VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Wrong timing. Kujiuzulu kwa Prof. Lipumba hakujasaidia chochote kama ilivyopangwa. Prof. Lipumba amekosea mambo kadhaa katika filamu yake ya kujiuzulu Uenyekiti wa CUF. Kwanza, amejiuzulu nafasi ya Uenyekiti na kubaki mwananchama wa kawaida hotelini. Alipaswa kuongea na wafuasi wake chamani mwake na ndipo ajiuzulu. Kujiuzulu ni jambo la kawadia,tatizo ni muda na namna ya kufanya hivyo.
Pili, Prof. Lipumba asingesafiri siku hiyo hiyo ya kujiuzulu. Angebaki kwanza ili asemwesemwe na kuandikwaandikwa kwenye media halafu ndiyo asafiri. Kitendo cha kujiuzulu na kusafiri siku hiyo hiyo kimejaza mashaka na machale kuliko uhakika wa kile. Waandaaji wa filamu yake hapa napo waliteleza na hawakuweza kupaona. Kumewaagusha na kusawajisha malengo ya chama.
Kutokana na shaka ya uhakika katika kujiuzulu kwake, Prof Lipumba ameiimarisha CUF na kuitangaza UKAWA. Filamu yake haina thamani kwa waandaaji. Imekosa soko. Kwa wabobezi tunajua kilichomuondoa Prof. Lipumba.
Kwanza,wivu wake kuwa kila anayehamia UKAWA,anahamia CHADEMA. Pili, kuchokwa kwake ndani ya CUF kama Mwenyekiti. Tatu, kutaka mambo mengi na kuonekana kuliko wengine ndani ya UKAWA.
Mambo hayo yakajenga ufa katika msimamo wake. Ufa ukatumika kupenyezea rupia. Filamu ikaandaliwa ingawa imewaangusha waandaaji. Filamu ingepangwa na kupangika vyema, muda huu tungekuwa na sherehe za ushindi. Ametuangusha!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam