Prof. Issa Shivji auchambua utawala wa Rais Magufuli

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
Wakati akifanya mahojiano maalum na AzamTV, Prof. Issa Shivji amebainisha dira na mwelekeo wa serikali ya Rais Magufuli.

Ndondoo:
Prof. Shivji amebainisha kutoka kwenye hotuba ya Rais Magufuli ambayo haikuwa imeandikwa rasmi wakati akiongea na wafanyabiashara ndiyo iliyotoa mwelekeo na dira ya serikali yake. Vile vile amelipongeza gazeti la Jamhuri na kusema ni gazeti pekee ambalo liliichapisha hotuba hiyo.

Hotuba hiyo ina maudhui ya kipekee kulinganisha na utawala wa Awamu ya 2,3 na 4. Kuna mambo makuu matatu katika hotuba hiyo ambayo yanatoa mwelekeo na mtazamo wa serikali ya Rais Magufuli.

1)Kujenga uchumi wa kitaifa(Nation Economy).

2)Kudhibiti uporaji wa raslimali na mtaji wa nchi hasa raslimali zinazoporwa na kusafirishwa kwenda nchi za nje bila wananchi wote kufaidika.

3)Kutokuridhika na sekta ya fedha hasa kuhusu mabenki makubwa kufanya biashara na serikali badala ya kujikita kwa wananchi. Kwa maana nyingine, serikali inafanya biashara na mabenki haya kwa kutumia fedha zake yenyewe.

Rais Magufuli ameainisha na kusema Mabepari wa ndani watakuwa na nafasi katika serikali yake lakini kama watakuwa mapepari wazalendo/mabepari wa kitaifa (National Bourgeoisie)pamoja na kwamba malengo ya bepari ni kupata faida. Serikali ya Rais Magufuli inataka mabepari wanaotanguliza mbele maslahi ya watanzania.

Rais Magufuli anataka bepari ambaye ni mzalishaji na siyo bepari ambaye ni mchuuzi. Kwa mfano hataki pia wale wanaotumia kete ya uzawa ili wapewe vitalu vya gesi ili waingie ubia na watu wa nje. Huu ni uchuuzi. Kama uzawa wa aina hii ni hoja, hata serikali inaweza kuwa mchuuzi kwa kuingia ubia na watu wa nje.

Rais Magufuli anataka bepari ambaye anatumia malighafi ya Tanzania ili kutengeneza bidhaa kwa ajili ya mahitaji ya soko la ndani na wananchi wakanufaika pia katika ajira.

Kwa Maelezo zaidi angalia VIDEO:

 
Last edited:
Huyu Prof toka aharibu wakati wa mchakato wa katiba mpya simwelewi kabisa, bora akalee wajukuu nitamwona wa maana.
 
Kama huo ndio uchambuzi toka kwa profesa wa Tz, sijui itakuea vipi kama tutaletrwa uchambuzi ea kijana ea datasa la 7?:
 
Hivi Magufuli aitaja hayo ya udalali wa gesi yeye mwenyewe?
au watu tu wameamua kumtafisiria?
Pasco.. Nguruvi3
 
Last edited by a moderator:
Prof alikuwa kimya mda mrefu sana
Amesema aliamua kuwa kimya kuangalia kwanza mwelekeo na dira ya serikali ya Awamu ya Tano kabla hajatoa mtazamo wake.

Hata hivyo amesema siku 50 za serikali ya Rais Maguifli haziwezi kutoa mtazamo kamili wa dira yake lakini hata hivyo mwanzo umeanza kuonyesha mwelekeo na dira ya serikali yake.
 
Huyu Prof toka aharibu wakati wa mchakato wa katiba mpya simwelewi kabisa, bora akalee wajukuu nitamwona wa maana.
Tatizo ni kwamba, pamoja na kutomwelewa lakini hauachi kuzisoma habari zake!

Kwa nini usimpuuze na kuachana na habari zake?

Wewe ungeonekana wa maana kama ungeachana na habari zake au maoni yake kwa sababu kuna wengine bado wanamwelewa. Matamanio yako yasifanye wananchi wote wakakosa maoni yake.
 
Profesa Shivji anaonekana ametumia muda mwingi kuchambua hotuba za raisi JPM na hasa ile alohutubia wafanya biashara katikati ya mwezi huu.
 
Kama huo ndio uchambuzi toka kwa profesa wa Tz, sijui itakuea vipi kama tutaletrwa uchambuzi ea kijana ea datasa la 7?:
Wewe kuandika tu ni tatizo/majanga, utaweza kuelewa uchambuzi wa Prof. Shivji.

Ama kweli ujinga ni mtaji na upumbavu ni kipaji!
 
Uchambuzi constructive ndo unahitajika kwa sasa, hii ndio maana ya kuelimika na si usomi pekee. Big up Prof and JPM..
 
Ukifuatilia vzuri makala zake waweza kusema Jenerali Ulimwengu ni profesa, uchambuzi mzuri wenye ukweli. Tofauti na Pro-pesa Kitila et al,
 
Back
Top Bottom