Prof. Lipumba: ACT-Wazalendo imeongeza damu yenye virusi ikidhani ni damu salama

Prof. Lipumba anasisitiza ofisi za CUF nchini kote ni mali ya chama cha CUF na sio mali ya mtu, hivyo amelaani kitendo cha watu kupora ofisi za CUF na kuzigeuza ni za ACT, amesema atazipigania ofisi hizo ambalo ni mali halali ya CUF, lazima zibaki CUF.
Atakuwa na ukichaa. Ofisi ambazo watu wenye majengo yao walikuwa wanajitolea kuwapa CUF, atazipigania kwa njia gani kama mwenye jengo lake akiamua kuwapa ACT?
 
Prof. Lipumba amesema CUF bado ni chama imara, na kutolea mfano Mrema alipohama na wafuasi na wanachama wake kutoka NCCR Mageuzi kwenda TLP, sasa wako wapi?, NCCR bado ipo imara, Mrema na TLP yake wana hali gani?.
 
Prof. Lipumba amesema kazi kubwa ya kwanza ya chama chake ni kuwaleta pamoja wanachama wake, kuwa kitu kimoja kujenga chama.
Pascal, huyo mtu ni sawa na mchawi aliyemtoa mwanaye kafara kwa wachawi wenzie.
Ameinyonga CUF kwa mikono yake mwenyewe !!. Na jibu lake ataona kwenye chaguzi zijazo za serikali zote mbili (mitaani & kuu)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Prof. Lipumba amekiponda ACT, ukimondoa Zitto na mwana mikakati wake Prof. Kitila Mkumbo, amesema ACT ni chama hoi bin taaban kama mgonjwa mahututi aliyepo ICU akihitaji kuongezewa damu, bahati damu yenyewe aliyoongezewa ni damu yenye virusi, badala ya kuponya mgonjwa, itamuangamiza.
 
Back
Top Bottom