VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Ukweli utaniweka huru. Nasema kweli na sisiti kusema kweli daima. Pamoja na kuwemo kwa miongo kadhaa ndani ya CCM, sijawahi kuunga mkono jambo lisilo na maan au kumuunga mkono mtu ambaye hafanyi katika matakwa ya kinchi. Sijawahi kuwa rafiki mnafiki. Ndiyo maana nimekuwa nikisema kwa kukosoa wapinzani na hata watawala-wa chama changu.
Katika uteuzi na utendaji wa Serikali ya awamu ya tano, Waziri wa Elimu, Prof. Joyce Ndalichako, ninamuunga mkono kwa asilimia mia moja. Namuunga mkono kwakuwa anashughulikia moyo wa Taifa. Moyo wa Taifa lolote ni Elimu. Elimu yetu kama nchi imeporomoka na kusawajika vya kutosha na kutisha. Yameondolewa mambo na kuingizwa mengine kiholela sana.
Prof. Ndalichako ndiye mwarobaini wa tatizo letu la elimu Tanzania. Prof. Ndalichako ana weledi, usomi na uzoevu wa kutosha kushughulika na elimu yetu ili kuirejesha ilipoondolewa. Kuwa na elimu bora. Ni muda wa Prof. Ndalichako kurejesha ufaulu wa haki na si wa idadi;ufaulu wa ubora na si wa kubebwabebwa. Elimu haina haja ya kuwa na BRN. Elimu ni mboni inayohitaji ulinzi wa kueleweka.
Madaraja ya zamani yarudi. Alama za zamani zirudi. Nidhamu shuleni irudi. Heshima kwa walimu irudi. Maslahi kwa walimu yarudi au kuboreshwa. Watanzania wanapaswa kujivunia elimu yao na kuilinda kwelikweli. Elimu yetu sasa imepoteza mvuto. Tunapaswa kujirudi kama Taifa. Prof. Ndalichako, nakuamini kama Nahodha imara. Najua, ulipokuwa mwaka wa kwanza UDSM, Rais Magufuli alikuwa mwaka wa tatu pale pale UDSM. Amekuamini mdogo wake.Usimuangushe Rais.
Prof. Ndalichako, elimu ni 'pyramidal in shape'. Tunapaswa kupata wachache elimu ya juu lakini walio bora. I love, support and appreciate you Prof. Joyce Ndalichako!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam