Prof. Kabudi, Maamuzi uliyochukua ni Makosa ya Jinai (Sio Kosa Moja)

Wana lumumba watakataa hilo, hata iwekwe wazi barua ya alieomba huo msaada tena kwa kutumia uongo/ulaghai, bado watakataa.
Yaani hawa jamaa ni shida tupu ni wazuri sana kwenye kupindisha mambo, Ukimwangalia Kabudi usoni jinsi alivyo mkavu utajua anachosema ni kweli kumbe ni uzushi mtupu.Kwa kweli hawa jamaa hawafai,wanakomaa kusema mbuzi ni kondoo na kondoo ni mbuzi
 
Lazima ushangae kwa sababu kichwani huna kitu
Mi nilishangaa sana kwa kabudi kurudishwa kwenye ile wizara, sikutegemea angerudi kwenye baraza la mawaziri na kama angerudi nilihisi atapewa wizara kama ya kilimo hivi ndo inaweza mfaa
 
Ni wazi kuwaita baadhi ya wabunge wa bunge la Europen Union "WAHUNI WACHACHE (HOOLIGANS)", na kukumbushia "TANZANIA HAIJAWAHI KUSHINDWA VITA", na "TANZANIA HAIJAWAHI KUPIGISHWA MAGOTI" ni kuwatisha/kuwakemea/kutangaza ishara ya uadui dhidi yao.

Mbona wao wanatutishia/wanatukemea/kutangaza dunia nzima wametupa msaada, huu si ndio unaitwa umbea/unafiki wa kimalaya.


NB: Ukizingatia hoja walizotoa za kuhoji "VIGEZO VILIVYOTUMIKA KUISAIDIA TANZANIA € MILLIONI 27 ZA KUPAMBANA NA COVID-19, WAKATI RAIS ALITAMKA HATUNA MAAMBUKIZI YA COVID NCHINI" zina mashiko na hukupaswa kuzijibu.

Huo ni upumbavu wao na kujipendekeza kwetu, sisi tuliwaambia hatuna Corona lakini bado wakaona inafaa sisi kupewa hizo fedha. WATAJIJU.
 
POLENI.

Hata hivyo, waliosema ni EU. Waliojibiwa ni EU. Kinawauma nini? Kwendeni zenu...
 
Prof alifanya alichoagizwa, na kama alienda mbali zaidi ilikuwa ni kwa ajili ya kumfurahisha mteuzi. weledi, hekima na busara havileti madaraka kwa awamu hii.
Awamu hii madaraka utayapata kwa "KAZI TU". Hekima na Busara vitani mpelekee mkeo.
 
Jibu hiyo hoja acha kuharisha upuuzi. Walitupa wenyewe huo msaada, tuliwalazimisha? Sasa wanatuuliza sisi eti tulipewaje?! Uhuni tu huo!
Kwani waliingiza tu kwenye account ya benki ya hazina bila sisi kusaini document yeyote?
 
View attachment 1632788
Sijui tutaweza bila misaada
Alafu sijui pesa zetu zaenda wapi na pita tu......
Kupewa na kopokea msaada sio dhambi. Msaada kwa kuheshimiana haina shida. Tatizo ni hao MASHOGA wenye tabia za kike. Hao MASHOGA wenye tabia za KUKU JIKE akitagaa anapiga kelele mtaa mzima mpaka ujue ametaga. Hao wazungu wenye tabia za KUKU JIKE tutaenda nao kibabe ivo ivo. Akipiga kelele tunakamata, chinja kula supu na mayai tunakaanga.
 
Habari WanaJF,

Kwa masikitiko makubwa naandika makala hii kumkumbusha "MSOMI" Prof. Palamagamba Kabudi (Waziri Wa Mambo Ya Nje) madhara ya kauli yake ya kichochezi. Nina amini kwa elimu aliokua nayo anatambua na kuelewa nitakacho andika.

Kwa mamlaka uliopewa kisheria, kama Waziri Wa Mambo Ya Nje Tanzania, ni wajibu wako kujibu hoja/malalamiko/tuhuma dhidi ya Tanzania kwa mataifa ya nje, ila majibu hayo yawe kwa weredi/utashi/buasara na misingi ya kimahusiano mazuri dhidi ya hao watoa hizo hoja kwa mstakbali wa taifa.

Ni wazi kuwaita baadhi ya wabunge wa bunge la Europen Union "WAHUNI WACHACHE (HOOLIGANS)", na kukumbushia "TANZANIA HAIJAWAHI KUSHINDWA VITA", na "TANZANIA HAIJAWAHI KUPIGISHWA MAGOTI" ni kuwatisha/kuwakemea/kutangaza ishara ya uadui dhidi yao.

NB: Ukizingatia hoja walizotoa za kuhoji "VIGEZO VILIVYOTUMIKA KUISAIDIA TANZANIA € MILLIONI 27 ZA KUPAMBANA NA COVID-19, WAKATI RAIS ALITAMKA HATUNA MAAMBUKIZI YA COVID NCHINI" zina mashiko na hukupaswa kuzijibu.

KWANINI HUKUPASWA KUJIBU HOJA HIZO???

Wabunge wa EU walimuuliza "MWENYEKITI WA BUNGE LAO", hawakuiuliza Tanzania wala Wewe kama Waziri Wa Mambo Ya Nje. Mwenyekiti wao ndio alipaswa na anapaswa kujibu hizo hoja.

Wewe ulipaswa kukaa kimya mpaka yule alioulizwa angejibu, na majibu yake yangekua na "UKAKASI" ndio ungeweza kumrekebisha (Sio kumjibu).

Juu ya yote wabunge wale walichokosea ni kipi (hawakutumia neno lolote kali/baya/tusi/kejeli dhidi ya tanzania) mpaka Waziri Kabudi akawatolea maneno ya dharau na dhihaka kiasi kile.

Kisa kumuuliza Mwenyekiti wa kwao "KIGEZO GANI" kimetumika kuipa tanzania msaada ya € Million 27 za kupambana na maradhi ya Covid-19??? Na hizo pesa zimetumika vipi???

■ Je ingekua, Kama EU walitoa huo msaada wa hela na hazikufika tanzania zikapigwa juu kwa juu. Bado ni kosa kwao kuuliza ili kujiridhisha???



LAW 1: Never outshine the master (Kamwe Usimuangaze Bwana).

LAW 5: So much depend on your reputation - Guard it with your life (Mengi yanategemea na heshima yako - ilinde kwa maisha yako).

LAW 12: Use selective honesty and generosity to disarm your victim (Tumia uaminifu wa kuchagua na ukarimu kumtolea silaha mhasira wako).

LAW 18: Do not build fortresses to protect yourself - Isolation is dangerous (Usijenge makasri kwaajili ya kujilinda -Kujitenga ni hatari).

LAW 19: Know who your dealing with - Do not offend the wrong person (Tambua unaekabiliana nae - usimchokoze mtu mbaya).

LAW 22: Use surrender tactic (Tumia mbinu ya kujisalimisha).

LAW 46: Never appear too perfect (Kamwe usijioneshe ni mkamilifu).



■ Nani atakae lia machozi, taifa letu likifa? EU??? Kenya??? Congo??? USA??? CHINA???

Umefanya hayo kwa hasira pengine kwasababu kuu;

"""""● Wewe kama waziri wa mambo ya nje, kwa mamlaka yako kisheria, ndio ulioomba huo msaada (Barua ya maombi ya msaada itawekwa hadharani na bunge hilo soon, na watanzania wataelewa kwanini umeongea ulicho ongea) wa hizo hela kupambana na Covid-19. Wakati ukijua Rais ameshawatangazia wananchi na dunia kwamba tanzania hatuna hayo maambukizi. Tangazo la Rais ni amri kisheria. Hivyo umekwenda kinyume na amri ya aliekuteua. Na pengine ulitumia uongo kuwashawishi EU watupe zile pesa za msaada. Na umemfanya aonekane muongo mbele ya EU.●"""""

Na kauli/muongozo anayotoa Rais kwa watendaji wa serikali (wote mpaka mawaziri) ni wajibu wa kisheria kuutii, sasa pengine ndicho kilichokufanya kuanza kutupandikizia chuki na hasira dhidi ya wanaotupa misaada, tuwachukie na kuwabeza kwa kutukumbusha pindi Mwalimu Nyerere alipowafukuza waingereza na wajerumani na kuwarudishia hela zao za misaada.

Dunia imebadilika, hatupo miaka hio. Hizo hela € MILLION 27 hata wakirudishiwa kesho, hii kashfa ya kuziomba wakati rais alishatangazia dunia kwamba hatuna maambukizi ya covod, haikwepeki. Na pili kashfa ya kukimbilia kuwajibu wakati hawajakuuliza wewe (Wamemuuliza mtu wao) haikwepeki.

■ Umejigamba kwamba Tanzania haijawahi kushindwa vita na haijawahi kupigishwa magoti. Inasikitisha kuona wewe ndio "UNAKUJA KUWA CHANZO" cha kuiharibu hio historia ya tanzania.

** Sheria Ya Makosa Ya Jinai (The Penal Code CAP 16) **

Kauli zako hizo ni wazi zitazaa uadui na mataifa ya nje na matumizi mabaya ya ofisi yako.

Chapter 10 - Section 69: Kosa La Matumizi Mabaya Ya Ofisi (Hatia ni Kifungo Cha Miaka 3).
Chapter 13 - Section 123: Kosa La Kutofuata Wajibu Wa Kisheria - Kauli/Muongozo wa Rais ni sheria kwa watendaji wake, kauli ya rais ya kusema tanzania hakuna covid ni wajibu kwa wafanyakazi wa serikali kutii kama sheria (Hatia ni Kifungo Cha Miaka 2).
Chapter 13 - Section 124: Kosa La Kutofuata Amri Kisheria (Hatia ni Kifungo Cha Miaka 2).

Alexander The Great
JamiiForums
punguza ujuaji dogo..kuongoza nchi sio kama kumsoma robert greene
 
Do not offend the wrong person = usimchokoze mtu mbaya

Mmh hapa umechapia mkuu
 
Back
Top Bottom