ndiyo rais wa kafu!!!!!!!!!!!!!
   
 3. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #3
  Dec 10, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Lipumba siku hizi anafaidika kwa kupita mlango wa nyuma na serikali ya Umoja huko visiwani; bila shaka kama mwenyekiti wa chama shiriki katika serikali ana maslahi binafsi yanayotekelezwa toka visiwani kwahiyo ndio maana amekwisha sahau kuwa kuna wazanzibari waliouawa na serikali ya CCM kwa kudai kile walichoamini kuwa ndio haki yao na wengine wakakimbilia uhamishoni huko Somalia!! Kile CUF walichokuwa wanadai ndicho hicho hicho Chadema wanadai huku bara sasa huko kutokomaa kwa siasa kuna toka wapi? Mbowe amekwisha kuwa mbunge wa kuchaguliwa mara mbili sasa, lakini Lipumba hajawahi hata kuwa diwani wa kuchaguliwa acha huo ubunge; sasa kati ya hawa wawili nani mkomavu wa siasa?
   
 4. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #4
  Dec 10, 2010
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  naipenda siasa kwani ni mchezo mchafu.....yesterday you were out..today you are in and tomorrow you will be out.......! NA KOTE HUKU UTAKUWA NA MITAZAMO TOFAUTI NA UTAITETEA UKIITA NI MISIMAMO YA CHAMA
   
 5. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #5
  Dec 10, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Lipumba kachoka kuwa Mpinzani anaona hataweza tena, kwisha habari yake! Sasa hivi yuko tayari kuchukuwa hata ukuu wa wilaya akipewa!
  Siasa inahitaji moyo ilikufikia malengo yake. Hawa jamaa wa siasa chafu za Ngangari sasa wanajiona wamefanikiwa sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

  kupewa umakamu usiokuwa na mchango wowote zaidi ya kumwakilisha Shein kwenye sherehe za mauldi na mikutano ya chaichai tu. There is nothing substantial will be given to Seif to manage, yetu macho. Hawaijui CCM kuwa haina chembe ya honest hata kidogo yatawatokea puani na wataona aibu kurudi kuomba msamaha. Lipumba pamoja na kuwa Prof lakini hajatambua kuwa hana mvuto kwa watanzania hata angegombea mpaka Yesu arudi hatakaa apate Uraisi nchi hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
   
 6. F

  Froida JF-Expert Member

  #6
  Dec 10, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Arudi UDSm akaendeleze libeneke la kufundisha vijana pale,anahitajika zaidi huko kuliko kukaa na kuropokaropoka mambo yasiyo mhusu
   
 7. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #7
  Dec 10, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,621
  Likes Received: 4,725
  Trophy Points: 280
  Katika jina lake mwisho ongeza VU
   
 8. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #8
  Dec 10, 2010
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  hakuna upinzani wa kudumu katika siasa.
   
 9. HISIA KALI

  HISIA KALI JF-Expert Member

  #9
  Dec 10, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaishiwa hoja za siasa. Na hili ni lazima kwa sababu yuko kwenye kambi ya vyama vya upinzani wakati sio mpinzani wa Kweli. Mtu yeyote ambaye hana msimamo lazima hatakuja na maneno ya kuchanganya tu. Na watu wengi watashindwa kumuelewa. Na ikifika hapo basi mtu huyo atakuwa amefilisika kihoja.
   
 10. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #10
  Dec 10, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kwani CHADEMA wao nao hawajaondoka patupu na Slaa wao, kiasi cha kwamba mzee watu haonekani tena kwenye jamii anajificha ficha tu, duh kushindwa kubaya sana
   
 11. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #11
  Dec 10, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Na wewe andika 'FREEDOM' sio 'FREDOM'
   
 12. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #12
  Dec 10, 2010
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Ni kweli lkn lipumba kazidi.. Mara zote kashindwa. Kapitwa hata na mrema mbunge.
   
 13. N

  Nonda JF-Expert Member

  #13
  Dec 10, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Nitaurudia huu msemo mara nyingi tu,
  Mafahili wawili wapiganapo ziumiazo ni nyasi.

  CHADEMA na Wafuasi wake wanawapaka tope na wanakirushia madongo CUF. CUF na Wafuasi wake wanafanya hivyo hivyo kwa CHADEMA.

  Name calling, kama hiyo kuongeza –vu katika jina la Prof. au DJ ni kuonesha kuwa upinzani una safari refu. Ni kweli baada ya Uchaguzi kila chama kina majeraha lakini kurushiana maneno, kuitana wasaliti hakuponeshi majeraha hayo bali kuongeza uchungu na hivyo kuongeza kasi ya kila mmoja wapo anapopata nafasi kumlenga shabaha mwenzake.

  Wakati Prof yuko sahihi anaposema kuwa yeyote anayekejeli maafikiano huko Zanzibar si mwanasiasa mahiri, anapomlenga kiongozi wa chama chengine, kumwambia arudi kwenye kazi ya muziki anakuwa anaondoa uzito wa kauli yake ya mwanzo na si sahihi kufanya hivyo.

  Kwa msikilizaji mshabiki, hataweza kusikia ujumbe huo ila atausikia kwa sauti kali huo ujumbe wa pili unaohusu muziki.

  Nimeshauri kuwa CHADEMA na CUF, NCCR waache hizi siasa za vita vya panzi. Waache kutumia viriri na vyombo vya habari kuhujumiana. Vyombo hivi vinapenda kukuza migogoro katika vyama vya upinzani.

  Kama kuna chama kinafikiri kinaweza kukikabili CCM pekee, kikae chini kifikiri tena !

  Na kwa wapenzi wa vyama , kwa kuongeza mafuta pale ambapo tayari moto unawaka kwa kutarajia tunauzima moto huo, tunajidanganya.
   
 14. Baiskeli

  Baiskeli JF-Expert Member

  #14
  Dec 10, 2010
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 335
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Wanjua nn atiii! sisi nkafu kushidwa na nchadehma ni haibu amiii..
   
 15. YanguHaki

  YanguHaki Senior Member

  #15
  Dec 10, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu Prof. Lipumba ni MSALITI wa ukweli kabisa. Yaani inaonesha wazi kwamba walichopigania wao kama CUF ni tumbo la viongozi wao wachache tu. Na sasa wamepata ulaji kwa staili ya Kenya na Zimbabwe wameanza kuona wenzao wote wendawazimu bila kuangalia future implications ya ndoa yao hiyo. Hebu fikiria maneno ya viongozi ya Mhe. Hamad Rashid juu ya CHADEMA kutoka nje ya Bunge na ule mdahalo na Mbowe utaona wana agenda yao. Ngoja tuendelee kuona ila so far hawaeleki hata kidogo kwa matendo na kauli zao.
   
 16. Isaac

  Isaac JF-Expert Member

  #16
  Dec 10, 2010
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 627
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  hivi alipata kura ngapi vile zinazoonesha amekomaa kisiasa?
   
 17. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #17
  Dec 10, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,621
  Likes Received: 4,725
  Trophy Points: 280
  Isikupe shida hiyo ndiyo namna yangu, ninafahamu kuwa freedom inatokana na neno free.By the way are you really genius?
   
 18. K

  Kishili JF-Expert Member

  #18
  Dec 10, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 293
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Sasa mbona kutokuonekana kwake kila wkati ni issue na wanajisikia vibaya wao kwa yeye kutoonekana? Si wakae kimya maana kwa tafsiri yenu kajificha aibu ya kushindwa ya nini kila mara oh kasusia uhuru oh alitakiwa aonekane kwenye tafrija fulani. KIMYA KINGI KINA MSHINDO MKUU. Subirini mtamwona tu simba aliyenyeshewa mmdhaniae paka
   
Loading...