Prof. Kabudi: Makonda kavunja sheria na faragha za watu kuwaita wanawake na watoto. Ilitakiwa kuwa siri sio alivyofanya

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868


Waziri wa Sheria, Prof Kabudi ameikosoa kampeni ya RC wa Dar, Paul Makonda ya kuwasaidia wanawake waliotelekezwa asema ilitakiwa kuwa ya faragha

Aidha kwa upande mwingine Mbunge wa Viti Maluum (Chadema), Sabrina Sungura amemtaka Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi atakapojibu hoja za wabunge waliochangia mjadala wa bajeti ya wizara hiyo mwaka 2018/19, kueleza sababu za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuvunja sheria mbalimbali za nchi.

Akizungumza katika mjadala huo leo Aprili 18 bungeni, Sabrina amesema moja ya sera zinazovunjwa na mkuu huyo wa mkoa ni pamoja na kuvunja mabaraza ya ardhi ya kata yaliyopo kisheria.

“Huyu mkuu wa mkoa, hivi sasa amesababisha hata hayo mabaraza hayafanyi kazi, ni kwanini anavunja sheria namna hii?” Amehoji Sungura.
 
Waziri wa Sheria, Prof Kabudi ameikosoa kampeni ya RC wa Dar, Paul Makonda ya kuwasaidia wanawake waliotelekezwa asema ilitakiwa kuwa ya faragha [HASHTAG]#MwananchiUpdates[/HASHTAG]
Huyu anaanza kugusa pasipogusika!
xmaguful-makonda45-1-640x375.jpg.pagespeed.ic.PEUCQM_Z24.jpg

Sky Eclat
 
Waziri wa Sheria, Prof Kabudi ameikosoa kampeni ya RC wa Dar, Paul Makonda ya kuwasaidia wanawake waliotelekezwa asema ilitakiwa kuwa ya faragha [HASHTAG]#MwananchiUpdates[/HASHTAG]
Inakuaje kila anapoanzisha jambo tata anaachwa tu mpaka hilo jambo lianze kushindikana approach yake ndiyo aonekane amevunja sheria? je,ikiwa amemchafua mtu atamsafishaje? Sheria zipo zinavunjwa kwa faida gani?
 
Mbunge Mlinga ametoa hoja bungeni kuwa Makonda hakuwatendea haki wabunge kwa kuwataja kuwa wametelekeza watoto. Wabunge wengine wamesema Makonda yuko sahihi na wale wote waliotelekeza watoto wakatoe matunzo. Mbunge Msukuma ametoa maoni ambayo kwa kweli yalikosa ustaarabu kabisa na siwezi kuyaweka hapa. Chanzo TBC!
 
Back
Top Bottom