Prof. Joseph Mbele atoa andiko kupinga kauli ya Dr. Mwakyembe

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Messages
1,382
Points
1,500

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined Feb 24, 2012
1,382 1,500
Profesa Mtanzania ambae kwa sasa yuko Marekani, Profesa Joseph Mbele, ameandika kwenye Facebook page yake (Joseph Mbele bila neno Prof) kuwa anapingana na Mwakyembe, na amesema hata yeye ana degree nne na mtu yeyote asiye na degree nne kama yeye ana nafasi ya kumkosoa.

Ameandika:

"NAPINGA KAULI YA WAZIRI MWAKYEMBE KUHUSU ELIMU"

Nimemsikia Waziri Mwakyembe akijitapa kwamba ana digirii nne na kwamba wasio na kisomo kama yeye hawana la kumwambia. Mimi pia nina digirii nne, tena nilikwaa tuzo za mwanafunzi bora katika chuo kikuu cha Dar es Salaam na chuo kikuu cha Wisconsin-Madison, hapa Marekani.

Siafiki kauli ya Waziri Mwakyembe. Ninaona ni kauli mbaya sana. Ninaleta hapa makala yangu mojawapo iliyomo katika kitabu changu kiitwacho “Changamoto: Insha za Jamii.”

1574237539333.png

Katika andiko hilo, Profesa Mbele ameweka moja kati ya andiko lako kuweka sawa mawazo yake kuhusu elimu ya mtu bila kuwa na madegeree mengi au kupitia vyuoni. Makala aliita ELIMU KIJIJINI, ambayo ipo kwenye blog yake, nami nawaletea hapa mawazo ya profesa Jospeh Mbele kama alivyoandika.

Mara kwa mara nakumbuka elimu niliyopata kijijini, kabla ya kuanza shule. Wengi wetu tulipitia njia hiyo. Ni elimu gani hiyo? Tangu utotoni, tulipata maelekezo kutoka kwa wazazi kuhusu mambo mbali mbali, kufuatana na umri, kuanzia namna ya kuvaa hadi namna ya kula kwa adabu na kuwasalimia watu.

Baadaye wavulana tulijifunza kuchunga mbuzi na ng’ombe, na kutandika nyasi kwenye zizi la ng’ommbe, na kukamua maziwa. Wasichana walifundishwa kazi za jikoni na kulea watoto.

Kama ilivyo kwa watoto wengine, baba na mama walikuwa wananituma kufanya shughuli hii au ile. Hata majirani walikuwa wanatutuma sisi watoto kuwasaidia shughuli mbali mbali. Yote hii ilikuwa ni sehemu ya elimu yetu.

Nilipokua kidogo nilianza kushiriki katika kilimo. Nilijifunza kulima, kupanda, kupalilia, na kuvuna mazao. Nilijifunza kuchuma kahawa na kuishughulikia baada ya hapo. Shughuli hizi ziliniwezesha kufahamu zaidi habari za udongo, nyasi, na magugu. Niliwafahamu wadudu wanaoishi mashambani, kama ni wadudu salama kwa mimea au ni adui wa mimea. Nilizijua tabia za wadudu mbali mbali, kuanzia siafu hadi sisimizi na mchwa. Nilijua kama wanauma au hawaumi. Tulijifunza namna ya kuwanasa kumbikumbi, ambao walikuwa ni chakula.

Katika kuchunga mbuzi na ng’ombe tulipata fursa ya kujifunza mambo mengi, sio tu kuhusu tabia za hao wanyama, bali pia elimu ya mimea na nyasi, zikiwemo nyasi ambazo ni chakula cha mbuzi au ngombe na kadhalika. Huko porini tulijifunza pia aina mbali mbali za mboga za porini, matunda, uyoga, na kadhalika. Tuliweza kutofautisha uyoga ambao unalika na binadamu na ule ambao ni sumu.

Katika kukua kwetu kijijini, tulisikiliza hadithi na nyimbo, tukaweza kusimulia hadithi hizi na kuimba nyimbo. Hadithi hizi zilisheheni falsafa, maarifa, na maadili. Tulishiriki katika ngoma, tukaweza kupiga ngoma na ala zingine za muziki, kucheza na kuimba. Mbali ya kwamba hii ilikuwa ni burudani, ilikuwa pia elimu ya sanaa. Ilikuwa ni elimu kuhusu namna ya kushirikiana na wengine, kwani ngoma inahitaji nidhamu na ushirikiano.

Kwa kuwa nilisoma shule ya msingi nikiwa bado naishi kijijijini, niliendelea kuipata elimu ya kijijini hata baada ya kuanza shule. Baada ya masomo shuleni, niliporudi nyumbani, niliendelea na shughuli ya kuchunga mbuzi na ng’ombe, na kusaidia shughuli mbali mbali za nyumbani ambazo ziliendelea kuimarisha elimu yangu ya kijijini.

Baada ya kumaliza darasa la nne, mambo yalibadilika sana. Nilikwenda shule ya bweni, mbali kabisa na nyumbani kwangu. Elimu niliyoipata kule ilikuwa ya vitabuni zaidi. Ingawa tulifanya pia shughuli za nje, kama vile shambani na bustanini, muda mwingi zaidi tulitumia katika kujifunza yaliyomo vitabuni. Elimu ya vitabuni ilishamiri kichwani mwangu nilivyozidi kuendelea na madarasa, hadi chuo kikuu Dar es Salaam, na hatimaye Marekani.

Kadiri nilivyoendelea na elimu ya shuleni, nilizidi kusahau elimu ya kijijini. Kusoma sana kuliendana na kufifia kwa elimu niliyoipata kijijini. Leo hii, sikumbuki majina ya mimea mingi, wala ya aina nyingi za majani niliyojifunza kijijini. Nimesahau majina na tabia za wadudu, wanyama, na ndege mbali mbali. Sina tena ufahamu mzuri wa miti na majani ambayo ni dawa, miti ambayo ni bora kwa kuni na ile ambayo si bora, kwa vile labda haishiki moto haraka au inatoa moshi mwingi. Hii ni hasara kubwa.

Elimu ya kijijini ni elimu thabiti. Ni elimu ambayo imekusanya ujuzi na maarifa kutoka enzi za zamani. Vizazi kwa vizazi vimechuja na kuhifadhi yale yaliyo muhimu tu. Kila kinachofundishwa kina maana katika maisha. Ndio elimu ya kijijini.

Hapakuwa na vitabu wala maktaba. Kila kitu kilihifadhiwa akilini na kurithishwa kutoka kizazi hadi kizazi kwa maneno ya mdomo na kwa vitendo. Elimu ya kijijini haikuwa inakaa maktabani, bali watu walitembea nayo vichwani. Kutokana na ulazima wa kuhifadhi kila kitu katika akili ya binadamu, hapakuwa na nafasi kubwa ya kuhifadhi lolote ambalo halikuwa na maana au umuhimu. Hii ni tofauti na leo, ambapo tunatumia zaidi vitabu. Tunao uwezo wa kuhifadhi vitabu kiasi chochote, hata kama havina maana.

Hakuna ubishi kuwa vitabu vingi ni muhimu, kwani vinabeba elimu ya aina aina. Lakini, kuna pia vitabu ambavyo havina uhusiano na maisha ya wale wanaosoma. Katika shule, kuanzia enzi za ukoloni hadi leo, tunawafundisha vijana mambo mengine ambayo hayana mantiki wala umuhimu katika hali na mahitaji ya jamii zetu. Wakoloni walianzisha mtindo wa kufundisha mambo ya kwao bila kuzingatia umuhimu au uhalali wake katika mazingira ya kwetu. Walizipotosha akili za vijana, na kwa bahati mbaya upotoshaji wa aina mbali mbali bado unaendelea, kama walivyoelezea watalaam kama Franz Fanon na Mwalimu Nyerere. Hii ni tofauti na elimu ya kijijini, ambayo ilienda sambamba na maisha na mahitaji ya wahusika.

Kwa vile elimu ya shuleni inadhihirishwa kwa vyeti, wako ambao wanatafuta njia za mkato, zisizo halali, kupata hivyo vyeti. Wengine wanaiba mitihani. Huu ni udhaifu wa mfumo wa elimu ya shule. Elimu ya kijijini haikuwa na mwanya wa namna hiyo. Hapakuwa na njia za mkato. Hapakuwa na mitihani ya kuiba. Kama ilikuwa ni kwenda kwenye unyago na jando, kila mhusika alitimiza yaliyohitajika.

Tujiulize swali moja: Je, kuna sababu yoyote ya kuendelea kuisahau au kuififisha elimu ya kijijini kwa vile tu mtu anaendelea na elimu ya shuleni? Je, haingekuwa bora kuiingiza elimu ya kijijini mashuleni ili kuhifadhi na kudumisha hazina hii ya urithi wetu?
 

3 Angels message

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2017
Messages
2,222
Points
2,000

3 Angels message

JF-Expert Member
Joined Aug 3, 2017
2,222 2,000
Kwa hiyo Dr Mwakyembe akiwa na wazazi/walezi wake au hata kanisani kwake anakoabudu yeye ndiyo huwa mzungumzaji tu au huko kote huwa anakutana na wenye degree 4+?

Hizo majigambo wanayaweza wahaya tu yeye awe mpole tu, maana kipindi kile cha ugonjwa hao anaowadharau ndiyo waliomuombea sana apone leo analeta dharau
 

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Messages
1,382
Points
1,500

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined Feb 24, 2012
1,382 1,500
Huyo Prof nilipoona kavaa kofia imeandikwa "Make Africa great again"Nimekata tamaa hata kusoma bandiko lake. Ingawa hata mimi nampinga Mwakyembe.
Can he tell us when Africa was great?Bora hata angesema make Africa great.
Prejudice
 

Yamakagashi

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2016
Messages
8,718
Points
2,000

Yamakagashi

JF-Expert Member
Joined Sep 19, 2016
8,718 2,000
Historia ya Africa kweli sio wengi wanailewa, Africa kabla ya colonialism umeisoma? Ya Timbuktu nk?
Unashangaa nini Prof mbele anaposema Make Africa Great Again?
Huyo Prof nilipoona kavaa kofia imeandikwa "Make Africa great again"Nimekata tamaa hata kusoma bandiko lake. Ingawa hata mimi nampinga Mwakyembe.
Can he tell us when Africa was great?Bora hata angesema make Africa great.
 

Victoire

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2008
Messages
15,790
Points
2,000

Victoire

JF-Expert Member
Joined Jul 4, 2008
15,790 2,000
Historia ya Africa kweli sio wengi wanailewa, Africa kabla ya colonialism umeisoma? Ya Timbuktu nk?
Unashangaa nini Prof mbele anaposema Make Africa Great Again?
If it was great kweli ingekuwa colonised ? she was weak, that is why Africa was easily invaded.
 

Swet-R

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2018
Messages
2,764
Points
2,000

Swet-R

JF-Expert Member
Joined Aug 25, 2018
2,764 2,000
Kiukweli huyo mbele hana tofauti na mwakyembe. Huwa napata shida sana kuwaelewa hawa wanajiita wasomi waliolowea huko nje. Sasa msaada wake kwa nchi yake ni upi?. Si lazima uajiriwe,kama wewe ni prof,basi kichwa chako kicheze kila namna,unaweza ukawa mfugaji wa mfano,au mkulima wa zao fulani wa mfano,au ukaanzisha jambo na ukaajiri vijana wengi. Yaani prof anazidiwa na Diamond msaniii wa darasa la saba maarifa (hata kama ni form 4). Diamond ameajiri vijana,anasadia jamii. Ona maprof wetu,ona kilichoandikwa kwenye kofia yake,ona anavyozidi kuzeekea nchi za watu,ona alivyochoka hata kimuonekano tu. Na hiyo kofia wazungu wanabaki kutuzooom tu,huyu ni prof toka Tz. Bora asingezaliwa tu
 

Victoire

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2008
Messages
15,790
Points
2,000

Victoire

JF-Expert Member
Joined Jul 4, 2008
15,790 2,000
Swet-R,
Kumbe na wewe umeona eeeh. Prof mzima unavaa kofia imeandikwa make Africa Africa great again. Jamani. Halafu slogan hiyo si alikuja nayo Trump ? Prof mzima you cant even come with a slogan which is relative to Africa. When Africa was great so we can make her great again ?
 

Yamakagashi

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2016
Messages
8,718
Points
2,000

Yamakagashi

JF-Expert Member
Joined Sep 19, 2016
8,718 2,000
Matusi ya nini tena? Wewe umetumia sense zako kusema Africa was weak ndio maana ikawa colonised, Kwa sense zako hizo ambazo unahisi ziko sawa sana ni Africa peke yake ndio walikuwa invaded?

Weakness ndio umeona sababu?

Puta madre..


Common sense is not common. Stay blessed.
 

Forum statistics

Threads 1,381,734
Members 526,184
Posts 33,810,304
Top