Prof. Anna Tibaijuka, kuza heshima yako kwa hili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Prof. Anna Tibaijuka, kuza heshima yako kwa hili

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ntamaholo, Dec 25, 2011.

 1. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #1
  Dec 25, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  Hbr. Wanajamvi.

  Jana nilikuwa kwenye msiba, ambpo pamoja na utani wa makabila yetu, SIASA huwa ni ajenda mhimu watu wenye uelewa tofauti wanapokutana. Kati ya vitu tlivyoongea, kimoja kimenivutia na kufikiria kukileta kwenu ili kukifikisha kwa wahusika kwa urahisi zaidi. Kitu hicho ni sera ya ardhi.

  Ni wazi kuwa, tunayo sera na sheria ya ardhi, ambayo imetoa mamlaka ya utoaji hatimiliki za kimila kwa serikali za mitaa. Lakini malengo ya utoaji hatimiliki, upanuliwe na kuwekewa sheria nzito ili kuzuia uuzaji holela wa aridhi. Maoni ya wananzengo yalikuwa kama ifuatavyo:-

  (a) Aridhi yote ipimwe na ipewe hatimiliki. serikali iandae mipango kamambe ya kuhakikisha ardhi yote imepimwa kama walivyo RWANDA, BOTSWANA, LIBYA na wananchi kumilikishwa n.k
  (b) Iundwe sheria kali ya kudhibiti uuzaji wa ardhi hasa kwa wageni ili wanapokuja kuwekeza, wenye ardhi, tukubaliane kumiliki hisa za kampuni kwa thamani ya ardhi yetu. Hii itasaidia kuwaingiza wenye ardhi kwenye biashara kubwa tena zenye faida.
  (d) Serikali ibaki na jukumu la kuwalea wote wenye ardhi, na mtu akifanya kinyume, basi sheria ichukue mkondo wake.

  Ilivyo sasa hivi, ardhi inatambulika ni mali ya umma. Viongozi mda wowote wanamamlaka ya kunyang'anya ardhi ya mtu kwa kisingizio cha maslahi ya umma, wakati ukweli umma haunufaiki. Sehemu zote za migodi, watu wamenyang'anywa ardhi zao na hwajalipwa fidia na hawanifaiki kwa lolote.

  kama wangemilikishwa ardhi ile, wawekezaji wangelazimika kugawa hisa kwa wamiliki wa ardhi na hivyo kuwawezesha wenyeji kumiliki hisa katika uchimbaji wa madini.

  Tibaijuka, ni nafasi yako, ukifanikiwa hili, utakumbukwa milele, kama huwezi, vyama mbadala wekeni suala hili katika ajenda zenu ili 2015, utekelezaji wake uanze.

  nawasilisha.
   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  Dec 25, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  hili linafanyika mkuu,
   
 3. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #3
  Dec 25, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  pamoja mkuu, uko fasta heshima kwako muungwana.
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Dec 25, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Thanks nafahamu kuna mikoa ilianza kama vile ruvuma na tabora/singida na ni zoezi zuri sana... ila ningependa sana kama wizara ingeimarisha public private partnership kwenye zoezi kwani ingeharakisha zoezi na ku-add value sana ya ardhi kwa kupunguza ukiritimba uliopo sasa

  binafsi naamini kabisa watendaji wa wizara ya ardhi ndio wanaoharibu zoezi zima la land management nchini kwa mifano midogo tu kama ile ya viwanja wanavyopima na kuuza vocha (kujiuzia to say the least), na baadae kulangua kwa few individuals who also langua to others, in that case unakuta maeneo mengi yaliyopimwa na serikali yanaendelea kuuzwa na bila kuendelezwa hata miaka kumi baada ya kupimwa na kugawiwa. huu pia ni uhujumu uchumi

  we have people, resources, technical skills, serikali ingefikiria kutumia PPP kukamilisha zoezi
   
 5. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #5
  Dec 25, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  nchi zinazojali ardhi, hawaruhusu uuzaji holela, hata kama utanunua, unajipalia makaa, yaani umetapeliwa. Kinachotakiwa ni serikali kuwa nania ya dhat, kuwamilikisha watu au kijiji, ili hawa wezi wanaotuibia wakija na mbwembwe za kuwekeza, tunawaambia sisi hatuna pesa, hatuna vifaa, lakini tuna watu na tuna ardhi. inapigwa hesabu labda kwa kila hekta moja, inakuwa na thamani ya dolar 50,000 theni kama uwekezaji utagharimu dolar 2,000,000 zinapigwa hesabu ili vijiji vijue vitakuwa na hisa ngapi katika uwekezaji.

  kama haya yakifanyika, watu wengi watahamia vijijini kwani kila kitu kizuri kitapatikana huko
   
Loading...