PreGE2025 Prof. Kitila ahakiki taarifa zake kwenye daftari la mpiga kura

PreGE2025 Prof. Kitila ahakiki taarifa zake kwenye daftari la mpiga kura

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,498
Mbunge wa Jimbo la Ubungo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji), Prof. Kitila Mkumbo, ameongoza kwa mfano kwa kuwa miongoni mwa watu wa kwanza kuhakiki taarifa zake katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura, baada ya kuanza kwa zoezi la uboreshaji wa daftari hilo Machi 17, 2025.

Prof. Mkumbo alihakiki taarifa zake katika kituo alichojiandikishia, kilichopo katika ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Ubungo, kabla ya kutembelea vituo mbalimbali katika kata zote nane za Jimbo la Ubungo, zikiwemo Ubungo, Kimara, Makuburi, Makurumla, Mabibo, Manzese, Mburahati, na Sinza.

Soma, Pia: Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura Dar es Salaam Kufanyika Machi 17-23, 2025. Wapiga Kura wapya 643,420 kuandishwa

Katika ziara yake, aliwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kuboresha taarifa zao na kuhakikisha wale waliopoteza vitambulisho vyao wanapata vipya. Pia, aliwasihi vijana waliotimiza umri wa kupiga kura kujiandikisha ili kutekeleza haki yao ya kikatiba ya kushiriki uchaguzi mkuu kwa kumchagua diwani, mbunge na rais.

Prof. Mkumbo alikumbusha kuwa uandikishaji wa wapiga kura katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura unafanyika kuanzia Machi 17 hadi Machi 23, 2025, na kuwataka wananchi wa Jimbo la Ubungo na Watanzania kwa ujumla kutumia fursa hiyo kwa manufaa ya taifa.

 
Back
Top Bottom