Prof. Lipumba amewaimarisha CUF, amewatangaza UKAWA

Prof. Lipumba amewaimarisha CUF, amewatangaza UKAWA

Lipumba kacheza picha kama ilivyo andaliwa na Producer (ccm) hivyo kama imebuma sio kosa la sterling bali la Producer. Ndio maana pengine hata yeye alitaka mshiko wake wote kwa mpigo hakuna cha baadae ili kama picha isipouzika wasidaiane.
Kibaya ni kuwa mtu ukijijengea heshima yako kwa miaka mingi ni aibu kuiuza kwa vipande vya fedha.

Pole,pesa sabuni ya ROHO japo haikufikishi kwa Muumba wako ukichezea vibaya.Kumbuka hta Yesu na wema wake wote aliuzwa kwa VIPANDE THELATHINI VYA PESA.
 
Lipumba kacheza picha kama ilivyo andaliwa na Producer (ccm) hivyo kama imebuma sio kosa la sterling bali la Producer. Ndio maana pengine hata yeye alitaka mshiko wake wote kwa mpigo hakuna cha baadae ili kama picha isipouzika wasidaiane.
Kibaya ni kuwa mtu ukijijengea heshima yako kwa miaka mingi ni aibu kuiuza kwa vipande vya fedha.

Pesa wanasema ni SABUNI ya ROHO,japo siamini sana maana amepata pesa lakini sidhani kama ana AMANI ndani ya moyo wake.

Hii itukumbushe tu hata YESU aliuzwa kwa vipande thelethini vya dhahabu/pesa
 
Wrong timing. Kujiuzulu kwa Prof. Lipumba hakujasaidia chochote kama ilivyopangwa. Prof. Lipumba amekosea mambo kadhaa katika filamu yake ya kujiuzulu Uenyekiti wa CUF. Kwanza, amejiuzulu nafasi ya Uenyekiti na kubaki mwananchama wa kawaida hotelini. Alipaswa kuongea na wafuasi wake chamani mwake na ndipo ajiuzulu. Kujiuzulu ni jambo la kawadia,tatizo ni muda na namna ya kufanya hivyo.

Pili, Prof. Lipumba asingesafiri siku hiyo hiyo ya kujiuzulu. Angebaki kwanza ili asemwesemwe na kuandikwaandikwa kwenye media halafu ndiyo asafiri. Kitendo cha kujiuzulu na kusafiri siku hiyo hiyo kimejaza mashaka na machale kuliko uhakika wa kile. Waandaaji wa filamu yake hapa napo waliteleza na hawakuweza kupaona. Kumewaagusha na kusawajisha malengo ya chama.

Kutokana na shaka ya uhakika katika kujiuzulu kwake, Prof Lipumba ameiimarisha CUF na kuitangaza UKAWA. Filamu yake haina thamani kwa waandaaji. Imekosa soko. Kwa wabobezi tunajua kilichomuondoa Prof. Lipumba.

Kwanza,wivu wake kuwa kila anayehamia UKAWA,anahamia CHADEMA. Pili, kuchokwa kwake ndani ya CUF kama Mwenyekiti. Tatu, kutaka mambo mengi na kuonekana kuliko wengine ndani ya UKAWA.

Mambo hayo yakajenga ufa katika msimamo wake. Ufa ukatumika kupenyezea rupia. Filamu ikaandaliwa ingawa imewaangusha waandaaji. Filamu ingepangwa na kupangika vyema, muda huu tungekuwa na sherehe za ushindi. Ametuangusha!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Mzee wangu hapo ndipo nintiyo napopata AHUENI kwamba kuna watu wanalipenda TAIFA lao pamoja kuwemo kenye ile nyumba ya MAJANGILI.Ila nakuomba angalia kucha zako,macho,meno na masikio.

Inaonyesha ni kwa jinsi gani wafanyakazi wa SERIKALI yetu pamoja na RAIS wanavyoshindwa kuwa WAZALENDO.Sielewi ni akili ya UJINGA au UPUMBAVU kuhonga viongozi wa upinzani ili kuendelea kukaa madarakani!!!!!Sijui hata hawa wanoitwa TISS wako kwa ajili ya TAIFA au wafanyabiashara wanaoanzia IKULU hadi pembezoni mwa NCHI.

Hakika watu kama hawa hata WAFUNGE RAMADHANI au KWARESIMA mwaka mzima hawatasamehewa kamwe.Hivi hawaoni hata uchungu wa wale watanzania wakilala mzungu wa nne hospitali lakini wapo tayari kutoa Bilioni 3.5 kulipa binadamu mwingine?

Ninaimani pesa hizi zinatoka kwenye lile fungu la ESCROW,na hapo ndipo namuona hata huyo Magufuli kama alikuwa hajachafuka sana sasa hivi naona ndiyo wanamwagia oil chafu achafuke zaidi.Hata kwa wengine tuliokuwa na NIA ya kuharibu kura zetu kwa kumpa kwa sasa itabidi tusitishe,maana najiuliza pesa hizi zinavyomwagwa zitarudishwaje?

Rais wetu JK lionee huruma TAIFA lako japo kwa kipindi hiki kifupi ulichobakiza,ili wadanganyika tupate kukusamahehe kwa yale maovu ya kukwapua mabilioni ya ESCROW,unataka akulinde kwa lipi baya ulilotenda?

Kama unaweza Mzee wangu mwambie Rais wangu JK hata Muumba wake hata msamehe kwa hili.Chuki zake apunguze kwani kuna kesho asiyoijua!!!!!!!:embarrassed1::A S-frusty2:
 
hadi tufike oct 25 tutashuhudia mipango mingi kweli ya Mungu. ila huu wa lipumba kweli ni mpango wa Mungu maana ukawa wameongeza mshikamano zaidi tangu jamaa akimbie nchi. mipango ya Mungu ilianza jk tangu anaingia madarakani miaka kumi iliyopita. Mengi aliyafumbia macho na kuruhusu yatokee akijua au asijue kuwa anawaandaa watz kufanya mabadiliko ya mfumo wa kiutawala. tukashuhudia pia akiwaingiza bungeni viwembe kama kina Mbatia. likaja suala la uundwaji wa katiba mpya ambapo ndipo asili ya ukawa. hongera jk. ukawa ikawa imara hadi kumtisha lakini kwa kuwa ni mpango wa Mungu, shingo yake ikashupazwa.

hatujapumua likaja suala la kura za maoni ya madiwani hadi urais. hapo tukashuhudia tena ccm ikipukuchuliwa na inakaribia kubakia gunzi. sote tunajua hatima ya gunzi. hapo wanaccm mamia kwa mamia wakatorokea ukawa kutokana na udhalimu ndani ya ccm, akiwepo nguli lowassa ambaye kwa sasa ndiye anapeperusha bendera ya ukawa kuelekea uchaguzi mkuu.

hatujakaa sawa tukasikia dk slaa katikisa kidogo, kumbe hiyo yote ni mipango ya Mungu. Slaa akakaa sawa baadae kwani atazindua kampeni za ukawa. wakati ule vumbi slaa linatua ndipo tukasikia tena mvumo mwingine tokea cuf kwa lipumba. haijajulikana rasmi chanzo cha kimbunga kile ila kwa mujibu wa nyakati ni mpango wa Mungu. lipumba akaondoka zake ila kwa kuwa ni mipango ya Mungu ili agano litimie, lipumba hakung'oa hata unyoya mmoja wa ukawa. zaidi sana alisaidia watu kuungana na kukabiliana na upepo ule na hatimaye hali imerudi shwari. nenda lipumba. hujajua ni kuasi gani umeimarisha ukawa. sasa ni daima mbele nyuma mwiko.
 
Profesa Lipumba Haruna ameonesha wazi kwamba hayupo tayari kuwaletea watanzania mabadiliko kwa kuiondoa CCM madarakani kama lengo la vyama pinzani vyote nchini. Pia ameonesha ni namna gani alivyo mbinafsi na wenye kujali maslai yake mwenyewe na familia yake. Maana kama angekuwa ni mtu aliye na uchungu wa kuikomboa nchi hii kutoka kwenye mikono ya CCM asingeondoka kwa sababu alizozitoa, ukizingatia tangu siasa za Tanzania za mfumo wa vyama vingi kuanza, wapinzani hawajawai kufikia stage hii inayowapa matumaini makubwa ya kuondoka kwa CCM. Hata hivyo, Lipumba hana mvuto na ubavu wa kupambana na mgombea yeyote yule; hata kama CCM wangemteuwa Mwinyi:smile-big:.
 
well said tupa tupa filamu imebuma tayari kwa ule muziki wa leo balaa.Nadhani lumumba hakukaliki
 
Uko sawa kabisa Mtumishi wa Mungu Mr JF Junior. Kuondoka kwa Lipumba ni mpango mzima wangu. Na siasa za Tanzania mwaka huu zinachanganya watu kwa sababu moja tu kwamba ni mpango wa Jehovah ambaye akili zake hazi chunguziki na njia zake hazizoleki na wanadamu. Sababu kuu iliyomfanya Lipumba kujiuzuli ni ubaguzi wake wa kidini tuuuuuu... na si kitu kingine. Ukitaka kupata full story tafuta gazeti la DIRA la tarehe 10 - 16.
Na anajipanga kuibukia ACT-Wazalendo ili kutafuta mbinu zingine za kudhofisha UKAWA, kitu ambacho kitamgharimu sana; msemo wa wajumbe wa JF kwamba ''MAFURIKO AYAZUILIWI KWA MKONO''. Mungu akisema ''NDIYO'' hakuna awezaye kusema ''HAPANA''. HUU NI MWAKA WA TANZANIA KUKOMBOLEWA NA MUNGU. Na bado vituko vitakuwa vingi sana kabla ya Oktoba 25.
 
Back
Top Bottom