Prof. Lipumba aipasua CUF,CHADEMA wawapuuza

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
19,629
34,172
NDANI ya Chama cha Wananchi (CUF) kuna makundi mawili makuu, moja likimtaka Prof. Ibrahim Lipumba aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho na lingine likitaka atoswe, anaandika Happiness Lidwino.

Taarifa kutoka ndani ya chama hicho zinaeleza kuwa, kundi linalotaka atoswe limedhamiria kuvunja katiba huku kundi linalotaka arejeshwe kwenye nafasi hiyo limeapa kusimama na katiba ya chama hicho.

Taarifa zaidi zinaeleza kwamba, kundi linalotaka atoswe linafanya mkakati wa kuvunja Katiba ya mwaka 1992 Toleo 2013 Ibara ya 117 inayoeleza kwamba, “… kama hakuainisha tarehe ya kujiuzulu kwake basi mara baada ya katibu wa mamlaka iliyomteua ama kumchagua kupokea barua hiyo na kumjibu.”

Taarifa zinaeleza kuwa, maombi ya Prof. Lipumba kujiuzulu yalimfikia katibu wa mamlaka ambaye ni Maalim Seif Shariff Hamad na kwamba, kwa mujibu wa ibara hiyo, alipaswa kupeleka maombi hao katika Mkutano Mkuu wa chama hicho kuijadili barua hiyo na baadaye kujibu baada ya Mkutano Mkuu kujadili jambo ambalo mpaka sasa halijafanyika.

Prof. Lipumba aliteuliwa kutwaa nafasi hiyo na Mkutano Mkuu mwaka 1999. Ibara hiyo inaipa mamlaka mkutano huo kukubali ama kukataa kujiuzulu kwake.

“Kwa mujibu wa Katiba ya CUF Prof. Lipumba bado ni mwenyekiti wa CUF. Uenyekiti wake unakoma pale tu katibu wa mamlaka (baada ya Mkutano Mkuu) kuridhia maombi yake ya kujiuzulu na kumjibu kwa barua, Prof. Lipumba mpaka sasa hajajibiwa,” ameeleza mjumbe mmoja wa Mkutano Mkuu aliyeomba kuhifadhiwa jina lake na kuongeza;

“Watu walidhibitiwa sana kwenye mapato ya chama ndio maana wanataka asirudi, hili ndio linalosababisha hata kutaka kuvunja Katiba. Lakini cha kujiuliza kwanini wanataka kukwepa ibara ya 117? Wanajua kwenye Mkutano Mkuu wajumbe hawawezi kukubali.”

Kwa mujibu wa taratibu za CUF, Baraza Kuu halina mamlaka ya kukubali ama kukataa.

“Mpaka sasa katibu wa mamlaka halijaleta taarifa ama maombi ya kujiuzulu kwa Prof. Lipumba, tunaisuburi ije na hakuna chochote kitakachofanyika mpaka utaratibu huu ufuatwe. Hatopatikana mwenyekiti mwingine mpaka taarifa hiyo itufikie,” amesema.

Mvutano wa CUF umedhihiri juzi kwenye kongamano lililoandaliwa na Kata ya Makurumla Manispaa ya Kinondoni ambapo wajumbe waliibua hoja ya ukimya wa taarifa kuhusu maombi ya kujiuzulu ya Prof. Lipumba.

Katika kongamano hilo, Mohamed Mgomvi, mmoja wa wanachama wa CUF alisema, upande wa bara chama hicho kimebaki kwenye uyatima na kwamba hakuna mtu madhubuti anayeweza kukiendesha kama Prof. Lipumba.

“Nashangaa viongozi wetu mnasema habari zisizoeleweka juu ya kujiuzulu kwa Lipumba badala ya kusema ukweli nini kinaendelea huko ndani, tangu alipoondoka Lipumba hakuna maendeleo alafu mnasema tupo pamoja naye, haiingii akilini hata kidogo,” alisema.

Maganga Dachi, mwanachama wa CUF katika mkutano huo pia alisema, kwa mujibu wa Katiba ya CUF, barua ya kujiuzulu inatakiwa ifike katika Mkutano Mkuu uliomchagua jambo ambalo halijafanyika.

“Kwa hatua hiyo chama kinavunja Katiba maana hadi leo hakuna kinachoendelea kama hivyo suala la Lipumba, linatakiwa kuwasilishwa kwenye Mkutano Mkuu nasi tunamtaka Lipumba arudi katika nafasi yake ili chama kiendelee na shughuli za kimaendeleo,” alisema Dachi.

Ushawishi ndani ya chama hicho unaendelea kufanywa na baadhi ya wanachama pia viongozi wa chama hicho kumrejesha Prof. Lipumba kwenye nafasi hiyo.

Prof. Lipumba alijiuzulu nafasi yake mwaka jana kwa madai ya kutoridhishwa na uamuzi wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kuridhia Edward Lowassa kuepusha bendera ya umoja huo kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015 kupitia Chadema.

Akizungumza na MwanaHALISI Online leo Sheweji Mketo, Naibu Mkurugenzi wa Uchaguzi na Mipango wa CUF amesema, kwa mujibu wa Katiba ya CUF, Prof. Lipumba anayo nafasi ya kurejea kwenye nafasi hiyo.

Mketo amesema, Katiba ya chama inamruhusu mwanachama aliyejiuzulu uongozi kurudi kuwania tena nafasi yoyote kwani kujiuzulu ni haki ya mwanachama.

Akijibu hoja ya Prof. Lipumba kurejea kwenye nafasi hiyo amesema, “anaruhusiwa kurudi kama kawaida, atajaza fomu za kuomba kuwania uongozi na atapigiwa kura na baraza la chama kama wagombea wengine.”

Amesema utaratibu wa chama hicho katika kumpata mwenyekiti ni kuitisha Mkutano Mkuu ndani ya miezi sita ili kumchagua mwenyekiti mpya.

“Tatizo ni kwamba, mpaka hadi sasa bado hatujafanya kikao kutokana na kukosa fedha hivyo chama kimeongeza miezi mingine sita ambapo mkutano mkuu unatarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu,” anasema.

Chanzo: MwanaHalisiOnline
 
hao CUF wameshakufa kisiasa. Kitendo cha kumsikiliza maalim seif na kususia uchaguzi hakika kimekuwa kaburi kwa chama hicho
 
Nyie watu, Prof aliamua mwenyewe kupumzika. Hakulazimishwa na mtu, na ameonekana kuwa na msimamo wake huo wa kuendelea kuwa mwanachama wa kawaida. Sasa kwa nini watu wanajaribu kumlazimisha kuwa kiongozi?

Kwani ili uwe mwanachama mzuri wa CUF ni lazima uwe kiongozi? Give this professor a good break.

Ni hawa watu wenye njaa kwenye vyama ambao wanaamini mtu hawezi kuishi maisha ya kawaida nje ya vyama vya siasa kitu ambacho ni upuuzi mtupu. Leave him alone.

Na nimshauri tu Professa wangu, asikubali kabisa mwito huo. Aendelee kuwa mwanachama wa kawaida na aendelee kuwa mshauri wa CUF, atakuwa na amani zaidi.
 
Hatimaye naiona Tanzania isiyo na chama matumbo! Kwa heri upinzani, tulikupenda sana ila viongozi wetu walipenda fedhaa.
 
sijui kwa nini ccm wana amini CUF ni Lipumba na chadema ni Dr. slaa, sijui kwa nini hawataki kuamini kuwa ccm Ni Nyerere?
 
hao CUF wameshakufa kisiasa. Kitendo cha kumsikiliza maalim seif na kususia uchaguzi hakika kimekuwa kaburi kwa chama hicho

NAONA LEO UTAKULA VIZURI NA KULALA SAFI MANA HIZI HABARI UNAZIPENDA SANA UKISIKIA WAKO VIZUR UMAUMWA HADI NA DRIPU ZINAHUSIKA.
 
Nyie watu, Prof aliamua mwenyewe kupumzika. Hakulazimishwa na mtu, na ameonekana kuwa na msimamo wake huo wa kuendelea kuwa mwanachama wa kawaida. Sasa kwa nini watu wanajaribu kumlazimisha kuwa kiongozi?

Kwani ili uwe mwanachama mzuri wa CUF ni lazima uwe kiongozi? Give this professor a good break.

Ni hawa watu wenye njaa kwenye vyama ambao wanaamini mtu hawezi kuishi maisha ya kawaida nje ya vyama vya siasa kitu ambacho ni upuuzi mtupu. Leave him alone.

Na nimshauri tu Professa wangu, asikubali kabisa mwito huo. Aendelee kuwa mwanachama wa kawaida na aendelee kuwa mshauri wa CUF, atakuwa na amani zaidi.

Unaweza kukuta yeye Prof. Lipumba ndio yuko nyuma ya hili shinikizo la kurudi kama mwenyekiti.
 
hao CUF wameshakufa kisiasa. Kitendo cha kumsikiliza maalim seif na kususia uchaguzi hakika kimekuwa kaburi kwa chama hicho
Kibaya zaidi mwenzao MAALIM SEIF Mpaka sasa anakula mafao ya SUK.Wabunge wao kina JUSSA Wako JOBLESS,Maisha magumuu.Unyumbu mbaya sana.
 
Nyie watu, Prof aliamua mwenyewe kupumzika. Hakulazimishwa na mtu, na ameonekana kuwa na msimamo wake huo wa kuendelea kuwa mwanachama wa kawaida. Sasa kwa nini watu wanajaribu kumlazimisha kuwa kiongozi?

Kwani ili uwe mwanachama mzuri wa CUF ni lazima uwe kiongozi? Give this professor a good break.

Ni hawa watu wenye njaa kwenye vyama ambao wanaamini mtu hawezi kuishi maisha ya kawaida nje ya vyama vya siasa kitu ambacho ni upuuzi mtupu. Leave him alone.

Na nimshauri tu Professa wangu, asikubali kabisa mwito huo. Aendelee kuwa mwanachama wa kawaida na aendelee kuwa mshauri wa CUF, atakuwa na amani zaidi.
Muulize Kubenea mkuu,Mzee wa elimu ya HAPA na PALE
 
Kibaya zaidi mwenzao MAALIM SEIF Mpaka sasa anakula mafao ya SUK.Wabunge wao kina JUSSA Wako JOBLESS,Maisha magumuu.Unyumbu mbaya sana.
Akili yako inawaza pesa tu, nilivyokusoma unaweza kuuza hata utu ili ujikimu kimaisha
 
Unaweza kukuta yeye Prof. Lipumba ndio yuko nyuma ya hili shinikizo la kurudi kama mwenyekiti.

Ha ha ha, Yaweza kuwa kweli? Lakini sidhani. Nikimwangalia usoni, Prof naona wazi hawezi kufanya haya mambo. Wangekuwa wale jamaa zetu wa Tume ningekubali.
 
Kiukweli, naheshimu sana msimamo wa Prof Lipumba. Hakurupuki na wala hana maneno ya "hovyo hivyo" kama akina Dr. Mihogo. Hata waliomtilia mashaka wakati anatangaza kuachia uenyekiti CUF, sasa wamemwelewa vizuri.
 
[QUkweli Mkaruka, post: 15948693, member: 123346"]Tanzania hakuna U[inzani,kuna VITEGA UCHUMI TU VYA WATU.Chama ni CCM Tu.[/QUOTE]
Ni kweli hakuna upinzani ndio maana ZNZ CCM imeshinda kwa kishindo cha 92%
 
Kibaya zaidi mwenzao MAALIM SEIF Mpaka sasa anakula mafao ya SUK.Wabunge wao kina JUSSA Wako JOBLESS,Maisha magumuu.Unyumbu mbaya sana.
Sijui kama kuna mtu mwenye akili finyu kama wewe? Hivi unafikiri ubunge au uwakilishi ni kazi? Kwani binadamu wote ni lazima wawe wabunge na wasipokuwa wabunge basi wako jobless? Tuna wajinga wengi kama wewe ndio maana wanasiasa wanatuchezea akili zetu. Sijawahi kuona mawazo na majibu ya kijinga kama haya!
 
Back
Top Bottom