Prof. Baregu aivuruga CHADEMA

Prof. Baregu aivuruga CHADEMA

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2011
Posts
6,811
Reaction score
6,506
*Msimamo wake Katiba Mpya wakitikisa CHADEMA na Watanzania.
*Dk. Slaa asema atahukumiwa Kamati Kuu

MSIMAMO wa mwakilishi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Mwesigwa Baregu, kugomea agizo la chama chake lililomtaka ajiengue katika Tume hiyo ifikapo Aprili 30, umeonekana kukivuruga chama hicho, MTANZANIA Jumapili linaripoti.

Taarifa zilizolifikia gazeti hili na kuthibitishwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, zinaeleza kugoma huko kwa Profesa Baregu kumeilazimisha CHADEMA kufanya maamuzi ya kuitisha Mkutano wa dharura wa Kamati Kuu kwa ajili ya kulijadili suala hilo, ikiwa ni pamoja na kufikia maamuzi ya kichama na hatua za kuchukua.

Hivi karibuni CHADEMA kilisema kuwa hakiridhishwi na mchakato mzima wa kutunga Katiba mpya, baada ya masharti kiliyotoa kwa serikali kikitaka kifanye mabadiliko kutotimizwa, na hivyo kumuagiza mwakilishi wao, Prof. Baregu ajitoe ndani ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kwamba baada ya kujitoa kitaanzisha kampeni ya nchi nzima kuwahamasisha wananchi wasusie mchakato huo.

Hata hivyo, uamuzi huo wa CHADEMA ulipingwa na Prof. Baregu mwenyewe, ambaye alikataa kujitoa kwa hoja kwamba haoni kama kuna mambo yanapindishwa na serikali ndani ya Tume hiyo kama ambavyo chama chake kinadai.

Zikiwa zimepita siku tano (jana) tangu muda aliopewa Prof. Baregu na CHADEMA kujitoa katika Tume kuisha na yeye kugoma, kimesema kuwa suala hilo majibu yake yatapatikana kupitia kikao cha dharura cha Kamati Kuu kitakachoketi muda wowote kuanzia sasa.

Akizungumza na MTANZANIA Jumapili, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, alisema: "Suala hili alilitoa Mwenyekiti wangu na sina cha kuongea, nimekuwa najibu swali hili kwa waandishi mbalimbali wa habari, kwa ufupi jambo hili litazungumzwa kwenye kikao cha Kamati Kuu ya Chama. Sijui muda wala siku kwa sababu bado hakijapangwa."

Wakati Dk. Slaa akiweka msimamo huo wa chama, baadhi ya wafuatiliaji wa masuala ya kisiasa wanamshutumu Prof. Baregu kuwa amekataa kufuata maagizo ya chama chake kwa sababu ya malipo makubwa wanayopatiwa viongozi na wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Taarifa ambazo hazijathibitishwa kutokana na wahusika kugoma kuzungumza zinaeleza kuwa, viongozi na wajumbe wa Tume hiyo kwa siku wanalipwa kiasi cha shilingi laki tano, ambapo kwa mwezi ni karibu na shilingi milioni 12-16.

Pamoja na hilo, juzi wakati Msemaji wa Kambi rasmi ya Upinzani bungeni wa Wizara ya Katiba na Sheria, Tundu Lissu, alipokuwa akiwasilisha hotuba yake kuhusu mpango wa makadirio ya mapato ya fedha ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka wa fedha wa 2013/2014, alihoji matumizi makubwa ya mabilioni ya fedha za wananchi ndani ya Tume hiyo, akidai kuwa yanaashiria harufu mbaya ya ufisadi.

Alisema matumuzi hayo hayaelezeki wala kukubalika kwa misingi ya kisheria na kwa rekodi ya utendaji kazi wa Tume hiyo.

Lissu alihoji Bunge kuombwa tena kuidhinisha shilingi bilioni 33.944, kiasi kile kile kilichoidhinishwa mwaka jana kwa ajili ya matumizi ya Tume kwa mwaka huu wa fedha wa 2013/14.

Katika mwaka wa fedha 2012/2013, Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliidhinishiwa jumla ya shilingi bilioni 33.944 kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 ya Sheria za Tanzania.

Hata hivyo matumizi yake yamezua mashaka na kwa mujibu wa Lissu, kuna ulaji zaidi kwa wajumbe wa Tume hiyo.

Alipoulizwa Prof. Baregu kwamba dhamira ya kugoma kutekeleza maagizo ya chama chake imesukumwa na fedha nyingi anazozipata kutoka katika Tume ya Katiba na si utaifa kama anavyodai, alisema anachokifikiria kuhusu tume hiyo ni kwamba inapewa fungu dogo sana la fedha kuliko tume nyingine zilizopata kuundwa.

"Unajua kuna habari nyingi za uzushi ambazo zimekuwa zikiinyoshea kidole Tume hii, hasa wanasiasa wako mstari wa mbele katika hili, mara utawasikia, Tume tunalipana posho kubwa hadi wengine wanadiriki kusema tunachukua posho ya Sh. 500,000 kwa siku. Wengine utawasikia wanadai tunalipwa mamilioni ya fedha kwa mwezi, laiti kama wangeufahamu ukweli wasingeweza kutamka maneno hayo," alisema Prof. Baregu.

Kuhusu kukaidi kwake agizo la chama chake kilichomtaka ajiengue kwenye Tume ya Katiba, Prof. Baregu, alisema hajui kitu chochote kuhusu hilo kwa sababu hana taarifa zaidi kutoka katika chama chake inayomuelekeza afanye hivyo.

Aliwataka wanasiasa wasiingilie Tume hiyo, kwa sababu inafanya kazi muhimu kwa muktadha wa maisha ya Watanzania.

"Si vizuri tukiwa bado kwenye mchakato kuanza kutoka relini, suala la Katiba ni jambo nyeti na linahitaji mshikamano wa pamoja na si kutishia kujiondoa katika njia ya kuelekea kupata Katiba Mpya.

"Mimi kuwa CHADEMA kunatokana na dhamira yangu, lakini kikubwa ninachokiona ni kuwasaidia wananchi, hivyo hatuna budi kuungana kwa pamoja ili kuzaa Katiba yenye kumsaidia kila Mtanzania," alisema Baregu.

Alisema yeye katika Tume hiyo ni mtaalamu pekee wa masuala ya Sayansi ya siasa, hivyo ana ufahamu umuhimu wake ndani ya mchakato wa kutengeneza Katiba mpya.

Habari kwa hisani ya MTANZANIA Jumapili.
 
Unapomkabidhi mtu NYUNDO usitegemee ataenda kuliweka bila kulifanyia kazi au hawezi kulitumia kukupigia kichwani pale unapomkosea.

A LITTLE CHADEMA boy has turned out to be a MONSTER.

CHADEMA kwa sasa kinaweweseka na jinsi ya kumkabili asije akaivuluga nyumba yao.

IS THIS A MISSION IMPOSSIBLE?.

Yetu ni macho na masikio.
 
Nadhani ungebadilisha heading sio Prof Baregu aivuruga CHADEMA ila ingeleta maana kama ingesomeka CHADEMA WAMVURUGA PROF BAREGU .

Huyu Mzee Prof Baregu anatumia muda wake na akili zake alizojaliwa na MUNGU kusaidia kupata Katiba mpya na sio hao CHADEMA wanaotaka Public sympathy ili waende Ikulu !

Narudia tena Mwaka 2015 CHADEMA wakiingia Ikulu mnichome moto nikiwa hai !
 
Tatizo la viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani ni njaa, hilo halina ubishi kwani hizi kelele nyingi za Dr. Slaa ni kuwaonea donge wenzake, Yeye vipesa vyake vingi lakini vinahesabika

Hata yeye akipata nafasi hamtamsikia kamwe, Wapi maalim Seif, kashakuwa Makamu wa kwanza wa rais kushney! CUF imejifilia mbali.
 
source:Mtanzania

naona wimbo wa ugaidi umechuja sasa tunaingia wa Baregu!

HAKUNA KULALA MPAKA KIELEWEKE 2015 TUNACHUNA NGOZI KABLA YA KUCHINJA!
 
Poor Mtanzania.
Wimbo wao wa Ugaidi umechuja.Pia ule wa Dr Slaa kumuua Zitto nao umechuja.Sasa wameibuka na Baregu.

Hili gazeti ni sawa na Toilet Paper
 
Nani yuko sahihi CHADEMA au Prof?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Kwa hili CHADEMA wametanguliza maslahi binafsi na uchama kuliko utaifa!
Hii ni aibu kubwa,na itawapunguzia sana credit kama chama.
 
Unapomkabidhi mtu NYUNDO usitegemee ataenda kuliweka bila kulifanyia kazi.

A LITTLE CHADEMA boy has turned out to be a MONSTER.

CHADEMA kwa sasa kinaweweseka na jinsi ya kumkabili asije akaivuluga nyumba yao.

IS THIS A MISSION IMPOSSIBLE?.

Yetu ni macho na masikio.


Hata alichokisema Prof. Baregu pamoja na kuwa gazeti lenu limechakachua lakini bado tu hujamuelewa kwa sababu ya utando wa akili yako unaposoma na kujadili mambo ya chama makini hapa nchini cha Chadema.
 
CHADEMA wanatazama maslahi ya chama(VICOBA) chao kwanza. Utaifa na uzalendo hawana mioyoni mwao.
 
Poor Mtanzania.
Wimbo wao wa Ugaidi umechuja.Pia ule wa Dr Slaa kumuua Zitto nao umechuja.Sasa wameibuka na Baregu.

Hili gazeti ni sawa na Toilet Paper

Fisadi Rostam ameacha kupeleka mafungu ya bwerere new habari sasa ili wauze hiyo toilet paper yao inabidi waiandike Chadema.

Zaidi ya Chadema hakuna chama cha siasa kinachouza magazeti kwa sasa hapa nchini.

Bahati nzuri wananchi hawana muda wa kuzitilia manani hizi ''shits'' za mtanzania na nduguze akina jambaleo, habarileo, uhuru na mzalendo.
 
Kwa hili CHADEMA wametanguliza maslahi binafsi na uchama kuliko utaifa!
Hii ni aibu kubwa,na itawapunguzia sana credit kama chama.

Ila CCM iliwatumia barua viongozi wake wote kuakikisha wanawaengua wagombea wa upinzani wao ndio wameweka mbele utaifa?? come on
 
Sasa profesa anamwakilisha nani.?
Au atakua mjumbe wa mahakama.
 
Tatizo la viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani ni njaa, hilo halina ubishi kwani hizi kelele nyingi za Dr. Slaa ni kuwaonea donge wenzake, Yeye vipesa vyake vingi lakini vinahesabika

Hata yeye akipata nafasi hamtamsikia kamwe, Wapi maalim Seif, kashakuwa Makamu wa kwanza wa rais kushney! CUF imejifilia mbali.

mara hii vipesa vyake vinahesabika? Nyie si mlikuwa mnapiga kelele kuwa anajilipa pesa mingi sana?
 
Mi nashauri Aondolewe Baregu na nafasi hiyo Apewe Slaa maana naona ile milion 7.5 aliyoiweka kama sharti la kugombea urais haimtoshi mpika majungu huyu.

Wamezoea kufanya maamuzi chumbani kwa mtei sasa wamekumbana na kisiki.

Hongera Prof.
 
ushauri wangu kwa chadema muacheni baregu aendelee kama mtanzania mwingine yeyote yule wa kawaida isipokuwa musitambue uwepo wake kama anawakilisha chadema ilo ndio pekee yake mliondoe. binafsi ningelipenda kumpa prof.baregu benefit of doubt kuwa labda labda labda kuna kitu anakiona lakini sisi pengine hatukioni ni mtu msomi na anao uchungu wa ninaamini kuwa anao uchungu wa kweli kwani ccm imeshamsumbua sana miaka ya nyuma na nina mashaka kuwa anaweza kukubali kuuza utu wake kwa ajili ya pesa. muondoleeni lile cover la chadema mwacheni ashiriki kama mtaalamu.

la msingi ni kwa chadema kumuacha ashiriki kama mtaalamu mwingine yeyote ambaye angechaguliwa na wamtakie kila la heri na bado ataendelea kuwa mwanachama wao ila maamuzi atakayoyafanyia huko ni yake binafsi na cdm haiusiki.
 
Tatizo la viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani ni njaa, hilo halina ubishi kwani hizi kelele nyingi za Dr. Slaa ni kuwaonea donge wenzake, Yeye vipesa vyake vingi lakini vinahesabika

Hata yeye akipata nafasi hamtamsikia kamwe, Wapi maalim Seif, kashakuwa Makamu wa kwanza wa rais kushney! CUF imejifilia mbali.
Wewe una akili sana bhana kiujumla huwa namaindi sana post zako big up
 
hii post ya lumumba haijadiliki, jadilini wenyewe mkachukue buku 7,

hamjiulizi je wanachodai chadema ni cha msingi??, nyinyi mawaza migogoro tu. siyo kila kunapotokea kutofautiana kimtazamo ni mgogoro,

mbona JK na LOWASA wali tofautiana wakati wa kuvua magamba, pale Lowasa alipodai JK ndo alimtuma aipe dhabuni Kampuni ya richmond,

nyie mnawaza buku 7tu, ni umaskini wa kipato na mawazo. pole ni sana
 
Back
Top Bottom