- Tunachokijua
- Madai
Kumekuwepo na kipande cha video kinachomuonesha Mkurugezi wa Shirika la afya duniani (WHO) kanda ya Afrika, Prof. Mohamed Janabi akizungumzia kuwa kuna tiba ya moyo ambayo inaweza kumfanya mtu akapona kwa kutumia kikombe kimoja
Uhalisia wa madai hayo
JamiiCheck imefuatilia na kujiridhisha kuwa kipande hicho cha video kimehaririwa kwa teknolojia ya Akili Unde (AI).
Kipande hiko cha video kinachomuonesha Prof. Janabi kinaoneakana kuhaririwa kutoka kwenye moja ya mazungumzo aliyoyafanya Mkurugenzi huyo na baadae kuwekewa maneno hayo yanayosikika.
Ufuatiliaji kwa kutumia nyenzo za kubaini maudhui yaliyotengenezwa kwa Akili Unde, JamiiCheck imebaini kuwa sauti iliyottumika katika video hiyo ni ya kutengeneza kwa Akili Unde na wala si sauti halisi ya Prof. Janabi.