Prof. Assad amlipua Magufuli kwa ufisadi uuzaji wa nyumba za Serikali

ufisadi wakuuza nyumba za Jamhuri nimkubwa sana kupata kutokea,nina uwakika bomu hili likija lipuka,madhara yake kisiasa yatasambaaa kuanzia Kwa mkapa,mawaziri,wakuu wa mikoa,wilaya, viongozi wa na makada mbalimbali wa xxm, na vyama vingine vya upinzani, ndio Mana viongozi wengi aidha wa upinzani au toka chama tawala hawalizingumziii, Prof Safari ashawahi kuliongelea hakupata support kubwa nje na ndani ya upinzani, ktk ufisadi huu wakutapanya Mali ya Jamhuri km kuku alievamia mahindi yaliyo anikwa hii ni kwasabb ufisadi huu umewanasa wengi....
 
Kama wewe ndiye Magufuli ama ni ndugu yake ama mnufaika wa huo ujasiria-siasa (political entrepreneurship) , tambua kwamba ni dhambi pekee ambayo watanzania hawatakaa waisamehe!


Huyu bwana hajamaliza hata mwezi kazini tayari anashambulia wanasiasa.

Prof.Assad amehojiwa na idhaa ya Kiswahili ya UN, na kutoa madai kwamba Tanzania kuna tatizo la "POLITICAL ENTREPRENEURSHIP."

Anadai watu wanaendekeza faida binafsi ktk maamuzi yao wakiwa madarakani.

Amekwenda mbali na kusema ule mradi wa MAGUFULI wa kuuza NYUMBA ZA SERIKALI ni mfano wa "POLITICAL ENTREPRENEURSHIP."

Kwa kweli Professor atakaporudi nyumbani anapaswa at least aseme kuwa alinukuliwa vibaya, hata kama kuna ushahidi wa sauti yake.

Mahojiano yake yapo hapa chini, lakini specifically unaweza kuanzia dakika ya 6.

Tutatekeleza majukumu kukidhi matarajio: Profesa Assad | Idhaa ya Redio ya UM



cc Ritz, Pasco, Sangarara, Tetty, VUTA-NKUVUTE, Nguruvi3, NasDaz, Mdondoaji
 
..tatizo ni kuyasema mambo hayo.

..je, ataweza ku-match maneno na vitendo?

..je, atapata support ya kutekeleza kazi yake vile anavyoamini na alivyofundishwa?

..hivi unaelewa kwamba RAISI aliyemteua ameuziwa hizo nyumba za serikali, halafu PROF.ASSAD anasema mradi wa kuuza nyumba za serikali ni "POLITICAL ENTREPRENEURSHIP"?!

cc Kubwajinga, Barubaru, NasDaz, Mdondoaji, ZeMarcopolo

Hivi mnataka uovu usikemewe kwa kuwa tu ati na kiongozi mkubwa naye ameshiriki kuutenda?! Mnataka kuaminisha watu kwamba viongozi hawatendi makosa?
 
Last edited by a moderator:
Nakubaliana na professor Assad Kama kuna ugaidi uliofanywa na serikali ni kuuza nyumba za serikali. Nasikitika Sana pale ninapowaona Government attornies wanapokaa mitaani. Wanatokwa na jasho na suti zao nyeusi. Unakuta hata Mkurugenzi Wa wizara au halmashauri anaishi in a pathetic and horrible resident. Huu ni uhuni uliopitiliza Kiwango katika taifa hili. Kitendo hili kimewafanya watumishi wengi kupoteze uzalendo thidi ya nchi yao. Hizi nyumba nivyema zikarudishwa Kwa umma ili wafanyakazi watambue kuwa wanaitumikia umma. Leo hii kickbacks zimeongezeka kwenye miradi Kwa sababu watu wanajitahidi kupata mgao ili kuwawezesha kujenga makaazi hapo kuna watumishi ambao naturally wanahusudu rushwa!

Nakubaliana na wewe kuwa uuzaji wa zile nyumba ulikuea ni kosa la ajabu hasa ukizingatia kuwa uliwabagua wananchi wa kawaida ambao nao walikuwa na haki ya kuzipata. Kwa nini watumishi wa serikali tu?

Natofautiana nawe kuhusu watumishi wakuu kukaa mitaani kwetu. Inatakiwa wakae huko ili wajue adha wanazokumbana nazo wananchi wa kawaida. Wataelewa kwa nini wananchi wanataka maji, mitaa, na barabara. Katika nchi nyingine hata mawaziri wanaishi na wananchi.
 
ufisadi wakuuza nyumba za Jamhuri nimkubwa sana kupata kutokea,nina uwakika bomu hili likija lipuka,madhara yake kisiasa yatasambaaa kuanzia Kwa mkapa,mawaziri,wakuu wa mikoa,wilaya, viongozi wa na makada mbalimbali wa xxm, na vyama vingine vya upinzani, ndio Mana viongozi wengi aidha wa upinzani au toka chama tawala hawalizingumziii, Prof Safari ashawahi kuliongelea hakupata support kubwa nje na ndani ya upinzani, ktk ufisadi huu wakutapanya Mali ya Jamhuri km kuku alievamia mahindi yaliyo anikwa hii ni kwasabb ufisadi huu umewanasa wengi....

Waliozinunua waanze kutafuta mahali kuishi kwani ni lazima zote zirejeshwe serikalini na walioziuza waanze kurejesha fedha za watu.
 
Waliozinunua waanze kutafuta mahali kuishi kwani ni lazima zote zirejeshwe serikalini na walioziuza waanze kurejesha fedha za watu.
kaka nyumba zimeishapigwa nyundo...ni vita ngumu sana kuzirudisha nyuma za watu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania...
 
Prof Assad hajaitendea haki neno entrepreneurship hasa linapokuja swala LA wanasiasa wa tz Hawaii no watu ambao hawana dira hivyo hawapaswi kuitwa wajasiriamali
 
Joka Kuu,

Professor Assad mie sina shaka nae just wait and see have patience brother you will get to know him.
 
MIMI SI Cag lakini najua nyumba zimeizwa kifisadi na kwaubinafsi, walio nunua wanauza kwe bei ya juu mno mbaka bilioni 3 wakati walinunua kwa bei ya kutupwa ya milioni 12, ni bora ingeuza serikali kwa bilioni 3 Maana wangeweza kujenga mpya maeneo mengine
 
Another prof. muhongo (muongo?) in the making? muhongo alianza kwa gia kama hizo hizo!
The difference between muhongo na Assad ni timing of appointment, inayomfanya muhongo asimame zaidi kwa leadership ya Leo iliyomjenga, wakati Assad anahitaji consensus ya future administration itakayo mtunza
 
Huyu magufuli hata contractors wa zawadi anataka kuwamaliza hawalipi wanafanya kazi baada wanaambiwa hela hakuna huku kila gali I napo weka mafuta lita moja unachangia tsh 120 kwa lt hela hizo zina kwenda wapi inaitwa road funds
 
kaka nyumba zimeishapigwa nyundo...ni vita ngumu sana kuzirudisha nyuma za watu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania...

Ni kweli ccm hawawezi kuzirejesha lkn eataondoka na ninaamini UKAWA wataibatilisha hiyo Sera mbaya pamoja ile ya viwanja vya michezo kumilikishwa ccm kinyemela!
 
Nadhani kwa mtu mwenye kuchambua masuala ya kisiasa hili wala halihitaji mjadala mrefu!.

Waziri Magufuri alikuwa ni msimamizi wa maamuzi yaliyofanywa na Baraza la Mawaziri kwa sababu yalikuwa yanahusu eneo lake la kazi.

Hakuna sehemu ambayo serikali ilisema usimamizi wake aliufanya kimakosa, kwa lugha nyingine, alichokisimamia Waziri Magufuli ndicho kile ambacho Baraza la Mawaziri lilimtaka akisimamie.

Ninampongeza kwa kuifanya kazi yake kwa ufanisi kama ilivyokubaliwa na Baraza la Mawaziri!.

Hii dhana ya kusema nyumba ziliuzwa kwa bei ya kutupa ni mtazamo wako lakini siyo mtazamo wa serikali. Kwa maana nyingine, hiyo ndiyo bei iliyokubaliwa na serikali kupitia Baraza la Mawaziri kwa sababu hakuna sehemu ambayo serikali inalalamika kuhusiana na usimamizi huo.

Nikiangalia kwenye jicho la pili, naona hoja yako haina tofauti sana na wale wanaomlaumu Mhe. Zitto kuhusiana na repoti ya PAC badala ya kuilaumu Kamati ya PAC.

Serikali (Baraza la mawaziri) unalolizungumzia hapa ndio wanufaika wa uamuzi huo watalalamikaje? Wataanzaje kulalamika dhidi ya manufaa yao yaliyolengwa na maamuzi hayo yaliyozingatia maslahi yao binafsi dhidi ya maslahi ya umma?
 
watu wanaoongea straight forward kama huyu bwana huwa hawakai sana serikalini.....atazushiwa udalali sasa hivi kama mwenzie muhongo kwa kutetea watanzania.

udalali tu??!! mbona c ishu me naogopa familia yake isije baki yatima kama ya waziri wa fedha wa ukweli ktk historia ya wizara hio MGIMWA! mara walimwita mzigo wakaona haitosh wakampatia escape velocity wakamwondoa duniani magamba hawa
 
kaka nyumba zimeishapigwa nyundo...ni vita ngumu sana kuzirudisha nyuma za watu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania...

Mkataba wa hizo nyumba ni miaka 25 ni ya serikali, baada ya hapo mnunuaji anazimiliki. Kinachofanyika sasa ni kusubiri miaka 25 ipite. Mpaka sasa hiyo miaka ni bada. Mafisadi hawataachia ngazi mpaka kipindo hicho kifikiwe

 
Hii ndo faida ya kuwa na wasomi walio straight forward kama Asaad. Na kilio kikubwa kitasikika kwenye report ya ukaguzi hapo mwakani.

Nchi za wenzetu walioendelea, hawawezi kumpa mtu madaraka makubwa kama ni maskini, wanaogopa atakapokuwa ofisini ataanza kwanza kurekebisha hali yake ili afanane na wenzake. Prof Asaad anaonekana kujivunia taaluma na weredi wake. rangi nyeusi anaiita hivyo na rangi nyeupe anaiita hivyo.
 
Magufuli hachafuliki, mnapoteza muda wenu bure
Pinga tuhuma alizotuhumiwa kwa ushahidi siyo unasema tu hawezi kuchafuliwa. Nyumba za serikali aliziuza au hakuuza na kama aliuza kwasababu gani,wakati wafanya kazi wa serikali hawana nyumba za kutosha.
 
Mkataba wa hizo nyumba ni miaka 25 ni ya serikali, baada ya hapo mnunuaji anazimiliki. Kinachofanyika sasa ni kusubiri miaka 25 ipite. Mpaka sasa hiyo miaka ni bada. Mafisadi hawataachia ngazi mpaka kipindo hicho kifikiwe


Siku inakuja tutakaporudisha nyumba za serikali. Na akina magufuli watalipa hujuma waliyotufanyia watanzania wote kwa ujumla wetu.
 
udalali tu??!! mbona c ishu me naogopa familia yake isije baki yatima kama ya waziri wa fedha wa ukweli ktk historia ya wizara hio MGIMWA! mara walimwita mzigo wakaona haitosh wakampatia escape velocity wakamwondoa duniani magamba hawa

Kwa kifupi hakukuwa na sababu ya kuuza nyumba serikali ila ubinafsi ulitawala. Hivi sasa zimejengwa nyumba ghorofa mpaka 15 ambazo hakuna mtumishi anayezitaka kwani zina kero kibao za maji,Umeme, uchafu kwenye ngazi, hata kuanika nguo ni shida no privacy nk. Ni kama ghetto.Iko siku nyumba zitarudi kwani wahusika wamepeana kifisadi na watawala watawajibika kwa matendo yao hata kama ni wastaafu!
 
Back
Top Bottom