Prof Kapuya ajisalimisha kwa Zitto

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,385
Katika hatua nyingine, Mbunge wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM), juzi alijisalimisha katika ofisi ya CHADEMA akimuomba Zitto azungumzie matatizo ya barabara katika jimbo lake ili aweze kusaidiwa.

Kapuya alitoa ombi hilo katika ofisi za CHADEMA wilaya baada ya Zitto kuwasili eneo hilo saa 9.30 mchana kwa ajili ya kufanya mkutano wa hadhara, ikiwa ni kutekeleza ahadi yake aliyoitoa wakati alipohutubia mkutano wa awali kwa njia ya simu wiki tatu zilizopita.

Akiwa ofisini hapo, Prof. Kapuya alihojiwa na Zitto akitaka kujua sababu ya kuikodishia Halmashauri ya Kaliua nyumba yake huku akiwa ni mmoja wa madiwani wa wilaya hiyo wanaopaswa kuhakikisha halmashauri inakuwa na majengo yake.

"Karibu mzee katika ofisi zetu, lakini unaweza kuniambia kama uamuzi wako wa kuikodishia halmashauri nyumba yako hauingiliani na vikwazo vya kuiwezesha kupata majengo yake?" alihoji Zitto.

Katika kujitetea, Prof. Kapuya alisema sababu ya kufanya biashara hiyo na halmashauri ni kutokana na wilaya kutokuwa na majengo yake binafsi.

"Ni kweli mimi ninakodisha, lakini kiasi ninachochukua ni kidogo kuliko kile anachochukua Waziri Magufuli katika Wilaya ya Chato, kwani naye anaikodishia halmashauri ya wilaya yake jengo linalotumika kama ofisi," alisema Kapuya.

Katika hali ya kuonyesha kuwa anaomba Zitto asizungumzie upungufu uliopo katika jimbo lake, Prof. Kapuya alimuomba azungumzie matatizo ya barabara.

Zitto alisema kimaadili kiongozi anapofanya biashara sehemu anayoweza kuwa na uamuzi inasababisha hali ya kulinda maslahi ya kiongozi huyo ikiwa ni pamoja na kukwamisha mradi wa eneo husika usikamilike au kujiongezea gharama katika biashara husika.

Alimueleza Prof. Kapuya kuwa kinachosabaisha Mkoa wa Tabora usiendelee, ni pamoja na matatizo ya ubinafsi kati ya wabunge wa mkoa huo, huku akiwaambia waache tofauti zao na Mbunge wa Urambo Mashariki, Samuel Sitta katika kuwatumikia wananchi.
 
Ha hahaha aaaaaaahhaaaaa!!!!!!!

Kwamba yeye anachukua kidogo kuliko mwenzake???????
Kwa kweli kwa upeo huu hatutoki yaani viongozi wapangishe halmashauri,hawa wanaopanga budget kumbe wana interest zao???!!!!

Sijui nchi hii tutaiondoaje hapa maana uzalendo kwisha baadhi ya watu!!!!!
 
Wakati hayo yakiendelea mchumba wa katibu mkuu wa CHADEMA amekuwa kwenye mikutano mizito na vijana wake hasa wale wawili wanaokesha JF kumtetea mchumba wake na kumtukana Zitto ili kujipanga upya baada ya HEKAYA zao ku back fire. Alipotafutwa na mwandishi wetu mwenyekiti wa CHADEMA anayetajwa kama ndiye mama wa vifaranga vilivyopo juu ya chungu aliporomosha matusi ya nguoni na kutishia kukatisha uhai wa mwandishi wetu.
 
Haya ni majanga.tumemshuhudia akihaha uwanja wa kolimba sijua ana wasiwasi gani kama anajiamini.
 
Sasa ndio mtaamini kuwa ccm ni wachumia tumbo na ndo wanaokwamisha maendeleo ya taifa letu. Wakiwa mbele ya mic mjengoni utafikiri wana jaema na sisi kumbe usanii tu. Zito usikubali kumbebea msalaba wake huyo kapuya mwachie ndo shimo lake aliingie mwenyewe. Kama aliwaahidi hewa atajua.
 
Mleta mada nisaidie kidogo, Zito pale Kaliua alenda kama nani!..
Sijaelewa kidogo hapo mpake akawasemee wanachi hapo kwani Mbunge wa hapo hayupo?
 
Huyo Prof Kapuya alimuachia Zitto sh ngapi? Maana Zitto hanyamazishwi hivihivi burebure lazima akazichukue CRDB au Berlin kupitia account ya yule demu.
 
Profesa wa Uyoga...... Nilicheka sana niliposikia kuwa alipata PHD baada ya kufanya utafiti wa Zao la Uyoga...
 
Back
Top Bottom