Prof. Kabudi: Makonda kavunja sheria na faragha za watu kuwaita wanawake na watoto. Ilitakiwa kuwa siri sio alivyofanya

Mbinu za Makonda ni Kali sana na huwa zinaleta matokeo chanya kila Mara Ingawa wasomi wanaokariri sheria na wanasiasa feki humjia juu.

Huyu Makonda Anatakiwa atutengenezee wananchi kitabu kizuri cha kurejea Mara kwa Mara pale sheria zinaposhindwa kutatua matatizo ya jamii. Ebu fikiri kwa kina motto hajala.anaumwa, hana safe za shule halafu mjtu Fulani analazimisha iwe siri sasa hapo siri yanini wakati IPO wazi tayari.

Sheria za hovyohovyo zinazotumia falisafa za watu Wa magharibi zifanyiwe marekebisho.Kwa wale wanasheria kumbukeni tu kuwa kufa njaa au na ugonjwa siyo siri maana tutakwenda kuzika na laxima tujue sababu ya kifo.
 
Tatizo kwenye mitandao wanasomaga mabaya tu na kuyafanyia kazi lakin KAMWE HAWASOMI MAZUR MAANA YATAWAHARIBIA RATIBA ZAO.Tulishasema kwamba MH MKUU WA MKOA AMEKOSEA SANA kwasababu hakuzingatia taratibu ikaonekana kama tusemao hivi nasi tunakesi kwake. SIMBA AKILA NYAMA YA BINADAMU HAACHI
 
Professor Kabudi ametutukana sana watanzania. Mpaka dakika hii nilikuwa nasubiri kuona wenzangu kama wameshtuka lakini inaonekana kama jambo la kukubalika. Katika majibu yake bungeni kuhusu DNA, alisema kuwa ma baba wa kitanzania ni "Social Fathers". Hivo anamaanisha mama zetu ni malaya????. Jamani matusi aina hii hayakubaliki.
 
Mtu anayepinga juhudi za Makonda katika kushughilikia suala la watoto wa mitaani, apimwe akili
 
Mwanamke mzazi wa mtoto mpaka aende kwa Makonda kulalamika na kulia lia ujue kuwa kasurubika sana : mosi kulea mimba bila msaada wa mzazi mwenzie, pili kutunza mtoto baada ya kuzaa

Wengi wa watoto wa akina mama wale walioenda kwa Makonda wangekuwa hawapo kama si uvumilivu wa akina mama wale kukubali kubeba yale majukumu. Mimba ingetolewa mapema au mtoto angewekwa kwenye rambo na kutupwa ajifie au aliwe Na mbwa. Tumeona na kusikia sana haya matukio

Pamoja na uvumilivu mkubwa wa akina mama hao leo hii bila aibu anatokea mtu anasema Eti hilo jambo lingefanyika kwa 'faragha'. Aisee hizi haki za kiraia au sheria zingine ovyo kabisa.

Huu ni mwendelezo wa kumnyanyasa na kumkandamiza mwanamke. Mwisho wa siku mnaishia kuwa na lundo la watoto wanaolelewa katika mazingira ya ovyo, hatarishi, magumu na yasiyo na maadili

Siku zingine tusikomae na kukariri hayo mavitabu. Common sense ni muhimu sana

Sheria ingetungwa tu, ukitajwa DNA kupima ina kuhusu hata kwa nguvu. Ndo wangekoma kuchomeka kila sehemu
 
Mbunge Mlinga ametoa hoja bungeni kuwa Makonda hakuwatendea haki wabunge kwa kuwataja kuwa wametelekeza watoto. Wabunge wengine wamesema Makonda yuko sahihi na wale wote waliotelekeza watoto wakatoe matunzo. Mbunge Msukuma ametoa maoni ambayo kwa kweli yalikosa ustaarabu kabisa na siwezi kuyaweka hapa. Chanzo TBC!
Msukuma std 7 hata kama alikosa kuingia darasani angejitahidi kutumia akili za kuzaliwa ili kujisitiri!
 
Back
Top Bottom