Taifa linahitaji watu wachapa kazi, watu wenye misimamo katika mambo ambayo wanayaamini na binafsi ninaona Prof Asad ana Sifa ambazo naweza kudiriki kusema raisi wetu akimaliza mda wake ni mtu anayeweza kuendeleza mapambano haya aliyoyaanzisha raisi wa awamu ya Tano.
Nakumbuka waliposema CAG Utto anastaafu wengi tulijiuliza kama angeweza kupatikana mtu anayeweza kuvaa viatu vyake. Alipoteuliwa Prof Asad kuwa CAG wengi hatukumjua ila kiukweli amefanikiwa kuendeleza juhudi alizokuwa akifanya Utto na kila mtanzania leo anaridhika kwa kile anachokifanya kama CAG.
Juzi juzi CAG alihojiwa katika redio ya umoja wa mataifa akaulizwa "kila mara mmekuwa mkitoa ripoti zinazoonyesha mapungufu lakini hakuna hatua zinazoonekana kuchukuliwa juu ya mapungufu mnayoyaibua katika ripoti zenu"
na yeye akajibu "kazi yetu ni kufanya ukaguzi na kutoa ripoti na ni kazi ya bunge kufanyia kazi ripoti zetu ili kuhakikisha hatua zinachukuliwa na kama hakuna hatua zinazochukuliwa huo ni udhaifu wa bunge"
Hili ni jibu fasaha kwa watu makini.
watanzania tumechoshwa na tabia za wanasiasa waliowengi wanaotafuta daima kupaka viongozi wenzao mafuta kwa mgongo wa chupa. Kuna uzembe sehemu fulani unasema wazi na hili ndilo analolifanya raisi wetu kwa sasa ingawaje yeye anakwenda mbali zaidi na kutumbua pia.
wanasiasa waliolelewa na siasa zetu zilizotukuza za kuamini kiongozi huwa hakosei, wananchi wakilalamika unatafuta maneno ya kuwaambia waridhike na sio kuhoji kiongozi,
Kitendo cha mtu mkubwa kama aliyejitokeza kupambana na CAG kupiga mkwara mkali pamoja na mbinu nyingi lakini CAG akabaki na msimamo wake uleule wa kuamini katika kile anachokiamini na kuendelea kukisimamia. " Hii ni kariba ya hali ya juu ambayo kama mtu mwenye kariba hii anaweza kuwa na machungu na nchi yake ni mtu mwafaka sana kupewa uongozi wa juu"
Tatizo kubwa la viongozi wengi ni kutokujiamini kwa waliomzunguka wakisema jambo au kupinga jambo basi ingawa yeye ndiye mwenye maamuzi lakini anabaki kukaa kimya hata kwa mambo ya kipuuzi ya wazi.
ingawaje akitokea mtu mwenye kariba hiyo akawa mbinafsi asiye na machungu na nchi mtu huyo huwa anawatesa sana watu na kufanya vitu vya kipuuzi na watu wote hakuna wa kumbadilisha.
Tanzania kama nchi tusipende sana kuendekeza tabia za wanasiasa wengi za "bagenda ngenda bagaruka ngaruka" yaani wanasiasa wengi wanakuwa bendera hufuata upepo wanachosapoti wenzangu ndicho nasapoti na wanachopinga wenzangu ndicho napinga.
Tuangalie watu makini wanaoweza kutufikisha kwenye malengo ya taifa letu na Prof Asad nimeona ni mtu sahihili