G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,596
- 36,018
Jana rais Magufuli alitua Bank of Tanzania (BoT) akiwa na iliyojulikana kama list ya wafanyakazi wote wa pale wakiwemo wafanyakazi "hewa"
Nitafafanua kidogo hili linaloitwa wafanyakazi hewa ila naomba isiletwe nongwa kuwa ni utaratibu wangu kumpinga rais! Lah!
Nakumbuka mwaka juzi aliyekuwa katibu mkuu wa NECTA daktari Joyce Ndalichako aliondolewa pale NECTA kwa kile kilichoitwa "likizo ya kufanya utafiti"
Hilo kama halitoshi, pale UDSM (CoET ) na kwingine kote ukienda utakuta wafanyakazi hewa kwelikweli! Siyo hewa kwa maana ya hewa bali wapo kwenye masomo yao ama nje ya nchi ama hapahapa nchini! Wengine wapo kwenye tafiti! Mimi nina rafiki zangu watano pale hawapo! Wapo wanasoma na mshahara unaingia kama kawaida!
Ukienda pale BoT ni kitengo ambacho ni nyeti sana! BoT ni zaidi ya taasisi nyeti za elimu ya juu mfano UDSM! Pale ni kawaida kabisa mfanyakazi kuwa nje ya kituo cha kazi hata mwaka mzima! Pia tukumbuke kuwa pale BoT napo pana watu wenye uelewa wa juu na wengi wao wapo kwenye mizunguko kielemu na kiajira! Swala la BoT ni zaidi ya maswala mengine yote ya taasisi nyingine nchini!
Mimi niliwahi kufanya project pale na kama kawaida yangu nikaanza udodozi wa hapa na pale! Niligundua mambo mengi sana ikiwemo namna ambavyo taasisi ile imejiimarisha katika mfumo wa ulinzi! Mambo kama EPA na ESCROW hayakutokea bahati mbaya! Yale ni maamuzi kutoka ngazi ya juu ya nchi!
Kwa namna hiyo basi, kuna ukweli kuwa wale wanaoitwa wafanyakazi hewa wa pale walikuwa ama kwenye kozi mbalimbali au research! Huo ndiyo utaratibu wa BoT na watu wa pale ni wawekezaji wakubwa kwenye tafiti na elimu! Wengine wako kwenye mizunguko ya kazi!!
Ikiwa Magufuli atataka watu waliokuwa kule ndani wanaoshinda mle na kutoka 24×365 ndiyo wenye mamlaka ya kulipwa mshahara pekee basi no more BoT!
Hata huyo gavana atakayemteua basi atamkosa! Na uchumi utaenda kuleee!!

Hatimaye gavana wa BoT Prof. Beno Ndulu ametoa majibu kwa rais John Magufuli huku akisisitiza kuwa watu wanaongea wasiyoyajua na kuomba apewe majina pamoja na taarifa za wale watu wanaodhani kuwa ni wafanyakazi wasio na umuhimu BoT.
Hayo yanajiri siku moja baada ya rais John Magufuli kumuagiza gavana huyo kuwaondoa ndani ya utumishi wa BoT wafanyakazi wote wasio na umuhimu pamoja na wale wanaojulikana kuwa ni wafanyakazi hewa.
Jana gavana akiongea na vyombo vya habari pamoja na gazeti la MTANZANIA alisema kuwa kila mfanyakazi wa BoT ana umuhimu wake huku akisisitiza kuwa watu wanaongea wasiyoyajua. Prof. Ndulu pia alisisitiza kuwa yule anayedhani kuwa kuna wafanyakazi wasio na umuhimu BoT basi ampelekee majina yao pamoja na taarifa zao!
Hata hivyo gavana huyo aliweka wazi kuwa rais ametoa agizo hivyo ni muhimu kuzingatia agizo la rais lakini akaweka mkazo kuwa BoT itajiridhisha kwa kina kwanza kabla ya kuchukua hatua yoyote ile!