Hakika,vitabu vyake, bila kujali miaka vilivyochapishwa,vitaendelea,kwa kipindi kirefu kijacho,kuakisi mienendo ya kisiasa barani Afrika ikiwa hatua za dhati na za makusudi hazitachukuliwa na watawaliwa dhidi ya watawala wa bara hili.Kote barani Afrika,maandishi yake yamechangia kuzalisha ''critical mass'',nyenzo mwafaka katika kuleta mapinduzi, mageuzi na mabadiliko katika nyanja za kisiasa,kiuchumi na kisiasa.
Kwa kuwa Tanzania hatukuwahi kuonyesha namna tunavyokerwa na watawala-kwa uamuzi wetu wa kuendelea kukumbatia tawala dhalimu ,kandamizi na onevu,basi mwaka 2015,miaka mitatu baada ya kifo chake,tuwaondoe wale wote ambao Achebe alipata kuwazungumzia.Kwa hakika,kama kuna nchi inatakiwa kuyapitia upya maandishi yake kwa sasa,basi,jamii hiyo inapatikana katika pande la ardhi liitwalo Tanzania.