Prof. Kabudi, Maamuzi uliyochukua ni Makosa ya Jinai (Sio Kosa Moja)

Mnakuza mambo out of proportions, hiyo watu wachache / wahuni aliisema by the way. Lakini pia , wao si ndio walitoa hiyo pesa? Sasa kuanza kutuhoji tulipewajr huo ni uhuni tu, hababaishwi mtu!
Na wao hawakumhoji yeye bali walikuwa wanawahoji ujumbe wa EU ulioko huku bongo. Sikilza vizuri clip. Hata hivyo nashangaa leo Mtendaji wa serikali anahamaki na mambo ya mitandaoni. Nafikiri balozi alijibu vizuri kwani suala lenyewe bado liko kwenye mijadala na sidhani kama kuna official complains kutoka EU kwenda serikali yetu. Hapo ndipo Waziri amepotoka kuhamaki wakati hakuna formal complains.
 
Naona Lobbying ya Amsterdam inaendelea kwenye corridors za Int agencies na watetezi wakutosha.

No 42. STRIKE THE SHEPHERED AND THE SHEEP WILL SCATTER.
 
Habari WanaJF,

Kwa masikitiko makubwa naandika makala hii kumkumbusha "MSOMI" Prof. Palamagamba Kabudi (Waziri Wa Mambo Ya Nje) madhara ya kauli yake ya kichochezi. Nina amini kwa elimu aliokua nayo anatambua na kuelewa nitakacho andika.

Kwa mamlaka uliopewa kisheria, kama Waziri Wa Mambo Ya Nje Tanzania, ni wajibu wako kujibu hoja/malalamiko/tuhuma dhidi ya Tanzania kwa mataifa ya nje, ila majibu hayo yawe kwa weredi/utashi/buasara na misingi ya kimahusiano mazuri dhidi ya hao watoa hizo hoja kwa mstakbali wa taifa.

Ni wazi kuwaita baadhi ya wabunge wa bunge la Europen Union "WAHUNI WACHACHE (HOOLIGANS)", na kukumbushia "TANZANIA HAIJAWAHI KUSHINDWA VITA", na "TANZANIA HAIJAWAHI KUPIGISHWA MAGOTI" ni kuwatisha/kuwakemea/kutangaza ishara ya uadui dhidi yao.

NB: Ukizingatia hoja walizotoa za kuhoji "VIGEZO VILIVYOTUMIKA KUISAIDIA TANZANIA € MILLIONI 27 ZA KUPAMBANA NA COVID-19, WAKATI RAIS ALITAMKA HATUNA MAAMBUKIZI YA COVID NCHINI" zina mashiko na hukupaswa kuzijibu.

KWANINI HUKUPASWA KUJIBU HOJA HIZO???

Wabunge wa EU walimuuliza "MWENYEKITI WA BUNGE LAO", hawakuiuliza Tanzania wala Wewe kama Waziri Wa Mambo Ya Nje. Mwenyekiti wao ndio alipaswa na anapaswa kujibu hizo hoja.

Wewe ulipaswa kukaa kimya mpaka yule alioulizwa angejibu, na majibu yake yangekua na "UKAKASI" ndio ungeweza kumrekebisha (Sio kumjibu).

Juu ya yote wabunge wale walichokosea ni kipi (hawakutumia neno lolote kali/baya/tusi/kejeli dhidi ya tanzania) mpaka Waziri Kabudi akawatolea maneno ya dharau na dhihaka kiasi kile.

Kisa kumuuliza Mwenyekiti wa kwao "KIGEZO GANI" kimetumika kuipa tanzania msaada ya € Million 27 za kupambana na maradhi ya Covid-19??? Na hizo pesa zimetumika vipi???

■ Je ingekua, Kama EU walitoa huo msaada wa hela na hazikufika tanzania zikapigwa juu kwa juu. Bado ni kosa kwao kuuliza ili kujiridhisha???



LAW 1: Never outshine the master (Kamwe Usimuangaze Bwana).

LAW 5: So much depend on your reputation - Guard it with your life (Mengi yanategemea na heshima yako - ilinde kwa maisha yako).

LAW 12: Use selective honesty and generosity to disarm your victim (Tumia uaminifu wa kuchagua na ukarimu kumtolea silaha mhasira wako).

LAW 18: Do not build fortresses to protect yourself - Isolation is dangerous (Usijenge makasri kwaajili ya kujilinda -Kujitenga ni hatari).

LAW 19: Know who your dealing with - Do not offend the wrong person (Tambua unaekabiliana nae - usimchokoze mtu mbaya).

LAW 22: Use surrender tactic (Tumia mbinu ya kujisalimisha).

LAW 46: Never appear too perfect (Kamwe usijioneshe ni mkamilifu).



■ Nani atakae lia machozi, taifa letu likifa? EU??? Kenya??? Congo??? USA??? CHINA???

Umefanya hayo kwa hasira pengine kwasababu kuu;

"""""● Wewe kama waziri wa mambo ya nje, kwa mamlaka yako kisheria, ndio ulioomba huo msaada (Barua ya maombi ya msaada itawekwa hadharani na bunge hilo soon, na watanzania wataelewa kwanini umeongea ulicho ongea) wa hizo hela kupambana na Covid-19. Wakati ukijua Rais ameshawatangazia wananchi na dunia kwamba tanzania hatuna hayo maambukizi. Tangazo la Rais ni amri kisheria. Hivyo umekwenda kinyume na amri ya aliekuteua. Na pengine ulitumia uongo kuwashawishi EU watupe zile pesa za msaada. Na umemfanya aonekane muongo mbele ya EU.●"""""

Na kauli/muongozo anayotoa Rais kwa watendaji wa serikali (wote mpaka mawaziri) ni wajibu wa kisheria kuutii, sasa pengine ndicho kilichokufanya kuanza kutupandikizia chuki na hasira dhidi ya wanaotupa misaada, tuwachukie na kuwabeza kwa kutukumbusha pindi Mwalimu Nyerere alipowafukuza waingereza na wajerumani na kuwarudishia hela zao za misaada.

Dunia imebadilika, hatupo miaka hio. Hizo hela € MILLION 27 hata wakirudishiwa kesho, hii kashfa ya kuziomba wakati rais alishatangazia dunia kwamba hatuna maambukizi ya covod, haikwepeki. Na pili kashfa ya kukimbilia kuwajibu wakati hawajakuuliza wewe (Wamemuuliza mtu wao) haikwepeki.

■ Umejigamba kwamba Tanzania haijawahi kushindwa vita na haijawahi kupigishwa magoti. Inasikitisha kuona wewe ndio "UNAKUJA KUWA CHANZO" cha kuiharibu hio historia ya tanzania.

** Sheria Ya Makosa Ya Jinai (The Penal Code CAP 16) **

Kauli zako hizo ni wazi zitazaa uadui na mataifa ya nje na matumizi mabaya ya ofisi yako.

Chapter 10 - Section 69: Kosa La Matumizi Mabaya Ya Ofisi (Hatia ni Kifungo Cha Miaka 3).
Chapter 13 - Section 123: Kosa La Kutofuata Wajibu Wa Kisheria - Kauli/Muongozo wa Rais ni sheria kwa watendaji wake, kauli ya rais ya kusema tanzania hakuna covid ni wajibu kwa wafanyakazi wa serikali kutii kama sheria (Hatia ni Kifungo Cha Miaka 2).
Chapter 13 - Section 124: Kosa La Kutofuata Amri Kisheria (Hatia ni Kifungo Cha Miaka 2).

Alexander The Great
JamiiForums
kalamaganda kadudi mtamuelewa tu, ukiona yale macho yanataka kutoka ujue anaongopea anacho ongea.

Ni sawa na yule waziri wa Saddam kipindi cha vita ya Marekani na Iraq, wasomi wana vipaji vya kuongopea
 
Mnakuza mambo out of proportions, hiyo watu wachache / wahuni aliisema by the way. Lakini pia , wao si ndio walitoa hiyo pesa? Sasa kuanza kutuhoji tulipewajr huo ni uhuni tu, hababaishwi mtu!
Wabunge wa EU walimuuliza "MWENYEKITI WA BUNGE LAO", hawakuiuliza Tanzania wala Wewe kama Waziri Wa Mambo Ya Nje. Mwenyekiti wao ndio alipaswa na anapaswa kujibu hizo hoja.
Nmequote tu.
 
Kuwaita watoa msaada wahuni alikosea sana sijui hizi tabia za namna hii tunazitoa wapi kwa kweli...kumsikiliza jamaa inatakiwa uwe na moyo sana anadharirisha watu na Elimu zao...
 
Na wao hawakumhoji yeye bali walikuwa wanawahoji ujumbe wa EU ulioko huku bongo. Sikilza vizuri clip. Hata hivyo nashangaa leo Mtendaji wa serikali anahamaki na mambo ya mitandaoni. Nafikiri balozi alijibu vizuri kwani suala lenyewe bado liko kwenye mijadala na sidhani kama kuna official complains kutoka EU kwenda serikali yetu. Hapo ndipo Waziri amepotoka kuhamaki wakati hakuna formal complains.
Regardless, hiyo ina raise maswali mengi sana kwamba kuna kitu nyuma ya pazia, kwamba inawezekanaje mtu aliyekwambia hana malaria na bado ukampa pesa ya kununua dawa, na bado wanaukizana wenyewe kwa wenyewe kwamba walitupaje huo msaada, hizo ni dalili za uhuni tu, na kama ulisikiloza hiyo clip, aliuoiza kama kuna haja ya kuendelea kutoa budgetary support kwa Tanzania, means wanataka kutuSanction, nadhani tuna haki ya kuwajibu hata kama walizungumza wao kwa wao
 
Wabunge wa EU walimuuliza "MWENYEKITI WA BUNGE LAO", hawakuiuliza Tanzania wala Wewe kama Waziri Wa Mambo Ya Nje. Mwenyekiti wao ndio alipaswa na anapaswa kujibu hizo hoja.
Nmequote tu.
Hao bunge walihoji kama kuna haja ya kuendelea kutoa budgetary support kwa Tanzania, hiyo inatranslate kwamba wanataka kutusanction, sasa kwanini tusiwajibu?
 
Tanzania kwa hii miaka 10 ipo kwenye mapito mazito !! Maombi kwa Mungu wetu yanahitajika sana, la Taifa linakwenda kuparaganyika na sifa yake yote inakwenda kupotea kwa muda mfupi tu.
 
Back
Top Bottom