Ki Mun
JF-Expert Member
- Oct 6, 2014
- 3,442
- 4,389
Akizungumza Dar es Salaam leo katika Mhadhara wa III wa Kavazi la Mwalimu Nyerere, Prof. Kitila Mkumbo ameilaumu serikali kwa tabia yake ya kuingilia na kuvuruga shughuli za Vyuo Vikuu nchini hata kufikia hatua ya kuzuia vyuo kuajiri na kupandisha vyeo watumishi wao.
Ameshangaa pia kuwa midahalo ya kisomi katika vyuo vikuu siku hizi inahitaji vibali vya polisi na mingi kama siyo yote inazuiliwa na wakuu wa vyuo wenyewe kwa kushirikiana na polisi na wakuu wengine wa vyombo vya dola...amesema hili ni janga la wazi na anashangaa kuwa Maprofesa katika vyuo vikuu wako kimya!
Mada iliyokuwa ikijadiliwa ni "Umuhimu wa Elimu ya Juu katika Maendeleo Afrika"