huo ndo upuuzi kabisa na UMBUMBUMBU uliokubuhu! Hivi kweli mtu na akili zako humwamini Mungu wa kweli? Mungu yule alotuumba na Mungu yule anayetuvumilia kwa dhañbi na makosa yetu kila leo! Hii inashangaza sana kuona mtu na elimu yake kubwa lakini anakuwa kama mwendawazimu vile, how comes mwanadamu ulieumbwa na udongo leo hii usimwamini baba yako alokuumba? In Spirutual research taifa la urusi lilianguka kiutani utani koz hawakumwamini Mungu wa kweli hatimaye mahasimu wao wa magharibi waliijua siri ya mafanikio ambayo ni kumwamini Mungu wa kweli'
MTU YEYOTE YULE HATA KAMA AWE NA UMAARUFU NA ELIMU KUBWA KIASI GANI ALAFU HAMWAMINI MUMGU WA KWELI, HUYO NI MJINGA NA MPUMBAVU KABISA KWANI NI HERI UWE MASKINI NA HUJASOMA LAKINI UNAMWAMINI MUNGU"
Mungu wa kweli ni yupi? Wa waislamu? Wa Wakristo? Wa Wayahudi? Wa Wa Buda? Wa Wazoroasti? Wa Warasta? Wa Wanyeramba? Wa Wanavajo?
Unajuaje kama katuumba? Unajua au unaamini? Unajua tofauti kati ya kujua na kuamini?
Kama mungu katuumba na kumjua ni kwa neema, utatulaumu vipi kwa dhambi? Kama mungu kaumba vyote, je kaumba dhambi nayo? Uwezo wa kutenda dhambi umetoka wapi? Kama haujatoka kwa mungu, mungu hakuumba vyote. Kama umetoka kwa mungu, utaweza kumlaumu binadamu kwa kutenda dhambi?
Kati ya anayeuliza maswali magumu na asiyekubali majibu ya juu juu na yule anayelazimisha majibu ya mapokeo yasiyo na mshiko wala yasiyojitosheleza, nani anakaribia uandawazimu?
Una ushahidi gani kwamba mwanadamu kaumbwa kwa udongo?
Una hakika kwamba Urusi ilianguka kwa sababu hawakumuamini mungu?
Mbona Uchina ni taifa lisiloamini mungu na mpaka leo linatisha kiuchumi? Mbona unachagua chagua cha kusema katika hili? Ukisema tu yanayokubaliana na hoja yako. Mbona European Union leo wana taabu za kiuchumi ingawa wanaamini mungu, na taifa la China haliamini mungu lakini ndilo hata wachumi wanasema Wachina wanaweza kuwakopesha hao wazungu?
Mungu wa kweli unamtajataja bila ya kumuelezea, huyu mungu wa kweli ni yupi? Ana characteristics gani?
Ndiye huyu huyu tuliyeletewa na wakoloni walipokuwa wanataka kutunyanganya nchi yetu?
Ndiye huyu huyu aliyetumika katika utumwa?
Ndiye huyu huyu aliyetuambia kwamba anawapendelea watu wake "wateule" wana wa Israel na sie wengine Wamakonde ni pretty much "second class citizens" katika macho yake?